Bosnia na Herzegovina

(Elekezwa kutoka Bosnia - Herzegovina)


Bosnia na Herzegovina (Bosna i Hercegovina au Босна и Херцеговина) ni nchi ya Ulaya kusini mashariki kwenye rasi ya Balkani. Mara nyingi huitwa kwa kifupi "Bosnia" tu na watu wake "Wabosnia". Ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi mwaka 1992.

Bosna i Hercegovina
Босна и Херцеговина

Bosnia na Herzegovina
Bendera ya Bosnia na Herzegovina Nembo ya Bosnia na Herzegovina
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: "Intermeco"
Lokeshen ya Bosnia na Herzegovina
Mji mkuu Sarajevo
43°52′ N 18°25′ E
Mji mkubwa nchini Sarajevo
Lugha rasmi Kibosnia, Kikroatia, Kiserbia
Serikali
Marais

Mwenyekiti wa
halmashauri ya mawaziri
Jamhuri
Šefik Džaferović (Mbosnia)
Milorad Dodik 1(Mserbia)
Željko Komšić (Mkroatia)
Zoran Tegeltija
Uhuru
Ilitambuliwa

6 Aprili 1992
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
51,197 km² (128)
--
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - 2014 sensa
 - Msongamano wa watu
 
4,498,9762 (ya 1273)
3,871,643[1]
76/km² (ya 1163)
Fedha Convertible mark
pamoja na Euro (BAM4)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .ba
Kodi ya simu +387

-

1 Maraisi watatu wanaobadilishanan
2 Kadirio ya CIA World Factbook [2].


Eneo lake ni km² 51,129 linalokaliwa na wakazi karibu milioni nne.

Mji mkuu ni Sarayevo.

Kati ya wakazi kuna vikundi vitatu vinavyotofautiana kiutamaduni na kidini: Wabosnia (48%), Waserbia (37.1%) na Wakroatia (14.3%). Wanadai ya kwamba lugha zao ni tofauti, lakini hali halisi ni lugha ileile ya Kislavoni. Wakati wa Yugoslavia iliitwa "Kiserbokroatia". Tofauti ziko kwa sababu Wabosnia hutazamiwa kuwa Waislamu, Waserbia kuwa Waorthodoksi na Wakroatia kuwa Wakristo Wakatoliki.

Nchi ina vitengo viwili: Shirikisho la Bosnia na Herzegovina linalounganisha maeneo ya Waislamu na ya Wakatoliki na Republika Srpska au eneo la Waserbia Waorthodoksi.

Ramani ya Bosnia na Herzegovina

Historia

hariri

Bosnia ilitokea kama eneo la pekee wakati wa Karne za kati chini ya utawala wa Dola la Uturuki.

Jina la Bosnia limetokana na mto Bosna. Jina la Herzegovina lilitokana na watemi wa kusini katika eneo la mji wa Mostar waliotumia cheo cha Kijerumani cha "Herzog" na eneo lao liliitwa "nchi ya Herzog" au "Herzegovina".

Utawala wa Kiislamu ulisababisha kugeuka kwa sehemu kubwa ya wakazi kuwa Waislamu walioendelea kutumia lugha yao ya Kislavoni.

Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Uturuki katika karne ya 19 utawala wa nchi ulifika mikononi mwa Austria-Hungaria.

Vita kuu ya kwanza ya dunia ilisababishwa mjini Sarayevo kutokana na mauaji ya mfalme mteule wa Austria na mke wake.

Kati ya 1918 na 1992 Bosnia na Herzegovina ilikuwa jimbo la Yugoslavia.

Baada ya uhuru ilitokea vita kali kwa sababu sehemu ya Waserbia na ya Wakroatia walitaka kuunganisha nchi au sehemu zake na Serbia au Kroatia. Wakazi wengi walifukuzwa nyumbani kwao kufuatana na maeneo ambako wanamgambo Waserbia au Wakroatia walitawala kufukuza wote wengine.

Jumuiya ya kimataifa iliingilia kati na kuwalazimisha washiriki kukubali amani katika mkataba wa Dayton wa 1995.

Mamlaka kuu haimo mikononi mwa serikali ya wenyeji bali mikononi mwa Kamishna Mkuu kwa Bosnia na Herzegovina anayeteuliwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Ana mamlaka ya kubatilisha sheria zilizoamuliwa na bunge, pia kuachisha mawaziri kazi.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bosnia na Herzegovina kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.