Guinea

nchi huru katika Afrika Magharibi
(Elekezwa kutoka Gine)

Gine, (pia: Gini; Kifaransa: Guinée; Kiingereza: Guinea) kirasmi Jamhuri ya Gine, ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Gine-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Gine-Bisau na Gine ya Ikweta.

Jamhuri ya Gine
République de Guinée (Kifaransa)
Hawtaandi Gine (Kipular)
ߖߌ߬ߣߍ߫ ߞߊ ߝߊߛߏߖߊߡߊߣߊ (Kimaninka)
Kaulimbiu ya taifa:
Travail, Justice, Solidarité (Kifaransa)
"Kazi, Haki, Mshikamano"
Wimbo wa taifa: Liberté (Kifaransa)
"Uhuru"
Mahali pa Guinea
Mahali pa Guinea
Ramani ya Guinea
Ramani ya Guinea
Mji mkuu
na mkubwa nchini
Conakry
9°31′ N 13°42′ W
Lugha rasmiKifaransa

Imepakana na Gine-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Kodivaa, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi.

Eneo lake ni chanzo ya mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia.

Jina hariri

Jina la "Gine" liliwahi kutaja sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Ghuba ya Gine ya Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberberi.

Watu hariri

Makabila yaliyopo nchini ni 24. Kubwa zaidi ni lile la Wafulani (40%).

Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wakazi wanatumia zaidi lugha asilia kadiri ya makabila, hasa Kipular, Kimaninka, Kisusu, Kikisi, Kikpelle na Kiloma,

Upande wa dini, 85% ni Waislamu (hasa Wasuni), 8% ni Wakristo (hasa Wakatoliki) na 7% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali hariri

Habari hariri

Muziki hariri

Orodha hariri


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guinea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.