Aidani wa Lindisfarne

Aidani wa Lindisfarne (Ireland, 590 hivi - Northumberland, Uingereza, 31 Agosti 651) ndiye aliyeanzisha kituo cha utawa na kuwa askofu wake wa kwanza kwenye kisiwa cha Lindisfarne. Kabla hajafika Northumbria alikuwa mtawa katika kwenye kisiwa cha Iona katika nchi ya Uskoti.

Mtakatifu Aidani katika dirisha la kioo cha rangi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu kwa kufufua Ukristo katika eneo la Northumbria hata akaitwa Mtume wa Northumbria.

Sikukuu yake huadimishwa tarehe 31 Agosti[1].

Maisha hariri

Wakati wa enzi ya Warumi, Ukristo ulikuwa umeenea mpaka Uingereza, lakini kwa sababu ya kushindwa kwa Warumi, Upagani ukaanza kurudi upande wa kaskazini wa Uingereza.

Oswald, mfalme wa Northumbria, mwaka 616 alilazimishwa kwenda uhamishoni katika kisiwa cha Iona ambako akabadilika kuwa Mkristo na kubatizwa.

Mwaka 634 Oswald alirudishiwa ufalme wa Northumbria akaamua kuwaingiza katika Ukristo wananchi wake ambao wengi wao walikuwa Wapagani. Ili kutekeleza lengo hilo aliwaomba watawa wa Iona wamtumie wamisionari, naye Aidani akafika mwaka 635.

Aidani alichagua kisiwa cha Lindisfarne kiwe makao makuu ya dayosisi yake kwa vile kilikuwa karibu na ngome ya kifalme kule Bamburgh.

Mwanzoni alikuwa mfalme Oswald mwenyewe aliyewatafsiria Aidan na watawa wake kwa vile walikuwa hawajajifunza lugha ya kale ya Kiingereza. Baada ya kifo cha Oswald mwaka 642, Aidan alisaidiwa na mfalme Oswine wa Deira, nao wakawa marafiki wa karibu sana.

Aidani alikuwa huwatembelea watu kijiji hadi kijiji, na kuongea nao kwa adabu na kujaribu katika maongezi hayo wavutwe na Ukristo.

Kufuatana na hadithi moja, mfalme alimpa Aidani farasi ili asihitaji kutembea kwa miguu lakini Aidan akatoa farasi kama zawadi kwa mtu maskini.

Aidani aliweza kuongea na watu na hivyo alifaulu kuwasaidia wananchi wengi wa Northumbria wawe Wakristo. Pia katika kituo chake cha utawa aliwafundisha wavulana kumi na wawili, wenyeji wa Northumbria, ili kuhakikisha kwamba Kanisa la Uingereza liongozwe na Waingereza wenyewe.

Aidani alifuata tawi la Kiselti la Ukristo, si mapokeo ya Kiroma. Hata hivyo tabia yake na bidii katika umisionari zilisababisha Papa Honorius I amheshimu.

Kituo cha utawa cha Lindisfarne kiliendelea kukua na kuanzisha makanisa na vituo vingine. Pia kilikuwa kama hazina ya ujuzi wa kitaalamu.

Baadaye, Beda Mhashamu aliandika wasifu wa maisha yake Aidanipamoja na miujiza yake yote.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
  • Powicke, F. Maurice and E. B. Fryde Handbook of British Chronology 2nd. ed. London:Royal Historical Society 1961

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.