Nyanda za Chini za Ulaya ya Kaskazini

(Elekezwa kutoka North European Plain)

Nyanda za Chini za Ulaya Kaskazini (pia: za Ulaya ya Kati) ni eneo la Ulaya ya Kati, hasa katika Poland, Denmark, Ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi, pamoja na sehemu ndogo ya kaskazini mwa Ufaransa na Ucheki.

Nyanda za Chini za Ulaya ya Kati/Kaskazini (kijani).
Nyanda za Chini za Ulaya huonekana kwenye ramani hii kwa rangi ya kijani.

Yote hayo ni maeneo ya kimo cha chini kati ya Bahari ya Kaskazini na Bahari Baltiki upande wa kaskazini na nyanda za juu za Ulaya ya Kati upande wa kusini. Upande wa mashariki yanaendelea katika Nyanda za Chini za Ulaya Mashariki (East European Plain), ilhali zote ni sehemu za Nyanda za Chini za Ulaya (European Plain).

Kwa Kijerumani na Kipoland eneo hilo huitwa "Nyanda za Chini za Ulaya ya Kati" maana kwao "Ulaya ya Kaskazini" iko upande wa kaskazini wa bahari.

Matumizi hariri

Kwa jumla maeneo hayo hutumiwa kwa kilimo; uoto asilia umebaki kwa viwango vidogo tu. Miji ilikua kando ya mito iliyokuwa njia za usafiri tangu zamani.

Jiografia hariri

Miinuko hufikia kati ya mita 0 na 200 juu ya usawa wa bahari; hakuna vilima juu ya mita 200-300[1]. Sura ya nchi ilipata umbo lake kutokana na vipindi vya enzi za barafu zilizopita ambako matabaka manene ya barafu yalisukumwa juu ya nchi kutoka kaskazini yakisukuma viwango vikubwa vya miamba, mchanga na udongo mbele yake. Yaliyobaki ni sehemu za vilima ambavyo mara nyingi ni mchanga bila rutuba na tambarare zilizofanywa na maji ya mito wakati wa kuyeyuka kwa barafu ambako matope yenye rutuba yamebaki.

Uenezaji hariri

Nyanda za Chini hizo zinaanza upande wa magharibi pale Flandria (kaskazini mwa Ubelgiji), zikiendelea Uholanzi, Ujerumani Kaskazini, Denmark na Poland; zinagusa Jamhuri ya Ucheki na sehemu ya kusini magharibi ya Uswidi pia.  

Mito hariri

Mabeseni makuu ya mito ni pamoja na, kutoka magharibi hadi mashariki: Rhine, Ems, Weser, Elbe, Oder na Vistula .

Marejeo hariri

  1. European Plain, tovuti ya Britannica.com, iliangaliwa Agosti 2020

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za Chini za Ulaya ya Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

54°00′N 14°00′E / 54.000°N 14.000°E / 54.000; 14.000