Daraja la Umoja
Daraja la Umoja (kwa Kiingereza: Unity Bridge) ni daraja la kuvukia mto Ruvuma linalojengwa kwa shabaha ya kuunganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji.
Daraja la Umoja 1 (Unity Bridge 1) English: Unity Bridge Kireno: Ponte da Unidade | |
---|---|
Majina mengine | Daraja la Umoja 1 |
Yabeba | Leni 2 |
Yavuka | Mto Ruvuma |
Mahali | Negomano, Msumbiji Mtambaswala, Tanzania |
Mbunifu wa mradi | Norconsult |
Aina ya daraja | Box girder bridge |
Vifaa vya ujenzi | Saruji (Prestressed concrete Reinforced concrete) |
Urefu | mita 720 |
Upana | mita 13.8 |
Idadi ya nguzo | 18 |
Mjenzi | China Geo Engineering Corporation |
Ujenzi ulianza | 16 Oktoba 2005 |
Gharama za ujenzi | US$ 35 milioni |
Kilizinduliwa | 12 Mei 2010 |
Anwani ya kijiografia | 11°24′52″S 38°29′39″E / 11.41444°S 38.49417°E |
Mahali pa daraja ni takriban km 240 kutoka mdomo wa mto Ruvuma kati ya mkoa wa Mtwara, wilaya ya Nanyumbu na mkoa wa Cabo Delgado, wilaya ya Mueda upande wa Msumbiji.
Daraja hilo linavuka Rovuma mita chache baada ya sehemu ambako Lugenda unaingia. Kijiji cha Mtambaswala katika kata ya Masuguru kinachofikiwa kutoka Masasi kupitia Nangomba kiko karibu na daraja upande wa Tanzania.
Daraja hili linatajwa pia kama "Daraja la Umoja 1" kwa kulitofautisha na daraja lingine takriban kilomita 330 upande wa mashariki katika Mkoa wa Ruvuma linaloitwa Daraja la Umoja 2.
Wazo la ujenzi wa daraja hili lilitolewa tangu mwaka 1975 na Marais wa nchi hizo mbili, ambao walikuwa hayati Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na hayati Samora Machel wa Msumbiji.
Wazo hilo lilijumuishwa rasmi katika Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa mwezi Septemba 1975.[1] Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Pastory Ngaiza na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Zacaria Kupele.
Kikao hicho kilipokea taarifa nzima ya mradi kutoka kwa wataalamu wa pande zote mbili, taarifa hizo zilielezea kukamilika kwa mradi huo ambao hadi unakamilika uligharimu kiasi cha dola milioni 27.5 sawa na Sh bilioni 35.
Makatibu wakuu hao pamoja na wataalamu walikagua eneo la daraja kujionea hali halisi ya kazi iliyofanywa na mkandarasi huyo. Baada ya ukaguzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu injinia Omar Chambo alisema kazi zote muhimu zimekamilika kwa wakati na kwa mujibu wa mkataba.
Daraja la Umoja lina urefu wa mita 720 na upana wa mita 13.5. Pia, ilielezwa kuwa daraja lina upana huo unajumuisha mita 6.5 kwa ajili ya magari na mita 1.5 ya mabega ya barabara kwa watembea kwa miguu kila upande. Kilomita tano kila upande wa daraja zimejengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika.
Hali halisi ujenzi haukuanza hadi mwaka 2005, daraja likafunguliwa tarehe 12 Mei 2010.
Hadi mwaka 2020 daraja halikuunganishwa vizuri na mitandao ya barabara yaani upande wa Tanzania kuna kilomita 7 za lami halafu ni kilomita 60 barabara ya vumbi hadi kufikia tena barabara ya lami ya A19 huko Nangomba. Upande wa Msumbiji ziko kilomita 5 pekee za lami halafu njia ya vumbi. Kuna mipango ya kujenga kilomita 150 za barabara ya lami kutoka daraja hadi Mueda[2].
Marejeo
hariri- ↑ "Sainisho la mkataba wa ujenzi wa daraja la umoja". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-16. Iliwekwa mnamo 2010-05-10.
- ↑ MUEDA - NEGOMANO ROAD PROJECT PHASE I, tovuti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika afdb.org