Kingamwili

(Elekezwa kutoka Kinga (tiba))

Kingamwili (pia kingamaradhi, kwa Kiingereza immunity, kutoka Kilatini immunis, lenye maana ya msamaha kutoka malipo ya kodi, huduma ya kijeshi au huduma nyingine za umma[1]) ni uwezo wa mwili wa kujihami dhidi ya pathojeni (bakteria, virusi, fungi au vidubini vingine vinavyoweza kusababisha magonjwa). Kinga nzuri inazuia maambukizi, ugonjwa, au uvamizi wa kibiolojia usiotakiwa katika mwili.

Kingamwili inahusisha vijenzi mahususi na visivyo mahususi. Vijenzi visivyo mahususi hufanya kazi ama kama vizuizi au kutoa visababishi magonjwa mbalimbali bila kujali umahususi wa antijeni. Vijenzi vingine vya mfumo wa kinga hujitohoa kwa kila ugonjwa vinavyokabiliana nao na vinaweza kuzalisha kinga maalum kwa visababishi magonjwa.

Kinga tohozi mara nyingi hugawanywa katika aina mbili kuu kulingana na jinsi kinga ilivyoletwa. Kinga inayopatikana kimaumbile hutokea kupitia mgusano na kikolezo kinachosababisha ugonjwa, wakati ambapo mgusano haukuwa makusudi, lakini kinga inayopatikana kwa kughushi hutokea tu kwa vitendo vya makusudi kama vile chanjo. Kinga zote mbili zinaweza kugawanywa zaidi kutegemea na kama kinga imesababishwa katika kimelea au ilihamishwa kimyakimya kutoka kwa kimelea mwenye kingamaradhi.

Kinga tulivu inapatikana kwa njia ya uhamisho wa kingamwili au seli za T zilizoamilishwa kutoka kwa kimelea mwenye kingamaradhi, na inadumu muda mfupi - kwa kawaida miezi michache tu - lakini kinga tendi husababishwa katika kimelea mwenyewe na antijeni, na hudumu muda mrefu zaidi, wakati mwingine kwa maisha yote. Mchoro wa hapa chini ni muhtasari wa migawanyiko hii ya kinga.

Mgawanyiko zaidi wa kinga tohozi unajulikana kwa seli husika; kinga katika ugiligili ni kipengele cha kinga kinachoibuliwa na kingamwili zilizonyunyizwa, wakati ambapo ulinzi unaotolewa na kinga iliyoibuliwa na seli inahusisha limfosaiti-T pekee. Kinga katika ugiligili iko hai wakati kiumbehai kinazalisha kingamwili zake mwenyewe, na tulivu wakati kingamwili zinahamishwa kati ya watu binafsi. Vile vile, kinga iliyoibuliwa na seli ni hai wakati seli-T za kiumbehai zimechangamshwa na tulivu wakati seli T zinatoka kwa kiumbehai mwingine.

Historia ya nadharia za kinga

hariri
 
Mfano wa janga la kipindupindu la karne ya 19.

Dhana ya kinga imevutia watu kwa miaka elfu kadhaa. Mtazamo wa kale wa ugonjwa ni kwamba ulitokana na nguvu zisizo za kawaida, na kwamba ugonjwa ulikuwa aina ya adhabu ya tambiko kwa "matendo mabaya" au "mawazo maovu" inayoletwa kwa nafsi na miungu au maadui wa mtu. [2]

Kati ya wakati wa Hippokrates na karne ya 19, ambapo misingi ya mbinu za kisayansi iliwekwa, magonjwa yalihusishwa na mabadiliko au kutolingana katika moja ya giligili nne (damu, kohozi, nyongo njano au nyongo nyeusi). [3] Nadharia ya miasma, iliyosema kwamba magonjwa kama vile kipindupindu au Tauni Nyeusi yalisababishwa na miasma, aina hatari ya "hewa mbaya" [2]ilikuwa maarufu wakati huo. Ikiwa mtu angefichuliwa kwa miasma, angeweza kupata ugonjwa.

Maelezo ya kwanza kuandikwa ya dhana ya kinga yanaweza kuwa yalitolewa na Wathusaidi wa Athene ambao, mwaka wa 430 KK, walieleza kuwa wakati ugonjwa ulipoathiri mji huo "wagonjwa na waliokuwa mahututi walihudumiwa na wale waliokuwa wamepona, kwa sababu walijua uelekeo wa ugonjwa na hawakuwa na hofu. Kwa maana hakuna mtu aliyepata ugonjwa mara ya pili, au si kwa matokeo mbaya." [1] Neno "wenye kingamaradhi", pia hupatikana katika shairi la kishujaa "Pharsalia" lililoandikwa mnamo 60 KK na mshairi Marcus Annaeus Lucanus kuelezea upinzani wa kabila la Afrika Kaskazini kwa sumu ya nyoka. [3]

Maelezo ya kwanza ya kiafya ya kinga ambayo yalitokana na kiumbehai maalumu mwenye kusababisha ugonjwa huenda ni Kitab fi al-jadari wa-al-hasbah (Tasnifu juu ya Ndui na Surua, ilitafsiriwa 1848 [4]) yaliyoandikwa na daktari wa Kiislamu Al-Razi katika karne ya 9. Katika tasnifu, Al Razi anaeleza wasilisho la kiafya la ndui na surua na anaendelea kuonyesha kwamba ufichuo kwa vikolezo hivi maalum kufikia kinga ya kudumu (ingawa si kutumia muda). [3] Hata hivyo, ni nadharia ya viini-maradhi ya ugonjwa ya Louis Pasteur iliyoiruhusu sayansi mpya ya elimu ya kingamaradhi kueleza jinsi ugonjwa unavyosababishwa na bakteria, na jinsi, kufuatia maambukizo, mwili wa binadamu unapata uwezo wa kupinga maambukizo zaidi. [1]

 
Louis Pasteur katika maabara yake, 1885.

Matibabu hai ya maradhi kwa njia ya kuanzisha, kuimarisha au kuzuia mwitikio wa kingamwili huenda yalianza na Mithridates VI wa Ponto (leo nchini Uturuki). [5] Ili kusababisha kinga tendi kwa sumu ya nyoka, yeye alipendekeza utumizi wa mbinu sawa na tiba ya kisasa ya majimaji ya damu yaliyotolewa sumu, kwa kunywa damu ya wanyama waliokula nyoka wenye sumu. [5] Kulingana na Jean de Maleissye, Mithridates aliamini kuwa wanyama waliokula nyoka wenye sumu walipata nguvu za kuondoa jinsi ya sumu ya dutu ndani ya miili yao, na damu yao ni lazima iwe na vijenzi vya sumu ya nyoka vilivyopunguzwa au kugeuzwa. Kitendo cha vijenzi hivyo kinaweza kuwa kuimarisha mwili kuipinga sumu badala ya kugandamiza athari za sumu. Mithridates alitoa hoja kwamba, kwa kunywa damu ya wanyama hao, atapata upinzani sawa kwa sumu ya nyoka kama wanyama waliokula nyoka hao. [5] Vile vile, alitaka kujishupaza dhidi ya sumu, na alikunywa vipimo vya dawa vya kukaribia kusababisha mauti kila siku kujenga stahamala. Inasemekana kuwa Mithridates pia alitengeneza 'kimaliza-sumu cha hali zote' kumlinda kutokana na sumu zote duniani. [3] Kwa karibu miaka 2000, sumu zilidhaniwa kuwa sababu ya karibu ya ugonjwa, na mchanganyiko changamani wa viungo, uitwao Mithridati, ulitumika kutibu kuathiriwa na sumu wakati wa Mvuvumko. [3] Toleo la kisasa la tiba hii, Theriacum Andromachi, lilitumiwa hadi karne ya 19. [6]

Mwaka wa 1888 Emile Roux na Alexandre Yersin walitenga sumu ya dondakoo, na baada ya ugunduzi wa 1890 wa Emil von Behring na Kitasato wa kinga inayotokana na antitoksini dhidi ya dondakoo na pepopunda, antitoksini ikawa fanikio kuu la kwanza la elimu ya kingamaradhi ya kisasa. [3]

Ulaya, kusimika kwa kinga tendi kulijitokeza katika jaribio la kudhibiti ndui. Chanjo, hata hivyo, ilikuwepo katika aina mbalimbali kwa angalau miaka elfu moja. [1] Matumizi ya kwanza ya chanjo hayajulikani, hata hivyo mnamo 1000 BK Wachina walianza kufanya majaribio ya aina hiyo kwa kukausha na kuvuta poda inayotokana na maganda ya vidonda vya ndui. [1]

Mnamo karne ya 15 huko Uhindi, Milki ya Osmani na Afrika ya Mashariki, utaratibu wa kuchanja na virusi vya ndui ili kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo (kudukiza ngozi na nyenzo za poda zinazotokana na maganda ya ndui) kukawa kawaida. [1] Kuchanja na virusi vya ndui ili kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo kuliletwa magharibi mapema karne ya 18 na Maria Wortley Montagu. [1]

Mwaka wa 1796, Edward Jenner alianzisha utaratibu salama zaidi wa kuchanja na virusi vya ndui ya ng'ombe, virusi visivyo vya kufisha ambavyo vilisababisha kinga kwa ndui. Mafanikio na ridhaa ya jumla ya utaratibu wa Jenner baadaye yalisababisha hali jumla ya chanjo iliyoendelezwa na Pasteur na wengine karibu na mwisho wa karne ya 19. [3]

Kinga tulivu

hariri

Kinga tulivu ni uhamisho wa kinga tendi, katika hali ya kingamwili za kutungua, kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kinga tulivu inaweza kutokea kwa kawaida, wakati kingamwili za wanawake wajawazito zinapohamishiwa kutoka kwa kijusi kupitia kwa kondo, na pia inaweza kusababishwa kwa kughushi, wakati viwango vya juu vya kingamwili za binadamu au farasi maalum kwa ajili ya kisababishi magonjwa au toksini ni vinahamishwa kwa watu wasio na kinga. Kinga tulivu hutumika wakati kuna hatari kubwa ya maambukizi na wakati usiotosha kwa mwili kukuza kinga yake, au kupunguza dalili za magonjwa yanayoendelea au ya kukandamiza kinga. Kinga tulivu hutoa ulinzi mara moja, lakini mwili haukuzi kumbukumbu, kwa hivyo ya mgonjwa yuko katika hatari ya kuambukizwa na kisababishi magonjwa sawa baadaye.[7]

Kinga tulivu ya kimaumbile

hariri

Kinga tulivu ya uzazi ni aina ya kinga tulivu ya asili, na inahusu kinga iliyoibuliwa na kingamwili iliyowasilishwa kwa kijusi mamake wakati wa ujauzito. Kingamwili za uzazi (MatAb) huwasilishwa kupitia kwa kondo hadi kwa kijusi kupitia kipokezi cha FcRn kwenye seli za kondo. Hii hutokea katika mwezi wa tatu wa kipindi cha ujauzito. [8] IgG (imunoglobulini) ndio isotaipu pekee ya kingamwili inayoweza kupitia kwa kupitisha kwa kondo. [8] Kinga tulivu pia hutolewa kupitia uhamisho wa kingamwili za IgA (immunoglobulini A) zinazopatikana katika maziwa ya mama zinazohamishwa hadi kwa matumbo ya mtoto, kulinda dhidi ya maambukizi ya bakteria, hadi mtoto atakapoweza kusanisi kingamwili zake mwenyewe.

 
Moja ya chupa za kwanza za antitoksini ya dondakoo ilitengenezwa (1895).

Kinga tulivu inayopatikana kwa kughushi

hariri

Kinga tulivu inayopatikana kwa kughushi ni kingamardhi ya muda mfupi inayosababishwa na uhamisho wa kingamwili, ambayo inaweza kutolewa katika aina mbalimbali; kama plazma ya damu ya binadamu au ya mnyama, kama immunoglobulini iliyochangwa kwa matumizi ya ndani ya mshipa (IVIG) au ya ndani ya misuli (IG), na kama kingamwili za monoklonali (MAb). Uhamisho tulivu hutumika kukinga katika kesi za magonjwa ya ukosefu wa kinga mwilini, kama vile haipogamaglobulinemia. [9] Inatumika pia katika matibabu ya aina mbalimbali za maambukizi hatari, na kutibu kuathiriwa na sumu. Kinga inayotokana na kingamaradhi tulivu hudumu kwa muda mfupi tu, na pia kuna uwezukano wa hatari ya athari za wepesi kupita kiasi kuhisi, na ugonjwa unaotokana na mwili kukataa majimaji ya damu kutoka nje, hasa kutoka kwa gama globulini ya asili isiyo ya binadamu.

Kuingiza kinga tulivu kwa kughushi kumetumika kwa zaidi ya karne moja kutibu magonjwa ya kuambukiza, na kabla ya majilio ya viua vijasumu, mara nyingi yalikuwa matibabu pekee maalumu kwa maambukizi fulani. Tiba ya immunoglobulini iliendelea kuwa tiba ya mstari wa kwanza katika matibabu ya magonjwa hatari ya kupumua hadi miaka ya 1930, hata baada ya kuanzishwa kwa viua vijasumu vya salfonamidi. [9]

Uhamisho tulivu wa kinga iliyoibuliwa na seli

hariri

Uhamisho tulivu au "wa kupanga" wa kinga iliyoibuliwa na chembe, unatendeka kwa uhamisho wa chembe T "zilizohisishwa" au zilizoamilishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi ndani ya mwingine. Hautumiki sana kwa binadamu kwa sababu unahitaji changizi wenye tishu patanifu (sawa), na mara nyingi ni vigumu kuwapata. Katika changizi wasiopatana aina hii ya uhamisho ina hatari kubwa ya ugonjwa unaosababishwa na kutolingana kwa seli iliyobandikwa na iliyokuwemo. Hata hivyo, umetumiwa kutibu magonjwa kadhaa ikiwa ni pamoja na aina fulani za saratani na ukosefu wa kinga mwilini. Aina hii ya uhamisho hutofautiana na upandikizi uboho, ambapo seli za shina zenye uwezo wa kujitengeneza upya (zisizotofautishwa) huhamishwa.

Kinga tendi

hariri
 
Kipimo cha muda wa mwitikio ya kinga. Kutokana na utengenezaji wa kumbukumbu ya kinga, maambukizi mapya baadaye husababisha ongezeko la haraka katika uzalishaji wa zindiko na shughuli za seli za kichochezi T. Maambukizi haya ya baadaye yanaweza kuwa madogo au hata yasiyoonekana.

Wakati seli B na seli T zinapoamilishwa na kisababishi magonjwa, seli B na seli T za husitawi. Katika maisha yote ya mnyama seli hizi za kumbukumbu "zitakumbuka" kila kisababishi magonjwa maalum zilizo kabiliana nacho, na zina uwezo wa kuweka ulinzi mkali ikiwa kisababishi magonjwa hicho kitaonekana tena. Aina hii ya kinga ni hai na ya kupanga kwa sababu mfumo wa kinga wa mwili hujiandaa kwa changamoto za baadaye. Wakati mwingi kinga tendi huhusisha vipengele vya kuibuliwa na seli na vya ugiligili vya kinga pamoja na pembejeo kutoka mfumo asili wa kinga. Mfumo asili upo tangu kuzaliwa na humlinda mtu kutoka kwa visababishi magonjwa bila kujali uzoefu, ilhali kinga ya kupanga hutokea tu baada ya kuambukizwa au chanjo na hivyo "hupatikana" wakati wa maisha.

Kinga tendi ya kimaumbile

hariri

Kinga tendi ya kimaumbile hutokea wakati mtu anafichuliwa kwa kisababishi magonjwa hai, na anakuza mwitikio wa msingi wa kinga, unaosababisha kumbukumbu ya kinga. Aina hii ya kinga ni ya "kimaumbile" kwa sababu haisababishwi na dhihiriko la kimaksudi. Matatizo mengi ya kazi ya mfumo wa kinga yanaweza kuathiri uumbaji wa kinga tendi kama vile ukosefu wa kinga mwilini (inayopatikana na ya kuzaliwa) na uzuiaji wa mwitikio wa kingamwili.

Kinga tendi inayopatikana kwa kughushi

hariri
Makala kuu: Chanjo

Kinga tendi inayopatikana kwa kughushi inaweza kusababishwa na chanjo, dutu iliyo na antijeni. Chanjo huchangamsha mwitiko wa msingi dhidi ya antijeni bila kusababisha dalili za ugonjwa huo. Neno kuchanja liliundwa na Edward Jenner na lilitoholewa na Louis Pasteur kwa kazi yake tangulizi katika kuchanja. Mbinu iliyotumiwa na Pasteur ilihusu kutibu vikolezo vya kuambukiza kwa magonjwa hayo na hivyo vilipoteza uwezo wa kusababisha ugonjwa hatari. Pasteur alichukua jina chanjo kama jina tambulishi kwa heshima ya ugunduzi wa Jenner, ambalo kazi ya Pasteur ilitumia kama msingi.

 
Bango la kutoka kabla ya kukomesha kwa 1979 kwa ndui, kuendeleza chanjo.

Mwaka wa 1807, Wabavaria walikuwa kundi la kwanza kuwataka makuruta wake wa kijeshi kuchanjwa dhidi ya ndui, kwa sababu kueneza kwa ndui kulihusishwa na mapambano. [10] Baadaye utaratibu wa chanjo uliongezeka kwa sababu ya kuenea kwa vita.

Kuna aina nne za chanjo za jadi: [11]

  • Chanjo amabazo hazijaamilishwa zinajumuisha viumbehai wadogo waliouliwa na kemikali na/au joto na hawawezi tena kuambukiza. Mifano ni chanjo dhidi ya homa, kipindupindu, tauni ya mtoki, na hepatitisi A. Chanjo nyingi za aina hii zinaweza kuhitaji sindano za kuongeza nguvu.
  • Chanjo hai, zilizopunguzwa zinajumuisha viumbehai wadogo ambao wamekuwa katika hali ambazo hulemaza uwezo wao wa kusababisha ugonjwa. Miitikio hii hudumu zaidi na kwa jumla haihitaji sindano za kuongeza nguvu. Mifano ni pamoja na homa ya manjano, surua, rubela, na matumbwitumbwi.
  • Toksoidi ni misombo ya sumu ambayo haijaamilishwa inayotoka kwenye viumbehai wadogo katika hali ambapo toksoidi hizi (badala ya viumbehai wenyewe) husababisha ugonjwa, inayotumika kabla ya kukutana na sumu ya kiumbehai. Mifano ya chanjo yenye msingi wa toksoidi ni pepopunda na dondakoo.
  • Chanjo za vitengo vidogo vinajumuisha vipande vidogo vya viumbehai vinavyosababisha vidogo vya ugonjwa kusababisha athari ya viumbe. Mfano wa kawaida ni chanjo ya kitengo kidogo dhidi ya virusi hepatitisi B.

Chanjo nyingi hutolewa kwa udungaji sindano chini ya ngozi kwa sababu haifyonzwi kwa urahisi kupitia kwa matumbo. Chanjo hai iliyopunguzwa ya polio na baadhi ya chanjo za homa ya matumbo na kipindupindu hutolewa kwa kinywa ili kutoa kinga iliyo kwenye matumbo.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 Gherardi E. Dhana ya Kinga. Ilihifadhiwa 2 Januari 2007 kwenye Wayback Machine.Historia na Matumizi. Ilihifadhiwa 2 Januari 2007 kwenye Wayback Machine. Kozi ya Elimu ya kingamaradhi katika Shule ya Uuguzi, Chuo Kikuu cha Pavia.
  2. 2.0 2.1 Lindquester, Gary J. (2006) Utangulizi kwa Historia ya ugonjwa. Ilihifadhiwa 21 Julai 2006 kwenye Wayback Machine. Ugonjwa na Kinga, Chuo cha Rhodes.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 Silverstein, Arthur M. (1989) Historia ya Elimu ya kingamaradhi (Hardcover) Jarida la Kielimu. Kumbuka: Kurasa sita za kwanza za fungu hili zinapatikana mtandaoni kwa: ( Amazon.com msomaji rahisi )
  4. A "al-Razi." 2003 Ensaiklopidia ya Elektroni ya Columbia, Toleo la Sita. Jarida la Chuo Kikuu cha Columbia (kutoka Answers.com, 2006.)
  5. 5.0 5.1 5.2 Maleissye J (1991). Historia ya Sumu. Paris: Francois Bourin, ISBN 2876860821 (kwa Kifaransa. Imetafsiriwa kwa Kijapani: Hashimoto I, Katagiri T, Watafsiri (1996). [Historia ya sumu]. Tokyo: Shin-Hyoron, Ltd, ISBN 4-7948-0315-X C0020).
  6. Kimaliza-sumu ".
  7. Janeway, Charles (2001). Immunobiology; Fifth Edition. New York and London: Garland Science. ISBN 0-8153-4101-6. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help).
  8. 8.0 8.1 Coico, R., Sunshine, G., na Benjamin, E. (2003). "Elimu ya kingamaradhi: Kozi Fupi." Uk. 48.
  9. 9.0 9.1 Keller, Margaret A. and E. Richard Stiehm (2000). "Passive Immunity in Prevention and Treatment of Infectious Diseases". Clinical Microbiology Reviews. 13 (4): 602–614. doi:10.1128/CMR.13.4.602-614.2000. ISSN 0893-8512. PMC 88952. PMID 11023960. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-08. Iliwekwa mnamo 2010-11-06. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |month= ignored (help)
  10. Mashirika ya Kitaifa ya Afya "Ndui - Mjeledi mkubwa na wakutisha" Kuchanja na virusi vya ndui ili kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo
  11. Kinga: Una uwezo. Ilihifadhiwa 29 Septemba 2006 kwenye Wayback Machine. Mpango wa Kiaifa wa Kupeana Kingamaradhi katika Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Ugonjwa