Eujeni Mazenod (kwa Kifaransa Eugène de Mazenod au kirefu Charles-Joseph-Eugène de Mazenod) (Aix-en-Provence, 1 Agosti 1782 - Marseille, 21 Mei 1861) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa aliyeanzisha shirika la kimisionari maarufu kwa ufupisho O.M.I. kwa ajili ya kuinjilisha maskini.

Picha ya Mt. Eujeni Mazenod.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Paulo VI tarehe 19 Oktoba 1975, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 3 Desemba 1995.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoiaga dunia[1].

Maisha

hariri

Eujeni alizaliwa tarehe 1 Agosti 1782 akabatizwa kesho yake.

Baba yake, Charles Antoine de Mazenod, alikuwa mmoja kati ya wenyeviti wa Mahakama ya Biashara, na mama yake alikuwa Marie Rose Joannis.

Eujeni alianza masomo yake kwenye Chuo Bourbon, lakini hayo yalikatishwa na Mapinduzi ya Kifaransa ambayo yalifilisi familia yake na kuilazimisha kukimbilia Venice, Italia.

Baadaye akawa mwanafunzi wa bweni katika Chuo cha Masharifu huko Torino. Huko alipokea sakramenti ya ekaristi na kipaimara.

Majeshi ya kimapinduzi kutoka Ufaransa yalipovamia Italia, familia ilikimbilia tena Venice, ambapo baba yake alitafuta kazi mbalimbali bila kufanikiwa.

Mama yake alirudi Ufaransa pamoja na binti yake alipoomba talaka kwa lengo la kurudishiwa mali yake iliyokuwa imetaifishwa.

Eujeni alibahatika kukaribishwa na familia Zinelli huko Venice. Padri wa familia hiyo, Bartolo Zinelli, alishughulikia malezi ya mtoto huyo akitumia maktaba kubwa ya nyumbani, ambapo Eujeni alishinda saa kadhaa kwa siku. Padri Bartolo alimuathiri pia sana kiutu na kiroho.

Kwa msukumo wa jeshi tena, Eujeni na baba yake walilazimika kukimbilia kusini, kwanza Naples kwa karibu mwaka mzima, halafu Palermo, Sicilia.

Huko Eujeni aliweza kufuata mtindo wa maisha uliolingana na usharifu wake.

Hatimaye alirudi Ufaransa na kupewa upadrisho huko Amiens mwaka 1811.

Mwaka 1816 alianzisha shirika la Missionary Oblates of Mary Immaculate.[2]

Kati ya miaka 1837 na 1861 alikuwa askofu wa Marseille, akiliangaza jimbo lake kwa maadili, mipango, mahubiri na maandishi[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  • Biography in the Catholic Encyclopedia
  • "Eugene de Mazenod (1782-1861) - biography". Vatican Basilica. 3 Desemba 1995. Iliwekwa mnamo 2007-03-09.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Biography of Eugene de Mazenod at OMI Lacombe
  • Biography of St. Eugene de Mazenod from American Catholic.org Ilihifadhiwa 29 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
  • Biography of St. Eugene de Mazenod Ilihifadhiwa 12 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine. from the Oblate Missions Website Ilihifadhiwa 22 Machi 2022 kwenye Wayback Machine. of National Shrine of Our Lady of the Snows website Ilihifadhiwa 10 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine. of The Missionary Oblates of Mary Immaculate
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.