Gregori Yohane Barbarigo (Venezia, leo nchini Italia, 16 Septemba 1625Padova, 17 Juni 1697) alikuwa askofu na kardinali.

Mt. Gregori alivyochorwa na Giovanni Raggi.

Papa Klementi XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 16 Julai 1761 na Papa Yohane XXIII mtakatifu tarehe 26 Mei 1960.

Sikukuu yake huadhimishwa kwenye tarehe 18 Juni[1]

Maisha hariri

Muda mfupi baada ya upadrisho (21 Desemba 1655) aliitwa na Papa Aleksanda VII mjini Roma akafanywa mwenyekiti wa kamati ya kuhudumia waliopatwa na tauni. Hapo alijitosa kuwatembelea, kuwasaidia na kuwazika mwenyewe.

Mwaka uliofuatwa alifanywa askofu wa Bergamo. Alikataa mashangilio, akaagiza pesa ambazo zingetumika zigawiwe kwa fukara. Halafu mwenyewe aliuza mali yake yote kuwasaidia.

Tarehe 5 Aprili 1660 alifanywa kardinali.

Tarehe 24 Machi 1664 alihamishiwa jimbo la Padova ambalo aliliongoza miaka 33 akitembelea parokia zote 320.

Mkarimu kwa wote na mgumu kwake mwenyewe, alianzisha seminari kwa malezi ya miito na shule nyingi, alifundisha katekisimu kwa watoto katika kilugha chao, aliendesha sinodi ya kijimbo na kujadiliana na mapadri wake [2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum, Libreria Editrice Vaticana (2001), ISBN 88-209-7210-7
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/58050

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.