Historia ya Vietnam

Historia ya Vietnam inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam.

Nchi ilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe.

Milki jirani ya China hariri

Vietnam ilitawaliwa kwa karne kadhaa kutoka China kuanzia karne ya 2 KK. Athira ya utamaduni Wa China ilibaki muhimu hata katika uhuru.

Katika karne ya 18 nchi iliunganishwa chini ya makaisari wa mji wa Hue.

Koloni la Ufaransa hariri

Athira ya Ufaransa ilikua na kati ya miaka 1858 na 1883 utawala wa nchi ulichukuliwa na Ufaransa. Kusini mwa nchi kulikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Cochinchina. Annan (eneo la Vietnam ya Kati) na Tongking (kaskazini) zilikuwa nchi lindwa chini ya utawala wa kaisari wa Hue lakini hali halisi mamlaka ilikuwa mikononi mwa Ufaransa.

 
Hekalu la Kibuddha.

Vita vya ukombozi hariri

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Vietnam ilitwaliwa na Japani iliyoacha maafisa Wafaransa wa serikali ya Víchy ofisini lakini kushika utawala wa juu.

Kundi la Viet Minh walioongozwa na Mkomunisti Ho Chi Minh waliwapinga kwa njia ya vita vya msituni.

Mwaka 1945 Japani ilijaribu kutumia Wavietnam upande wake ukaondoa Wafaransa madarakani na kumtangaza Kaisari Bao Dai wa Hue mtawala wa Vietnam huru.

Lakini baada ya miezi michache vita vikaisha na Ho Chi Minh alitangaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam mjini Hanoi. Wafaransa wa serikali ya Paris walijaribu kujenga uhusiano naye lakini baada ya kurudi walilenga kuchukua utawala upya.

Vita vya kupigania uhuru vilifuata hadi mwaka 1954 Ufaransa uliposhindwa.

Kipindi cha Vietnam mbili hariri

Vietnam iligawiwa katika Vietnam Kaskazini na Vietnam Kusini. Jeshi na watawala wa kikoloni wa Ufaransa waliondoka kabisa. Wavietnam wengi wa kaskazini, hasa Wakristo, walioogopa serikali ya kikomunisti walikimbilia kusini.

Lakini uchaguzi huru uliokubaliwa huko Geneva haukutekelezwa kwa sababu serikali za kidikteta za kusini zilikataa.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianzishwa na wakomunisti wa kaskazini waliosaidiwa na China na Umoja wa Kisovyeti dhidi ya serikali ya kusini iliyopata msaada wa Marekani.

Kaskazini kuteka Kusini na kuunganisha taifa hariri

Katika vita vya Vietnam majeshi ya Marekani na Vietnam Kusini yalishindwa.

Tarehe 30 Aprili 1975 jeshi la Vietnam Kaskazini lilitwaa mji wa Saigon. Nchi yote iliunganishwa kama Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam tarehe 2 Julai 1976.

Nchi ilianza kubadilika mwaka 1986 kwa kuanza mahusiano na nchi zisizo za kikomunisti, na tangu hapo imepata maendeleo makubwa.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Vietnam kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.