Visiwa vya Falkland

(Elekezwa kutoka Falkland Islands)

Visiwa vya Falkland (kwa Kiingereza: Falkland Islands; kwa Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban km 450 mbele ya pwani ya Argentina.

Visiwa vya Falkland
Kanisa kuu la Christchurch, Stanley.
Nyumba ya mkulima katika nyika za Falkland.

Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake. Hivyo mwaka 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita vifupi vya wiki 6 Argentina ilishindwa; takriban wanajeshi 1,000 waliuawa.

Jiografia hariri

Funguvisiwa lina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban km² 6,000. Mwinuko mkubwa ni mlima Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) wenye kimo cha mita 708 juu ya uwiano wa bahari.

Hali ya hewa ni baridi na kuna mvua nyingi. Halijoto ya wastani ni 5 °C pekee. Kwa sababu hiyo mimea ni hasa nyasi; kutokana na baridi miti haizidi kimo cha mita 1.

Watu hariri

Idadi ya wakazi imepita 3,000 na wote hao ni Waingereza wanaosema Kiingereza. Wanajipatia riziki zao kwa uvuvi na ufugaji wa kondoo.

Upande wa dini, 66% ni Wakristo, hasa Waanglikana, lakini pia Wakatoliki na wengineo. 32% hawana dini yoyote.

Mji pekee ambao ni pia makao makuu ya utawala ni Port Stanley kwenye kisiwa cha mashariki wenye wakazi 2,100. Pamoja na wakazi kuna wanajeshi Waingereza 1,500.

Barabara ya lami ya pekee kisiwani ni ile inayounganisha Stanley na kituo cha kijeshi kwa umbali wa kilomita 50.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Falkland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.