Thutmose III [1] (inayomaanisha " Thoth amezaliwa") alikuwa farao wa sita wa nasaba ya 18.

Sanamu ya Thutmose III iko katika jumba la kumbukumbu la Luxor
Kipande cha ukuta wa ukuta.
Hieroglifi 'Mwana wa Ra' iko juu ya alama ya jina la Thutmose III. Nasaba ya 18. Jumba la kumbukumbu la Petrie la Akiolojia ya Misri, London

Thutmose III alikuwa farao kwa karibu miaka 54 (24 Aprili 1479 KK hadi 11 Machi 1425 KK). Alipewa ufalme alipokuwa na umri wa miaka miwili, aliaga dunia akiwa na umri wa miaka hamsini na sita.

Kwa miaka 22 ya kwanza ya utawala wake, alikuwa Farao kwa jina tu ilhali utawala halisi ulikuwa mIkononi mwa mama yake wa kambo na shangazi yake, Hatshepsut, aliyekuwa pia farao, na mtawala halisi kwa sehemu ya kwanza ya ufalme wake. [2] [3] Baada ya kifo cha Hatshepsut alishika utawala mwenyewe. Katika miaka miwili ya mwisho ya utawala wake, alimteua mwanawe na mrithi wake, Amenhotep II, kama farao wa pili na msaidizi wake. Mwanawe wa kwanza aliyemlenga kama mrithi aliitwa Amenemhat lakini alikufa kabla ya Thutmose III.

Alipokuwa mtawala pekee wa ufalme, baada ya kifo cha Hatshepsut, aliunda himaya kubwa zaidi iliyotawaliwa kutoka Misri katika historia hadi leo. Aliendesha kampeni za kivita 17. Alivamia nchi kutoka kaskazini mwa Syria hadi Nubia .

Wakati Thutmose III alipokufa, alizikwa katika Bonde la Wafalme. Wafalme wengine kutoka kipindi hicho cha Misri pia walizikwa huko.

Marejeo hariri

  1. sometimes written as Thutmosis or Tuthmosis III, Thothmes in older history works
  2. Shaw, Ian (ed) 2000. The Oxford Encyclopedia of Ancient Egypt. Oxford University Press, discussion p237 et seq. ISBN 0-19-815034-2
  3. Partridge R. 2002. Fighting Pharaohs: weapons and warfare in ancient Egypt. Manchester: Peartree, p202/203.