Cheche
Cheche wa Indo-Pasifiki (Megalops cyprinoides)
Cheche wa Indo-Pasifiki (Megalops cyprinoides)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii
Oda: Elopiformes
Familia: Megalopidae
D.S. Jordan, 1923
Jenasi: Megalops
Valenciennes, 1847
Ngazi za chini

Spishi 2 zilizopo:

Cheche ni samaki wa baharini na maji baridi katika jenasi Megalops ya familia Megalopidae wanaopumua hewa. Familia hii ina spishi mbili tu.

Spishi na makazi

hariri

Spishi mbili za cheche ni Megalops atlanticus (cheche wa Atlantiki) na Megalops cyprinoides (cheche wa Indo-Pasifiki). Cheche wa Atlantiki hupatikana pwani ya Atlantiki ya Magharibi kutoka Virginia mpaka Brazili, kupitia pwani ya Ghuba ya Mexico, na katika Bahari ya Karibi. Cheche pia hupatikana pwani ya Atlantiki ya Mashariki kutoka Senegali hadi kusini mwa Angola. Cheche wa Indo-Pasifiki hupatikana pwani ya Afrika ya Mashariki, kusini-mashariki kote mwa Asia, Japani, Tahiti na Australia.

Spishi hizi mbili hupatikana katika maji ya chumvi na maji baridi na mara nyingi huingia mito dhidi ya mkondo ili kufikia mabwawa ya maji baridi. Wana uwezo wa kuishi katika maji ya chumvi kidogo, maji ya pH mbalimbali na makazi yenye ukolezi wa chini wa oksijeni kwa ajili ya kibofuboya chao, ambazo hutumia kupumua hasa. Wanaweza pia kwenda juu ili kugugumia hewa, ambayo huwapa muda mfupi wa nishati.

Makazi ya cheche hutofautiana sana na hatua zao za maendeleo. Lava wa hatua ya kwanza hupatikana kwa kawaida katika maji mangavu na vuguvugu ya bahari karibu na uso. Lava wa hatua za pili na tatu hupatikana katika mabwawa ya chumvi, madimbwi ya maji mafu, hori na mito. Sifa za makazi ni maji vuguvugu na kame yenye giza na sakafu za matope ya mchanga. Wanapoendelea kutoka hatua za kitoto hadi samaki wazima, hurudi kwenye maji wazi ya bahari, ingawa wengi hubakia katika makazi ya maji baridi.

Tabia za mofolojia

hariri

Cheche hukua hadi urefu wa m 1.23-2.44 na uzito wa kg 27 - 127. Wana mapezi laini ya juu na ya chini na mgongo buluu au kijani. Huwa na magamba yang'aayo ya rangi ya fedha yanayofunika mwili wao isipokuwa kichwa. Wana macho makubwa na kope nono na kinywa kipana chenye taya la chini la kuchomoza ambalo linatokeza zaidi kuliko uso wote.

Kibofuboya

hariri

Moja ya tabia za pekee za cheche ni kibofuboya kinachofanya kazi kama aina ya ogani ya kupumua. Muundo huu wa gesi unaweza kutumika kwa ajili ya uelezi, kama ogani ya nyongeza ya kupumua, au yote mbili. Katika cheche muundo huo wenye hewa ndani yake unatokea juu ya sehemu ya nyuma ya koromeo. Cheche hutumia kibofuboya kama ogani ya kupumua na ukuta wa kupumua huvaliwa na kapilari za damu zenye epitheliamu nyembamba juu. Hii ni msingi wa tishu ya vijiribahewa iliyopatikana katika kibofuboya na inafikiriwa kuwa ni moja ya mbinu za kwanza ambayo cheche anatumia "kupumua". Samaki hawa wanalazimika kupumua hewa na ikiwa hawataruhusiwi kufikia uso, watakufa. Kubadilishana kwa gesi hutokea kwenye uso wa bahari kwa njia ya mwendo unaozunguka ambao huhusishwa na kuonekana kwa cheche. "Kupumua" huku kunafikiriwa kuwa kuingiliana na ishara zionazo, na mrudio wa kupumua ni kinyume na uhusiano na kiwango cha oksejeni iliyoyeyuka katika maji ambamo wanaishi.

Cheche na binadamu

hariri
 
Cheche wa Atlantiki akiruka juu wakati wa kumvua.

Cheche wanachukuliwa kama mmoja wa samaki muhimu wavuliwao katika bahari. Wanathaminiwa siyo kwa sababu ya ukubwa wao tu lakini pia kwa sababu ya mapigano yao na uwezo wao wa kuruka wa kushangaza. Hawa ni samaki wenye miiba mingi na nyama yao haipendekezi, kwa hivyo wengi hutolewa baada ya kukamatwa. Mashindano mengi yanalenga kukamata kwa cheche mwaka mzima.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri