Papa Anastasio I
Papa Anastasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 27 Novemba 399 hadi kifo chake tarehe 19 Desemba 401[1]. Alitokea Roma, Italia. Baba yake aliitwa Maximus.
Alimfuata Papa Siricius akafuatwa na mwanae Papa Inosenti I, aliyemzaa kabla hajapadrishwa, jambo la pekee katika historia ya Kanisa[2].
Alilaani mafundisho kadhaa ya Origen na kuhimiza Wakristo wa Afrika Kaskazini wapinge Udonato.
Alikuwa rafiki wa Augustino wa Hippo, Jeromu na Paulino wa Nola. Jeromu alimsifu kama mtu mwenye utakatifu mkubwa na tajiri sana katika ufukara wake[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Desemba[4].
Tazama pia
haririMaandishi yake
hariri- Maandishi yake yote katika Patrologia Latina iliyotolewa na Migne.
Tanbihi
hariri- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ "Sant' Innocenzo I su santiebeati.it".
- ↑ Campbell, Thomas (1907). "Pope St. Anastasius I". Catholic Encyclopedia. 1. New York: Robert Appleton Company.
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Anastasio I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |