Mapigano ya Tanga

(Elekezwa kutoka Vita vya Tanga)

Mapigano ya Tanga, ambayo hujulikana pia kama Mapigano ya Nyuki, yalitokea kati ya majeshi ya Ujerumani na Milki ya Uingereza wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia tarehe 2 hadi 4 Novemba 1914 huko Tanga, mji wa bandari wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, leo Tanzania. Tokeo lake lilikuwa ushindi wa upande wa Kijerumani.

Mapigano ya Tanga.

Yalianza kama shambulio ambalo halikufaulu wakati kikosi cha Uingereza, BritishIndian Expeditionary Force "B", chini ya Meja Jenerali AE Aitken walijaribu kuteka mji wa Tanga katika Afrika Mashariki ya Ujerumani, mwanzoni mwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kitendo hicho kilifanyika sambamba na mpango wa kuteka Longido, huko Mkoa wa Kilimanjaro, na kikosi kingine cha uvamizi, Force "C". Kilikuwa kitendo kikuu cha kwanza cha vita katika Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki na Waingereza walishindwa na kikosi kidogo sana cha askari wa Ujerumani na wakoloni wa kujitolea chini ya Luteni Kanali Paul von Lettow-Vorbeck.

Ofisi ya Mkoa wa Tanga mnamo 1914.

Ushindi huo unahesabika kama moja ya ushindi mkubwa wa Schutztruppe barani Afrika. Kurudisha nyuma jeshi la Waingereza, Schutztruppe walipata vifaa ya kazi na vya kutibu, mahema, mablanketi, vyakula na idadi ya bunduki za mashine, ili kuendelea kupigana na washiriki wa adui katika vita mpaka mwisho.

Utangulizi

hariri
 
HMS Fox kulia.
 
Tom na Magdalene von Prince, kabla ya mwaka 1908.

Mji wa Tanga uko kilometa 80 (maili 50) tu, kutoka mpaka wa Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (hasa Kenya ya leo). Mji wa Tanga ulikuwa na harakati nyingi ya bandari, na ulikuwa kituo cha bahari cha reli muhimu cha Usambara, kutoka Tanga mpaka Neu Moshi, chini ya Mlima Kilimanjaro. Mpango ulikuwa kupiga Tanga kwanza na mabomu ya manowari za Uingereza, lakini wazo hilo lilibadilishwa. Kabla yake, kulikuwa tayari na mapatano baina Ujerumani na Uingereza kuweka miji mikubwa ya Dar es Salaam na Tanga kwa usalama, lakini sasa mapatano hayo yaligeuzwa na kuonekana "ingekuwa sawa kuwaonya Wajerumani mapatano hayo yamekwisha"[1]

Badala yake, Waingereza waliamua kuteka Tanga na Wajerumani kwa shambulio la bahari na la nchi kavu, yote mbili pamoja.[2] Mpango huu, tofauti na mpango ulioandikwa, ulibadilisha shambulio hilo kuwa mchafuko. Siku ya 2 Novemba 1914, meli ya vita ya Uingereza, HMS Fox, iliwasili bandarini. Kamanda wa meli hiyo, Kapteni Francis Wade Caulfeild, alishuka nchini na akampa Tanga saa moja kujisalimisha na kushusha bendera ya kifalme. Kabla ya kurudi, alitaka kujua kwamba mabomu ya baharini yalikuwa yamelazwa bandarini; hakuwa hivyo, lakini aliambiwa, kweli, ndivyo. [3] Baada ya saa tatu, bendera ilikuwapo bado upeponi, haijashushwa, na meli ya Fox iliondoka kuleta nguvu ya Force "B", usafirishaji wa vikosi kumi na vinne.[4] Kituo hicho kiliwapa Schutztruppe na raia wa Tanga nafasi ya kujiandaa kwa shambulio. Kamanda wa Ujerumani, Luteni Kanali Paul Emil von Lettow-Vorbeck, alifanya haraka kufika Tanga. Yeye aliimarisha ulinzi (awali kulikuwa kampuni moja tu ya askari) kwa kuongeza askari waliopelekwa kwa reli kutoka Neu Moshi, hatimaye kuhesabu watu 1,000 katika kampuni sita. Naibu wake alikuwa Kapteni Tom von Prince, ambaye zamani alikuwa na Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki (kwa Kijerumani: Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft(DOAG))

 
Mapigano ya askari, 1914, labda huko Tanga.

Kapteni Caulfeild alitoa amri kufagia nyaya za mabomu ya baharini kwa bandari siku ya 2 Novemba, na hata siku ya pili. Wakati wa kufagia, kamanda wa Force "B", Aitken, alianza kutua, bila upinzani, wanajeshi na vifaa katika vikundi viwili bandarini, na maili tatu mashariki mwa mji, kwenye pwani bila mabomu ya ardhini.[5] Jioni ya tarehe 3 Novemba, karibu wote wa kikosi cha uvamizi walikuwa tayari katika pwani.[6] Saa sita mchana siku ya Novemba 4, Aitken aliwaamuru wanajeshi wake kuandamana mjini. Walinzi waliokuwa wamejifichia vizuri walikata mapema maendeleo yao. Si kitambo kirefu baadaye, vita hivyo viligeuka kuwa mapigano ya kundi la kusini, kati ya mashamba ya minazi na mipira, na mapigano makali ya barabara mjini na jeshi la bandari. Wanajeshi wa Wagurkha, Wakashmiri na Walancashire walifanya mwendo mzuri kwa bandari; waliingia mjini, wakateka nyumba ya forodha, na Hoteli ya Deutscher Kaiser, na walipandisha bendera ya Uingereza, Union Jac. Lakini baadaye walisimamishwa mapema.[7] Vikosi vya Wahindi wa 27 (Bangalore) Brigade walioongozwa vibaya na wenye zana za jeshi hafifu walitawanyika wakatoroka. Wanajeshi wa miguu wa 98th Infantry walirukiwa na makundi ya nyuki na kuvunjika. Nyuki waliwashambulia Wajerumani pia, ndiyo sababu ya jina la utani la vita hivyo.[8] Propaganda ya Uingereza ilianza uvumi wa uwongo kwamba Wajerumani walipanga njama mbaya, na walisetiri nyaya za kikwazo kuchochea mizinga ya nyuki.[9] Kundi la Warajput walikosa sana kushirikiana vizuri katika vita kwa sababu ya kuvunjika mioyo yao baada ya kushuhudia rejeo la wanajeshi wa kundi la Palamcottah Light Infantry.

 
Wanajeshi Wahindi wa kikosi cha Britania waliokufa kwenye pwani huko Tanga.

Wakoloni wa kujitolea wa kampuni ya 7 na 8 ya Schützenkompanien [kampuni za bunduki] walifika kwa reli ili kukaza mistari ya askari iliyobanwa. Schützenkompanie wa 8, ambao kwa kawaida walikuwa wenye farasi, walikuwa wameacha farasi wao huko Neu Moshi. Alasiri ya 4 Novemba, Lettow-Vorbeck aliamrisha mwisho wa wajeshi wa akiba wake, ya namba ya 13 na ya 4 Askari Feldkompanien (kampuni za shamba) - ya 4 ilikuwa imekwisha fika Tanga kwa gari la moshi - ili kuzunguka ubavu na kinyume cha Waingereza kwa mashambulio ya bayoneti upande mzima wa mbele, pamoja na mlio wa "baragumu na sauti kuu ya kelele za kikabila za vita." Utaratibu wote ulikwisha wakati Force B ilirudishwa nyuma, mpaka "kukoma na kumalizika kabisa."[10]

Kuwa wajeshi wanane kwa mmoja, baadhi ya maafisa wa Ujerumani walifikiwa na tahadhari. Mfululizo wa makosa yaliyofanywa na milio ya baragumu, na kutokuelewana kwa afisa ili kujiondoa na kujumuisha, askari badala yake waliondoka kwenda kambini Kange, maili kadhaa magharibi mwa Tanga. Lettow-Vorbeck alipogundua hiyo, mara moja alibatilisha hatua hiyo akaamuru utumo mpya ambao haukukamilika mpaka alfajiri. "Kwa karibu usiku kucha [kabla ya asubuhi 5 Novemba], Aitken alikuwa na uwezo wa kuchukua mji wa Tanga. Ilikuwa kejeli kubwa sana ya vita hivi."[11]

Matokeo

hariri

Kwa kukasirika na kufadhaika, Aitken aliamuru uondoaji wa jumla.[12] Kati ya kujihamisha na kurudi kwa usafirishaji, iliyoendelea hadi usiku, askari wa Britania waliacha karibu vifaa vyao vyote. "Lettow-Vorbeck aliweza kuzipatia kampuni tatu za askari na silaha za bunduki za kisasa, ambazo zilikuwa na risasi 600,000 pia. Tena alikuwa na bunduki za mashine kumi na sita zaidi, na simu za shamba zenye faida", na mavazi ya kutosha Schutztruppe mwaka mmoja mzima.[13] Asubuhi ya Novemba 5, afisa wa Force B - Kapteni Richard Meinertzhagen - aliingia Tanga chini ya bendera nyeupe, pamoja na vifaa vya matibabu, na alileta barua kutoka kwa Jenerali Aitken kuomba msamaha kwa kupiga hospitali kwa bomu. Barabara za Tanga zilikuwa zimejaa wafu na majeruhi. Daktari wa Ujerumani na waaguzi wao Waafrika walifanya kazi bila kupumzika na "bila kutazama rangi za nguo za wagonjwa wao."[14]

Wema wa ulinzi wa Tanga ulikuwa kitendo cha kwanza kati ya mafanikio mengi ya Paul von Lettow-Vorbeck katika kampeni yake ndefu huko Afrika Mashariki. Lakini kwa Waingereza, vita hivyo vilikuwa kama msiba, na iliandikwa katika 'Official History of the War' (Historia rasmi ya Vita) ya Britania kama "mojawapo ya makosa makubwa katika historia ya jeshi la Uingereza."[13] Walihesabiwa majeruhi 487, na wafu 360, upande wa Uingereza; [14] Schutztruppe walipotewa na Wajerumani 16, na askari 55 waliouawa, kwa jumla waliojeruhiwa walifika 76.[15]

Awali, Paul von Lettow-Vorbeck alikadiria idadi ya Waingereza waliouawa kama 800, lakini baadaye alisema kwamba alidhani idadi hiyo kuwa zaidi ya 2,000. Halafu, Wajerumani waliweka huru maafisa wa Uingereza ambao walikuwa wamejeruhiwa au kukamatwa, baada ya hawa kuahidi hawatapigana tena wakati wa vita.[16]

Tanbihi

hariri
  1. Farwell 1989, p. 166.
  2. Aitken's orders: "The object of the expedition under your command is to bring the whole of German East Africa under British authority." See Farwell 1989, p. 163.
  3. Farwell 1989, p. 167.
  4. Miller 1974, p. 58.
  5. Miller 1974, p. 59.
  6. Farwell 1989, p. 168.
  7. Farwell 1989, p. 170.
  8. Farwell 1989, p. 171.
  9. Hoyt 1981, p. 50.
  10. Miller 1974, p. 68.
  11. Miller 1974, p. 69.
  12. Hoyt 1981, p. 52.
  13. 13.0 13.1 Farwell 1989, p. 178.
  14. 14.0 14.1 Miller 1974, p. 70.
  15. Miller 1974, p. 71.
  16. von Lettow-Vorbeck, Paul (1920). Meine Erinnerungen aus Ostafrika. Hase & Köhler., p. 39/40

Marejeo

hariri
  • Byron Farwell|Farwell, Byron. The Great War in Africa, 1914–1918. New York: W. W. Norton & Company, 1989.
  • Hoyt, Edwin P. Guerilla: Colonel von Lettow-Vorbeck and Germany's East African Empire. New York: Macmillan Publishing Co., Inc. 1981; and London: Collier Macmillan Publishers. 1981.
  • Miller, Charles. Battle for the Bundu: The First World War in German East Africa. London: Macdonald & Jane's, 1974; and New York: Macmillan Publishing Co., Inc. 1974.
  • Paice, Edward. Tip and Run: The Untold Tragedy of the Great War in Africa. London: Weidenfeld & Nicolson, 2007.
  • von Lettow-Vorbeck, Paul. My reminiscences of East Africa. London: Hurst, 1920, https://archive.org/details/meineerinnerunge00lettuoft

Masomo zaidi

hariri
  • Anderson, Ross. 2001. "The Battle of Tanga, 2–5 November 1914". War in History. 8, no. 3: 294–322.
  • Anderson, Ross. Anderson, Ross. The Battle of Tanga 1914. Stroud, Gloucestershire: Tempus, 2002.
  • Harvey, Kenneth J. Harvey, Kenneth J. The Battle of Tanga, German East Africa 1914. [Washington, DC]: Storming Media, 2003
  • Page, Melvin E. (Melvin Eugene). 2003. "The Battle of Tanga 1914 (Review)". Journal of Military History. 67, no. 4: 1307–1308.