Kibla (kutoka Kiarabu: قبلة qiblah kwa maana ya "mwelekeo") ni neno la kutaja mwelekeo wa sala katika dini ya Uislamu. Mwislamu anatakiwa kusali mara tano kila siku akitazama upande wa Makka.

Mihrabu sahili nchini Misri inaonyesha kibla.
Ramani ya Dunia inayoonyesha upande wa kibla kutoka pande zote.

Misikiti huwa na kidaka kinachoitwa mihrabu kwenye ukuta. Mihrabu inaonyesha upande wa kibla.

Katika historia ya Uislamu kibla ya kwanza ilielekea Yerusalemu. Kilibadilishwa kwa njia ya ufunuo mpya kuelekea hekalu la Kaaba mjini Makka.