Historia ya Kroatia

Historia ya Kroatia inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Kroatia.

Maeneo ya Kroatia yalikuwa sehemu ya Illyria wakati wa Dola la Roma na kutawaliwa kama mikoa ya dola hilo.

Mnamo mwaka 395 Dola la Roma liligawiwa katika sehemu ya magharibi na sehemu ya mashariki. Sehemu hizo mbili ziliendela baadaye kwa namna mbili tofauti.

Kuanzia mwaka 600 makabila ya Waslavoni walianza kuingia na kukaa. Wakroatia waliunda utemi wao wa kwanza. Kroatia ilikuwa upande wa magharibi wa mstari wa mwaka 395, hivyo chini ya athira ya Kanisa Katoliki, ikaendelea kuwa sehemu ya utamaduni wa Ulaya ya magharibi. Kumbe Waslavoni wa jirani wanaotumia lugha ileile waliishi chini ya athira ya Bizanti na Kanisa la Kiorthodoksi, hivyo kuendelea kama sehemu ya Ulaya ya Mashariki na kuitwa Waserbia.

Mtemi Tomislav (910928) alichukua cheo cha mfalme mwaka 925. Huo Ufalme wa Kroatia uliendelea hadi mwaka 1102. Wakati ule mfalme wa mwisho hakuwa tena wa watoto na mfalme wa Hungaria alichaguliwa kuwa mfalme wa Kroatia pia. Maungano hayo na Hungaria yaliendelea kwa karne nyingi.

Tangu maungano wa Hungaria na Austria ni Kaisari wa Austria aliyekuwa na cheo cha mfalme wa Krotia hadi vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918).

Mwaka 1918 Dola la Austria liliporomoka. Waslavoni wa Kusini waliamua kuunda ufalme wa pamoja kwa jina la Yugoslavia. Kroatia ilikuwa sehemu ya Yugoslavia kuanzia 1918; kwanza katika ufalme wa Yugoslavia, halafu katika jamhuri ya kisoshalisti ya Yugoslavia hadi 1991.

Miaka 1990 / 1991 Yugoslavia iliporomoka na majimbo yake zilitafuta uhuru kama nchi za kujitegemea.

Kroatia ilikuwa kati ya majimbo ya Yugoslavia na ilipata uhuru wake mwaka 1991.

Imejiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Julai 2013.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Kroatia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.