Fatma Karume

Mwanasheria kutoka Tanzania

Fatma Karume (amezaliwa 15 Juni 1969) ni mwanasheria wa Kitanzania na wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019. Alipata wadhifa huo baada ya kushinda katika uchaguzi wa uraisi wa chama hicho uliofanyika Aprili 2018 na hivyo kumrithi mtangulizi wake Tundu Lissu aliyekiongoza chama hicho kutoka mwaka 2017 hadi 2018. [1][2][3]

Fatma Karume
Nchi Bendera ya Tanzania Tanzania
Kazi yake mwanasheria

Katiba ya chama cha TLS huruhusu kuongoza kwa muda wa mwaka mmoja tu. Rugemeleza Nshala alichaguliwa katika uchaguzi huo kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.[4] Hivyo alikuwa rais wa TLS hadi mwaka 2019 Dr. Rugemeleza Nshala alipochaguliwa kuwa rais mpya.[5]

Maisha

Fatma Karume ni mtoto wa raisi mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume[6] na mjukuu wa raisi wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume.

Elimu

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari alianza kusoma sheria huko Strasbourg, Ufaransa hadi 1991. Mwaka 1992 akaendelea kupata shahada ya awali ya sheria kwenye Chuo Kikuu cha Sussex[7][8]. Mwaka 1994 alikubaliwa kuwa wakili katika Tanzania bara na Zanzibar, mwaka 1997 alipata Shahada ya uzamivu katika sheria (LLM) kwenye Chuo cha Uchumi London mwaka 1997 akapokelewa katika uwakili mjini London[9].

Anaongea kwa ufasaha lugha tatu ambazo ni: Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa[10].

Kazi

Fatma Karume ni mwenza katika kampuni ya mawakili ya IMMMA yenye makao makuu katika jiji la Dar es Salaam, Tanzania[11].

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika nyanja ya sheria[12]. Ni mbobezi katika sheria za kodi na ameshawahi kuwakilisha benki kubwa katika kesi mbalimbali.

Amepata hitilafu nyingi kutoka serikalini tangu aanze uharakati wake juu ya uhuru wa kujieleza ambao aliona unapotea kwa kasi na hivyo kujipatia umaarufu sana katika Twitter kama Shangazi akiwa na wafuasi zaidi ya laki tisa kuanzia mwaka 2018.

Fatma Karume ni kati ya wachache ambao walisema mashoga wana haki pia mbele ya sheria na Paul Makonda hana haki wala mamlaka ya kuamua tu watu wakamatwe kwa kushtukiwa kuwa shoga.

Pia ni mtetezi wa haki za wanawake akipinga mfumo dume ambao umetawala sana siasa na utamaduni wa Tanzania.

Ofisi yake ilipigwa bomu ikiwa ni moja ya mashambulio dhidi yake. Aliondolewa uraisi wa TLS na mnamo Septemba 2020 alifutwa kabisa kwenye orodha ya mawakili ili asiweze kufanya kazi tena nchini. Lakini hii haijamzuia Fatma kuendelea na msimamo wake na harakati zake.

Tarehe 23 Septemba 2020 alifutwa katika orodha ya mawakili, lakini baada ya siku 243 Mahakama Kuu imetoa hukumu ya kuwa uamuzi huo ulikuwa batili[13]

Marejeo

  1. https://www.voaswahili.com/a/fatma-karume-apata-ridhaa-ya-tundu-lissu/4314328.html
  2. http://parstoday.com/sw/news/africa-i43134-fatma_karume_ashinda_urais_wa_chama_cha_wanasheria_tanganyika
  3. https://globalpublishers.co.tz/breaking-news-fatuma-karume-ashinda-urais-wa-tls
  4. https://globalpublishers.co.tz/breaking-news-fatuma-karume-ashinda-urais-wa-tls
  5. "TLS yapata rais mpya, asikitika Lissu kupigwa risasi mchana". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-11.
  6. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Fatma-Karume--Nitafanya-mambo-haya-TLS/1597578-4395578-rn1qtr/index.html
  7. Chuo Kikuu cha Sussex
  8. "The Legal 500 > IMMMA Advocates > Dar es Salaam, TANZANIA > Lawyer profiles > Fatma Amani Karume". www.legal500.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-11. Iliwekwa mnamo 2019-07-11.
  9. Fatma Karume, Senior Partner, tovuti ya IMMA advocates, iliangaliwa Septemba 2019
  10. "IMMMA Advocates". IMMMA Advocates (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-11.
  11. "The Legal 500 > IMMMA Advocates > Dar es Salaam, TANZANIA > Lawyer profiles > Fatma Amani Karume". www.legal500.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-11. Iliwekwa mnamo 2019-07-11.
  12. "IMMMA Advocates". IMMMA Advocates (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-11.
  13. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/kishindo-cha-fatma-karume-baada-ya-siku-243-kusimamishwa-uwakili-3447288
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatma Karume kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.