Paramaribo
Paramaribo (jina fupi: Par'bo) ni mji mkuu wa Surinam.
Jiji la Paramaribo | |
Nchi | Surinam |
---|
Iko kando ya mto Surinam takriban km 20 kutoka mwambao wa Bahari ya Karibi. Anwani ya kijiografia ni 5°52' N, 55°10' W.
Ina wakazi 250,000, karibu nusu ya wakazi wa nchi.
Kiini cha mji huo kimeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia mwaka 2002.
Historia
haririJina la Paramaribo limetokana na kijiji cha wakazi asilia "Parmirbo". Mwaka 1613 Waholanzi walijenga kituo cha biashara karibu na kijiji hicho. Mwaka 1651 eneo lilikuwa chini ya utawala wa Uingereza waliojenga hapa Fort Willoughby. Waholanzi walirudi mwaka 1667 wakatwaa eneo lote na kuita kituo Fort Zeelandia na kijiji mbele yake "Nieuw Middelburgh". Mwaka 1683 nyumba 27 zilihesabiwa zilizoongezeka hadi mwaka 1790 kuwa zaidi ya 1000.
Mji wa kale ulichomwa moto mara mbili (1821 na 1832).
Baada ya mwisho wa utumwa mwaka 1863 wengi waliowahi kuwa watumwa walihamia mjini na kusababisha kukua kwa Paramaribo. Tangu mwaka 1975 imekuwa mji mkuu wa Surinam huru.
Uchumi
haririBiashara ya nje kutoka Paramaribo ni hasa boksiti, sukari, mpunga, kokoa, kahawa na ubao. Kuna viwanda vya saruji, rangi na bia.
Utamaduni
haririUtamaduni wa Paramaribo una pande nyingi kutokana na mchanganyiko wa watu wenye asili ya Uhindi, Afrika, Indonesia, Uchina na Ulaya.
Wenyeji wanapenda mashindano ya uimbaji wa ndege wanaofugwa kwa kusudi hilo. Mashindano hayo hutokea kila Jumapili.
Viungo vya nje
hariri- Map of Paramaribo
- Page with some basic information and images
- Small Paramaribo gallery
- Clickable map
- (Kiingereza) Audio interview with Paramaribo resident about life in Paramaribo Archived 17 Novemba 2007 at the Wayback Machine.
- Image gallery Archived 12 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- Paramaribo photo gallery
- Photo gallery
- 1st gamers site in surinam Archived 24 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Paramaribo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |