Senegal
Senegal (pia Senegali) ni nchi ya Afrika ya Magharibi iliyopo upande wa kusini wa mto Senegal.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Un Peuple, Un But, Une Foi (Kifaransa: Taifa moja, Lengo moja, Imani moja) | |||||
Wimbo wa taifa: Pincez Tous vos Koras, Frappez les Balafons' | |||||
Mji mkuu | Dakar | ||||
Mji mkubwa nchini | Dakar | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali | Jamhuri Macky Sall Sidiki Kaba | ||||
Uhuru kutoka Ufaransa |
20 Juni 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
196,712 km² (ya 87) {{{percent_water}}} | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2015 sensa - Msongamano wa watu |
18,384,660 (ya 66) 13,508,715 93.3/km² (134) | ||||
Fedha | CFA Franc ({{{currency_code}}} )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+0) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .sn | ||||
Kodi ya simu | +221
- |
Imepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea na Guinea-Bisau kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi.
Nchi ya Gambia inazungukwa na eneo la Senegal isipokuwa upande wa bahari.
Visiwa vya Cabo Verde viko km 560 mbele ya pwani ya Senegal.
Jiografia
haririSenegal ni nchi inayogusana na kanda ya Sahel na pia kanda ya Tropiki.
Uso wa nchi ni hasa tambarare zinazopanda juu polepole kuelekea kusini mashariki. Sehemu nyingine zinafikia mita 580 juu ya UB. Kusini kabisa iko kasoko kubwa la Velingara.
Hali ya hewa ni ya kitropiki. Majira ya mvua ni hasa miezi ya Mei hadi Novemba.
Nchi imegawanyika katika mikoa 14 iliyogawanyika tena katika wilaya 45.
Miji
haririMiji mikubwa ni Dakar (wakazi 2 476 400), Pikine (wakazi 874 062), Thiès (wakazi 252 320), Saint-Louis (wakazi 176 000), Kaolack (wakazi 172 305), Ziguinchor (wakazi 159,788), Tiebo (wakazi 100 289). Karibu nusu ya watu huishi mijini.
Historia
haririKwa wakati na kiasi tofauti eneo la Senegal lilikuwa sehemu ya Dola la Ghana, ya Dola la Mali na hatimaye ya Dola la Songhai
Wakazi
haririKuna wakazi milioni 13.5 na idadi kubwa ni wa chini ya umri wa miaka 20. Wameongezeka sana, mnamo mwaka 1985 idadi ilikuwa milioni 5 tu.
Kikundi kikubwa nchini ni Wawolof (43%), wengine ni Wafula wakiwa pamoja na Watukulur (24%), halafu Waserer (14.7%), Wadiola (4%),Wamandinka (3%), Wasoninke.
Kwa ujumla kuna lugha 37 nchini Senegal. Kiwolofu kinazidi kuenea, lakini mpaka sasa lugha rasmi ni Kifaransa. Shuleni kinatumika pia Kireno, hasa kusini.
Theluthi mbili ya wakazi hawajui kusoma.
Senegal ni nchi isiyo na dini rasmi. Wakazi wengi sana (94%) ni Waislamu (hasa Wasunni); Wakristo (hasa Wakatoliki) ni takriban 5%.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- Babou, Cheikh Anta, Fighting the Greater Jihad: Amadu Bamba and the Founding of the Muridiyya of Senegal, 1853–1913, (Ohio University Press, 2007)
- Behrman, Lucy C, Muslim Brotherhood and Politics in Senegal, (iUniverse.com, 1999)
- Buggenhage, Beth A, Muslim Families in Global Senegal: Money Takes Care of Shame, (Indiana University Press, 2012)
- Bugul, Ken, The Abandoned Baobab: The Autobiography of a Senegalese Woman, (University of Virginia Press, 2008)
- Foley, Ellen E, Your Pocket is What Cures You: The Politics of Health in Senegal, (Rutgers University Press, 2010)
- Gellar, Sheldon, Democracy in Senegal: Tocquevillian Analytics in Africa, (Palgrave Macmillan, 2005)
- Glover, John, Sufism and Jihad in Modern Senegal: The Murid Order, (University of Rochester Press, 2007)
- Kane, Katharina, Lonely Planet Guide: The Gambia and Senegal, (Lonely Planet Publications, 2009)
- Kueniza, Michelle, Education and Democracy in Senegal, (Palgrave Macmillan, 2011)
- Mbacké, Khadim, Sufism and Religious Brotherhoods in Senegal, (Markus Wiener Publishing Inc., 2005)
- Streissguth, Thomas, Senegal in Pictures, (Twentyfirst Century Books, 2009)
- Various, Insight Guide: Gambia and Senegal, (APA Publications Pte Ltd., 2009)
- Various, New Perspectives on Islam in Senegal: Conversion, Migration, Wealth, Power, and Femininity, (Palgrave Macmillan, 2009)
- Various, Senegal: Essays in Statecraft, (Codesria, 2003)
- Various, Street Children in Senegal, (GYAN France, 2006)
Viungo vya nje
hariri- (Kifaransa) Serikali ya Senegal Ilihifadhiwa 16 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
- Country Profile from BBC News
- Senegal entry at The World Factbook
- Senegal Corruption Profile from the Business Anti-Corruption Portal
- Trade
- Senegal 2012 Summary Trade Statistics
- Senegal katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Senegal
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Senegal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |