Saizana
Saizana wa Axum alikuwa ndugu wa Ezana, mfalme (320 hivi – 360 hivi) wa Ufalme wa Aksum uliokuwepo katika sehemu ambayo inajulikana siku hizi kama Tigray, kaskazini mwa Ethiopia na Eritrea, lakini pia Yemen. Mwenyewe alijiita mfalme wa Saba, Salhen, Himyar na Dhu-Raydan."[1], miji ya zamani ambayo Ezana alimrithi baba yake Ella Amida (Ousanas) tangu alipokuwa mdogo, mama yake Sofya akiwa kama msaidizi wake.
Ezana ndiye alikuwa mfalme wa kwanza wa Axum kupenda dini ya Ukristo, na mmoja baada ya Zoskales kutajwa na wanahistoria maarufu, hali iliyopelekea S.C. Munro kusema kuwa, Ezana "ndiye mfalme maarufu zaidi kuwahi kuongoza ufalme wa Axum."[2]
Yeye alimchagua Frumensyo, mlezi wake wa utotoni kutoka Lebanoni, kuwa mkuu wa Kanisa la Ethiopia. Ni kwamba mwaka 316 hivi, wakati alipotawala Kaisari Konstantino Mkuu kule Roma, meli moja ilikuwa safarini kutoka Shamu kwenda Bara Hindi ikaharibika kwenye pwani ya Ethiopia. Vijana wawili waliokolewa wakapelekwa mbele ya mfalme kule Aksum.
Mmojawao, Frumensyo, alipata haraka sifa za kuwa mwenye elimu na hekima. Akapanda ngazi kuwa mshauri wa mfalme na mwalimu wa wana wa mfalme Ezana na Saizana. Frumensyo aliweza kupanda mbegu za imani moyoni mwa vijana hao. Baada ya kuwa mfalme, Ezana akaendelea kumtumia Frumensyo kama mshauri wake.
Siku moja Frumensyo aliomba ruhusa ya mfalme aende nyumbani kuangalia kama wazazi wake bado wanaishi. Mfalme akamruhusu akamwomba atafute kule walimu wanaoweza kufundisha elimu aliyokuwa nayo Frumensyo pamoja na imani ya Kikristo. Frumensyo akamwendea Askofu Mkuu wa Misri aliyemweka wakfu kuwa askofu kwa ajili ya Waethiopia. Hivyo Kanisa lilianza katika nyanda za juu za Ethiopia. Mfalme Ezana akabatizwa akifuatwa na watu wengi wa makao makuu.
Kuna barua ya Kaisari Mwario wa Roma Constantius II kwa Ezana na Saizana, iliyoomba Frumensyo apelekwe Aleksandria achunguzwe kuhusu imani yake; inawezekana kwamba Ezana alikataa au kupuuzia ombi hilo.[3]
Ezana na Saizana, wanachukuliwa kama watakatifu nchini Ethiopia na kukumbukwa tarehe 1 Oktoba[4].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ S. C. Munro-Hay, Aksum: An African Civilization of Late Antiquity (Edinburgh: University Press, 1991), p. 81. ISBN 0-7486-0106-6
- ↑ Munro-Hay, Aksum, p. 77
- ↑ Munro-Hay, Aksum, pp. 78ff
- ↑ Holweck, F. G., A Biographical Dictionary of the Saints. St. Louis, MO: B. Herder Book Co. 1924
Marejeo
hariri- Yuri M. Kobishchanov. Axum (Joseph W. Michels, editor; Lorraine T. Kapitanoff, translator). University Park, Pennsylvania: University of Pennsylvania, 1979. ISBN 0-271-00531-9
- Sergew Hable Sellassie. Ancient and Medieval Ethiopian History to 1270 (Addis Ababa: United Printers, 1972).
- African Zion, the Sacred Art of Ethiopia, (New Haven: Yale University Press, 1993).
- Stuart Munro-Hay, Aksum: An African Civilisation of Late Antiquity http://users.vnet.net/alight/aksum/mhak1.html
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |