Adhana
Adhana (neno hili asili yake ni Kiarabu أَذَان) ni wito maalumu wa kuwaita Waislamu kwenda kusali. Kwa kawaida Waislamu huwa na vipindi vitano vya ibada hasa katika sala za lazima (faradhi), hivyo wito huu hutumika kuwakumbusha waumini wa Kiislamu kwenda ibadani.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Lengo la adhana ni kuwajulisha watu kuwa muda wa ibada umefika na wakati mwingine hutumika kuwajulisha watu mahali nyumba ya ibada inapopatikana kwa wale wageni wa eneo husika.
Kitendo cha kutoa adhana huitwa kuadhini na mtu anayetoa adhana huitwa mwadhini.
Adhana hutolewa katika vipindi vya ibada yaani, alfajir, adhuhur, l-asr, magharib na l-ishaa.
Waislamu wote wanaitana hivyo katika sala zao:
- Allāhu Akbar (mara nne)
- Ašhadu an lā ilāh illā Allāh (mara mbili)
- Ašhadu anna Muḥammadan Rasūl Allāh (mara mbili)
- Ḥayya ʿalā al-salāt (mara mbili)
- Ḥayya ʿalā l-falāḥ (mara mbili)
- Allāhu Akbar (mara mbili)
- Lā ilāh illā Allāh (mara moja).
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |