Papa Silverio

(Elekezwa kutoka Silverius Mtakatifu)

Papa Silverio alikuwa Papa kuanzia tarehe 8 Juni 536 hadi mwaka 537[1]. Alitokea Frosinone, Italia[2].

Mt. Silveri.

Alimfuata Papa Agapeto I akafuatwa na Papa Vigilio.

Alizaliwa na Papa Hormisdas katika ndoa yake kabla ya kupata upadrisho.

Aliondoshwa madarakani mnamo mwezi Machi 537 kwa nguvu ya Theodosia, mke wa Kaisari wa Bizanti, aliyempendelea Vigilio. Alijiuzulu tarehe 11 Novemba 537.

Silverio alifungwa na kupelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Palmarola alipofariki kwa njaa tarehe 2 Desemba 537.

Angalau tangu karne ya 11 ameheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 2 Desemba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Marejeo mengine hariri

  • Louise Ropes Loomis, The Book of Popes ("Liber Pontificalis"). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8 (Reprint of the 1916 edition. English translation with scholarly footnotes, and illustrations).

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Silverio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.