Yohane wa Kety
Yohane wa Kety (kwa Kipolandi Jan z Kęt au Jan Kanty) (23 Juni 1390 - 24 Desemba 1473) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki, mwanafalsafa, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka Poland.
Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 28 Machi 1676. Halafu Papa Klementi XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767[1].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Desemba,[2][3] lakini pia 20 Oktoba.
Maisha
haririAlizaliwa Kęty, karibu na Oświęcim, Poland.
Baada ya kusoma chuo kikuu cha Kraków alipopata digrii mbili[4], mwaka 1418 alifikia udaktari wa falsafa.[5]
Miaka 3 iliyofuata alifundisha falsafa na kujiandaa kwa upadrisho.
Baadaye akawa gombera katika shule ya Wakanoni huko Miechow[5], akarudi Krakow kufundisha Sacrae Scripturae (Maandiko Matakatifu). Pia alipata udaktari wa teolojia na kuwa mkuu wa idara hiyo.
Yohane alitumia muda mrefu kunakili vitabu vya Biblia, teolojia n.k.
Katika fizikia, alisaidia kuendeleza theory of impetus ya Jean Buridan, akitangulia michango ya Galileo Galilei na Isaac Newton.
Huko Kraków, alijulikana sana kwa huruma na ukarimu wake kwa maskini, hasa wanafunzi wa chuo kikuu wenye shida. Alijipatia mahitaji halisi tu, ili kugawa mara kwa mara misaada kwa mafukara.
Mara moja alihiji hadi Yerusalemu na mara nne alihiji kwa miguu hadi Roma.[4]
Aliendelea kufundisha hadi kifo chake mwaka 1473, alipokuwa na umri wa miaka 83.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Patron Saints Index: "Saint John Cantius"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-18. Iliwekwa mnamo 2016-10-23.
- ↑ Calendarium Romanum (Libreria Editrice 1969), p. 111
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 4.0 4.1 Godrycz, J. (1910). "St. John Cantius". The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
- ↑ 5.0 5.1 ""St. John Kanty", Catholic Faith Community of Saint John Cantius, St. Cloud, Minnesota". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-29. Iliwekwa mnamo 2016-10-23.
Viungo vya nje
hariri- media kuhusu Yohane wa Kety pa Wikimedia Commons
- Biography from the Canons Regular of Saint John Cantius Archived 26 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
- Bull of Canonization (1767) by Pope Clement XIII Archived 4 Septemba 2012 at the Wayback Machine.
- Novena to Saint John Cantius Archived 26 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
- Biography at The Catholic Forum Archived 3 Januari 2006 at the Wayback Machine.
- Patron Saints Index: Saint John Cantius Archived 18 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
- The Saints: A concise Biographical Dictionary, (ed. John Coulson), Hawthorn Books, Inc. 1960 Archived 19 Aprili 2017 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |