Maria Magdalena Postel

Maria Magdalena Postel, ambaye jina la kiraia kwa Kifaransa lilikuwa Julie Françoise-Catherine Postel (Barfleur, Ufaransa, 28 Novemba 1756 - Saint-Sauveur-le-Vicomte, 16 Julai 1846) alikuwa mwanamke ambaye mwaka 1807 alianzisha shirika la Masista wa Shule za Kikristo wa Huruma (Congrégation des sœurs des Écoles chrétiennes de la Miséricorde) kwa ajili ya malezi ya Kikristo ya wasichana fukara [1].

Sanamu ya Marie-Madeleine Postel, Basilika la Utatu, Cherbourg.

Alitangazwa na Papa Pius X kuwa mwenye heri mwaka 1908 akatangazwa na Papa Pius XI kuwa mtakatifu tarehe 24 Mei 1925.

Sikukuu yake inaadhimishwa siku ya kifo chake, 16 Julai[2].

Maisha hariri

Mwaka 1774 huko Barfleur Julie Postel alifungua shule ya wasichana ambayo wakati wa mapinduzi ya Ufaransa ilitumika kwa shughuli za kidini za siri za Wakatoliki waliokataa masharti ya serikali yaliyo.

Baada ya dhuluma kwisha, aliendelea kufundisha na kufanya kazi nyingine za huruma.

Alipofikia umri wa miaka 51 aliweka nadhiri kwa jina la sista Maria Magdalena akaandaa uanzishaji wa shirika.

Miaka ya kwanza mafanikio yalikuwa madogo, lakini mwaka 1830 alifaulu kununua monasteri ya zamani huko St-Sauveur-le-Vicomte iwe makao makuu.

Shirika lilikubalika rasmi mwaka 1837 likabaki chini ya usimamizi wa mwanzilishi hadi mwaka wake wa mwisho.[3]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91039
  2. Martyrologium Romanum
  3. Donald Attwater. The Penguin Dictionary of Saints (Penguin Reference Books), 1965; pp. 237-38.

Marejeo hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • Pierre de Crisenoy, Sainte Marie-Madeleine Postel, Paris, Bonne Presse, 1938
  • Georges Grente, Une Sainte normande, Marie-Madeleine Postel, Paris, Bonne Presse, 1945
  • Abbé François-Augustin Delamare, Vie édifiante de la très honorée supérieure Marie-Madeleine, née Julie Postel, réédition le Livre d'histoire, 2005; ISBN 2-8437-3726-5
  • Wilhelm Hünermann Die Seilerstochter von Barfleur: Lebensbild der heiligen Maria-Magdalena Postel. Freiburg im Breisgau: Herder, 1956
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.