Papa Gelasio I
Papa Gelasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Machi 492 hadi kifo chake tarehe 21 Novemba 496[1]. Alikuwa Papa wa tatu mwenye asili ya Afrika kaskazini.[2][3][4]
Alimfuata Papa Felix III akafuatwa na Papa Anastasio II.
Maarufu kwa ujuzi na uadilifu, alidai utiifu kwake kutoka kwa Wakristo wa Magharibi na Mashariki vilevile na kutetea kwa nguvu imani sahihi hata kuchangia mabishano, ingawa alikuwa na mahusiano mazuri na watawala Waostrogoti waliokuwa Waario[5].
Akisukumwa na upendo wake mkubwa na mahitaji ya maskini, ili kuwasaidia yeye mwenyewe alifariki fukara sana [6].
Maandishi
haririMwandishi mahiri[7], kati ya Mapapa wa karne za kwanza, ndiye aliyeandika zaidi.
Mwaka 494, aliandika barua Duo sunt kwa kaisari Anastasius I kuhusu mahusiano ya Kanisa na Dola; barua hiyo aliathiri siasa kwa karibu miaka elfu.[8] Ili kuzuia mamlaka ya kaisari isidhuru umoja wa Kanisa, alichambua kwa dhati sifa za mamlaka hiyo ya kidunia na za ile ya kiroho, akisisitiza haja ya kila upande kuwa huru.
Pia zimetufikia barua zake nyingine zaidi ya 100[9]. Maandishi mengine yalitajwa kuwa ya kwake ingawa si kweli; lengo lilikuwa kuyatia maanani zaidi.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 21 Novemba[10].
Tazama pia
haririMaandishi yake
hariri- Opera Omnia katika Patrologia Latina ya Migne pamoja na faharasa
- Duo sunt: introduction and text in English
- Decretum Gelasianum: De Libris Recipiendis et Non Recipiendis Ilihifadhiwa 20 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine.
Tanbihi
hariri- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ Browne, M. (1998). "The Three African Popes". The Western Journal of Black Studies. 22 (1): 57–58. Iliwekwa mnamo 2008-04-10.
- ↑ J.Conant, Staying Roman: Conquest and Identity in Africa and the Mediterranean, 439–700, CUP, 2012, p. 83.
- ↑ "Book of Saints – Pope Gelasius". CatholicSaints.Info (kwa American English). 2013-06-23. Iliwekwa mnamo 2020-08-20.
- ↑ Cohen, Samuel (2022). "Gelasius and the Ostrogoths: jurisdiction and religious community in late fifth‐century Italy". Early Medieval Europe (kwa Kiingereza). 30 (1): 22–23. doi:10.1111/emed.12519. ISSN 0963-9462.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90444
- ↑ The title of his biography by Walter Ullmann expresses this:Gelasius I. (492–496): Das Papsttum an der Wende der Spätantike zum Mittelalter (Stuttgart) 1981.
- ↑ "Internet History Sourcebooks Project". sourcebooks.fordham.edu. Iliwekwa mnamo 2020-08-20.
- ↑ Gelasius I (2014). Neil, Bronwen; Allen, Pauline (whr.). The letters of Gelasius I (492-496) : pastor and micro-manager of the Church of Rome. Turnhout, Belgium. ku. 8–9. ISBN 978-2-503-55299-6. OCLC 893407493.
{{cite book}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) - ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Marejeo
hariri- Maisha yaliyoandikwa na Dionysius Exiguus, mwanafunzi wa Cassiodorus.
- Norman F. Cantor, Civilization of the Middle Ages.
- Cohen, Samuel (2022). "Gelasius and the Ostrogoths: jurisdiction and religious community in late fifth‐century Italy". Early Medieval Europe. 30 (1): 20–44. doi:10.1111/emed.12519. ISSN 0963-9462.
- Neil, Bronwen, and Allen, Pauline (eds. and trans.). The letters of Gelasius I (492-496) : pastor and micro-manager of the Church of Rome. Turnhout, Belgium. pp. 8–9. ISBN 978-2-503-55299-6. OCLC 893407493.
- Catholic Encyclopedia, 1908: [1]
- Rudolf Schieffer, Gelasius I, in Lexikon des Mittelalters, Bd. 4 (1989), Sp. 1197.
- Ullmann, W., Gelasius I. (492–496): Das Päpsttum an der Wende der Spätantike zum Mittelalter, Stuttgart, 1981.
Viungo vya nje
hariri- Liber pontificalis
- Fontes Latinae de papis usque ad annum 530 (Papa Felix IV)
- Kuhusu Papa Gelasio I katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Gelasio I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |