Karolo wa Sezze
Karolo wa Sezze (Sezze, leo katika wilaya ya Latina, Italia, 19 Oktoba 1613 - Roma, 6 Januari 1670), alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wareformati aliyeandika vizuri sana kuhusu maisha ya kiroho.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.[1]
Alitangazwa kwanza mwenye heri na Papa Leo XIII mwaka 1882, halafu mtakatifu na Papa Yohane XXIII tarehe 12 Aprili 1959.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, 6 Januari, au kesho yake[2].
Maisha
haririJina la kuzaliwa lilikuwa Giancarlo Marchioni. Tangu utotoni alilazimika kujitafutia riziki akahimiza wenzake kumuiga Yesu na watakatifu wake[3]. Alipokuwa kijana alitamani kwenda India kama mmisionari.
Kisha kuvutwa na maisha ya watakatifu mabradha Wafransisko Paskali Baylon na Salvador wa Horta, aliamua kujiunga na shirika lao, alipokubaliwa mwaka 1635.
Baadaye alieleza kuwa alifanya hivyo ili kuishi kifukara na kuombaomba "kwa upendo wa Kristo".[4] Pia alikuwa na heshima ya pekee kwa Yesu Ekaristi[5].
Karolo aliishi katika jumuia mbalimbali kama bradha, asiombe kamwe upadrisho: alikuwa mpishi, bawabu, mtunzasakristia, mtunzabustani na ombaomba. Kwa kukosa ufundi katika kazi hizo zote, alijulikana kwa sababu ya kuuunguza jiko zima.[4]
Akiwa bawabu, siku moja alikatazwa na mlinzi wa jumuia asitoe chakula kwa wasio watawa. Karolo alitii, lakini mara moja misaada iliyotolewa kwa jumuia ilipungua sana. Hapo alimsaidia mlinzi kutambua uhusiano kati ya mambo hayo mawili. Aliporuhusiwa tena kusaidia maskini, misaada kwa jumuia iliongezeka tena.[4]
Ingawa hakuwa padri, Karolo aliagizwa na muungamishi wake kuandika habari za maisha yake. Ndivyo kilivyopatikana kitabu Makuu ya Rehema za Mungu ambacho kilienea na kusomwa sana.
Vilevile alipaswa kutoa mashauri ya kiroho kwa watu mbalimbali akaandika vitabu vya namna hiyo. Papa Klementi IX alipokuwa mahututi alimuita ili kupata faraja na baraka yake.[4]
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Patron Saints Index: "Saint Charles of Sezze"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-23. Iliwekwa mnamo 2013-07-21.
- ↑ Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana 2001 ISBN 88-209-7210-7)
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 "Saint of the Day: Charles of Sezze". AmericanCatholig.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-02-01. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
hariri- Donald Attwater and Catherine Rachel John (1995). The Penguin Dictionary of Saints, 3rd Edition. New York: Penguin Books. ISBN 0-14-051312-4.
- Raphael Brown (1960). The Wounded Heart: St. Charles of Sezze. Chicago: Franciscan Herald Press. OCLC 3247159.
- St. Charles of Sezze (1963). St. Charles of Sezze: an autobiography, Leonard Perotti (trans). London: Burns & Oates. OCLC 221056796.
Viungo vya nje
hariri- Patron Saints Index: Saint Charles of Sezze Archived 6 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- Catholic Online - Saints & Angels: St. Charles of Sezze
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |