Alfonso Rodríguez, S.J. (Segovia, 25 Julai 1532Palma de Majorca, 31 Oktoba 1617) alikuwa Mkristo wa Hispania aliyejiunga na Wajesuiti kama bradha,

Picha yake.
Njozi ya Alfonso Rodríguez, mchoro wa Francisco de Zurbarán.
Sanamu ya Alfonso Rodriguez.

Alitangazwa mwenye heri mwaka 1825, na mtakatifu tarehe 15 Januari 1888.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1]

Maisha hariri

Rodríguez alikuwa mtoto wa mfanyabiashara ya sufu. Mtakatifu Petro Faber, mmoja wa waanzilishi wa Shirika la Yesu, alipofika kuhubiri Segovia, familia ya Rodriguez ilimkaribisha. Faber alimuandaa kijana Alfonso kwa Komunyo ya Kwanza.[2]

Alipokuwa na umri wa miaka 14, baba alifariki, hivyo Alfonso aliacha shule amsaidie mama katika biashara.[3]

Alipofikia miaka 26 alimuoa María Suarez, aliyemzalia watoto watatu.

Alipofikia umri wa miaka 31 alibaki mjane mwenye mtoto mmoja tu aliyebaki.

Tangu hapo alishika maisha ya sala na toba, akijitenga na ulimwengu.

Alipofiwa mtoto aliyebaki, alianza kusikia wito wa utawa.[4]

Kwa ajili hiyo, akiwa na miaka 39 alijaribu kurudi masomoni, lakini hakufaulu, pia kwa sababu ya ugumu wa malipizi yake ulioharibu afya yake.

Hatimaye, tarehe 31 Januari 1571, akiwa na miaka 40, alipokewa na Wajesuiti.[4] Hoja ya mkuu aliyemkubali kinyume cha taratibu ilikuwa kwamba, kama Alfonso hafai kuwa bradha au padri, anaweza kuingia awe mtakatifu.[2]

Aliweka nadhiri za daima mwaka 1585 akiwa na miaka 54.

Kwa miaka 46 alifanya kwa namna bora kazi ya bawabu katika shule ya bweni ya Palma de Majorca, katika visiwa vya Baleari, akiwajenga wanafunzi na watu wote waliofika huko kwa mashauri yake mazuri ajabu. Mmojawao ni Petro Claver, aliyeelekezwa naye kwenda Amerika kama mmisionari.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Holweck, F. G., A Biographical Dictionary of the Saints. St. Louis, MO: B. Herder Book Co., 1924.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.