Malkia wa Mbingu katika sanaa

Malkia wa Mbingu (kwa Kilatini: Regina caeli; tamka: reˈdʒina ˈtʃeli) ni sifa mojawapo ya Bikira Maria katika Kanisa la Kilatini inayotumika hasa katika sala maalumu ya wakati wa Pasaka, kuanzia Dominika ya Ufufuko wa Yesu hadi Pentekoste.

Mchoro wa kale zaidi (karne ya 6) wa Santa Maria Regina (Mtakatifu Maria Malkia), kanisa la Santa Maria Antiqua, Roma, Italia.

Katika siku hizo hamsini Malkia wa Mbingu [1] ndiyo antifona pekee inayotumika kumalizia Sala ya mwisho ya Liturujia ya Vipindi [2] lakini pia inashika nafasi ya sala ya Malaika wa Bwana (inayotumika karibu mwaka mzima mara tatu kwa siku: asubuhi, adhuhuri na jioni).

Uenezi wa sala hiyo umechangia kiasi chake kufanya wasanii wajitokeze kumchora au kuchonga sanamu ya Maria akiwa anatawazwa au ameshatawazwa kama malkia.

Picha hariri

Michoro hariri

Sanamu hariri

Michoro ya ukutani hariri

Altare hariri

Tanbihi hariri

  1. Loyola Press: Regina Caeli. Re-accessed Oct 2021.
  2. "Finally one of the antiphons of the Blessed Virgin Mary is said. In Eastertide this is always the Regina caeli" (General Instruction of the Liturgy of the Hours, p. 18, paragraph 92).

Vyanzo hariri

  • Fastenrath, E.; Tschochner, F. (1991). "Königtum Mariens". Katika Bäumer, Remigius; Scheffczyk, Leo. Marienlexikon (kwa Kijerumani) 3. EOS Verlag. ku. 589–596. ISBN 9783880968936. 

Viungo vya nje hariri