Kambaremamba

(Elekezwa kutoka Protopterus)
Kambaremamba
Kambaremamba wa Afrika (Protopterus aethiopicus)
Kambaremamba wa Afrika (Protopterus aethiopicus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
(bila tabaka): Dipnomorpha
Ngeli: Sarcopterygii (Samaki walio na mapezi yenye nyama)
Oda: Dipnoi (Samaki kama kambaremamba)
Müller, 1844
Ngazi za chini

Familia 2, jenasi 3, spishi 6:

Kambaremamba ni samaki wa maji matamu walio na mapafu na kwa hivyo wanaweza kupumua hewa. Pia wana mapezi yenye nyama na mifupa iliyokuzwa vizuri. Hutokea katika mito, maziwa, vinamasi na mabwawa. Mara nyingi wanaishi katika mashimo ndani ya sakafu. Wanaweza kuendelea kuishi katika mashimo hayo hata ikiwa maji yakikauka, isipokuwa kambaremamba wa Australia.

Maelezo

hariri

Kambaremamba wote wana uti wa mgongo ulioumbwa kwa gegedu na meno ya kaakaa yaliyokuzwa sana. Spishi zote za kisasa zinaonyesha kupunguka kwa kiasi kikubwa kwa mifupa ya mbavu na fuvu la ubongo la gegedu. Pia zinaonyesha kupunguka na kuunganisha kwa kiasi kikubwa cha mifupa ya paa la fuvu ambayo haionyeshi homolojia na mifupa ya paa la fuvu ya samaki walio na mapezi yenye tindi au tetrapodi. Wakati wa msimu wa kuzaliana kambaremamba wa Amerika ya Kusini hukuza viungo vifananavyo na manyoya ambavyo kwa kweli ni mapezitumbo yaliyotoholewa sana. Mapezi haya yanafikiriwa kuboresha ubadilishaji wa gesi kuzunguka mayai ya samaki katika kiota chake[1].

Meno ya kambaremamba ni tofauti na yale ya kundi lolote la vertebrata. Meno ya ngozi kwenye kaakaa na mataya ya chini hukua katika mfufulizo wa safu ili kuunda uso wa mguso wenye umbo la kipepeo (kifaa). Meno haya ya ngozi huchakaa na kuunda uso sawa wa kusaga. Katika Lepidosirenidae za kisasa viinuko hivyo vimetoholewa ili kuunda mabamba.

Kambaremamba wa kisasa wote wana mwili mrefu wenye jozi za mapeziubavu na mapezitumbo yenye nyama na pezimkia linalobadili pezimgongo, pezimkundu na pezimkia ya takriban samaki wote. Wana jenomu kubwa kabisa kati ya vertebrata.

Mapafu

hariri
 
Mwonekano wa pembeni wa mapafu ya kambaremamba madoa (Protopterus dolloi)

Kambaremamba wana mfumo maalum wa kupumua. Wana sifu bainifu kwa kuwa mapafu yao yanaunganishwa na koromeo na koo bila bomba la pumzi. Ingawa spishi nyingine za samaki zinaweza kupumua hewa kwa kutumia vibofuhewa vilivyobadilishwa na vilivyo na mishipa[2], vibofu hivi kwa kawaida ni vifuko rahisi visivyo na muundo tata wa ndani. Kinyume chake, mapafu ya kambaremamba yamegawanywa katika vifuko vingi vidogo vya hewa, na hivyo kuongeza eneo la uso linalopatikana kwa kubadilisha gesi.

Spishi zote za kambaremamba zilizopo zina mapafu mawili, isipokuwa kambaremamba wa Australia, ambaye ana moja tu. Mapafu ya kambaremamba yana homolojia na mapafu ya tetrapodi. Kama ilivyo katika tetrapodi na samakimagamba, mapafu huenea kutoka kwenye uso wa chini wa umio na utumbo[3][4].

Ekolojia na historia ya maisha

hariri

Kambaremamba ni walavyote na hula samaki, wadudu, gegereka, nyungunyungu, moluska, amfibia na mada ya mimea. Wana vali ya parafujo katika utumbo badala ya tumbo halisi[5].

Spishi za Afrika na Amerika ya Kusini zina uwezo wa kuokoa kukauka kwa majira kwa makazi yao wakichimba kwenye matope na kuokoa majira yote ya ukame. Mabadiliko katika fiziolojia huwaruhusu kupunguza metaboliki yao hadi 1⁄60 ya kiwango cha kawaida cha kimetaboliki, na takataka za protini hubadilishwa kutoka amonia hadi urea iliyo sumu dhaifu (kwa kawaida, kambaremamba hutoa takataka ya kinitrojeni kama amonia moja kwa moja ndani ya maji).

Kambaremamba wanaweza kuwa na maisha marefu sana. Kiolezo kutoka Queensland katika Shedd Aquarium huko Chicago alikuwa kipande cha mkusanyo wa kudumu wa moja kwa moja kutoka 1933 hadi 2017, ambapo alipata utanazia kufuatia kuzorota kwa afya kulingana na uzee[6]. Kambaremamba wa Australia anayeishi katika jumba la makumbusho la San Francisco anaaminika kuwa samaki mzee kabisa duniani katika tangisamaki. Methuselah ana urefu wa m 1.2 na uzito wa karibu kg 18.1[7].

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Marejeo

hariri
  1. Piper, Ross (2007). Extraordinary Animals: An encyclopedia of curious and unusual animals. Greenwood Press.
  2. Colleen Farmer (1997), "Did lungs and the intracardiac shunt evolve to oxygenate the heart in vertebrates" (PDF), Paleobiology, 23 (3): 358–372, doi:10.1017/s0094837300019734, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 11 Juni 2010{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Wisenden, Brian (2003). "Chapter 24: The Respiratory System – Evolution Atlas". Human Anatomy. Pearson Education, Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Novemba 2010.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Hilber, S.A. (2007). "Gnathostome form & function". Vertebrate Zoology Lab. U. Florida. Lab 2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Julai 2011. Iliwekwa mnamo 31 Desemba 2010. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Purkerson, M.L. (1975). "Electron microscopy of the intestine of the African lungfish, Protopterus aethiopicus". The Anatomical Record. 182 (1): 71–89. doi:10.1002/ar.1091820109. PMID 1155792. S2CID 44787314.
  6. "Chicago aquarium euthanizes 90 year-old lungfish". Retrieved on 2022-06-07. Archived from the original on 2017-02-07. 
  7. {https://www.youtube.com/watch?v=cmYYtzLeTgY Kambaremamba Methusalah}