Mikaeli Garicoits

(Elekezwa kutoka Mikaeli Garikoitz)

Mikaeli Garicoits (kwa Kieuskara Mixel Garikoitz, kwa Kifaransa Michel Garicoïts), alikuwa padri wa Ufaransa mwenye asili ya Kibaski (Ibarre, 15 Aprili 1797 - Betharram, 14 Mei 1863)

Alivyochorwa.

Papa Pius XI alimtangaza kuwa mwenye heri tarehe 15 Machi 1923, halafu papa Pius XII kuwa mtakatifu tarehe 6 Julai 1947.

Sikukuu yake huadhimishwa siku ya kifo chake, tarehe 14 Mei[1].

Maisha

hariri

Mixel alizaliwa na familia iliyobaki aminifu kwa Papa wakati wa dhuluma ya kidini iliyofuatana na mapinduzi ya Ufaransa.

Mtoto wa kwanza kati ya sita, Mixel alikuwa akisali na kuimba tenzi wakati wa kuchunga mifugo.

Alipofikia umri wa miaka 13 alitumwa kama boi kwenye shamba lingine, huko Oneix, alipojiandaa na hatimaye kupokea ekaristi kwa mara ya kwanza tarehe 9 Juni 1811.

Akiwa na nia ya kuwa padri, alihudhuria shule huko Saint-Palais, akisoma Kilatini na Kifaransa mpaka usiku kwa kutumia mishumaa.

Garicoits alijiunga na seminari ndogo ya Aire-sur-Adour, halafu ile kuu ya Dax. Akiwa bado masomoni, aliombwa kufundisha katika seminari ndogo ya Larressore.

Alipata upadrisho katika kanisa kuu la Bayonne tarehe 20 Desemba 1823.

Alipinga Ujanseni katika parokia yake ya Cambo alipofanya uchungaji miaka miwili, halafu akahamishiwa Bétharram akafundishe falsafa.[2]

Mapadri wa Betharram

hariri

Bétharram, chini ya milima ya Pirenei, maili 8 kutoka Lourdes, ilikuwa na patakatifu pa zamani pa Bikira Maria.

Mwaka 1833 askofu alifunga seminari ya Bétharram na padri Mixel aliachwa huko kuhudumia patakatifu na umati wa watu waliokwenda huko kuhiji.

Hivyo mwaka 1838 Mixel aliweza kutimiza ndoto yake ya kuanzisha shirika la mapadri na mabradha lililowekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Lengo la kulianzisha lilikuwa kuinjilisha watu kwa kuhubiri huko na huko na kwa kufundisha vijana.[2]

Mixel alifariki tarehe 14 Mei 1863.[2]

Baada ya kifo chake, shirika lilikubaliwa na Papa Pius IX tarehe 5 Septemba 1877.

Mwaka 2012 lilikuwa na wanachama 316, kati yao mapadri 212.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Martyrologium Romanum
  2. 2.0 2.1 2.2 ""St. Michael Garicoits", Olton Friary". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-05. Iliwekwa mnamo 2016-03-08.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.