Antoni wa Mt. Ana Galvão, O.F.M., kwa Kireno Antônio de Sant'Anna, maarufu nchini Brazil kama Frei (Ndugu) Galvão (Guaratinguetá, 173923 Desemba 1822) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo wakati wa ukoloni.

Mchoro wa mwaka 1850.

Mmoja kati ya Wakristo wanaojulikana zaidi kati ya watu wa nchi yake, pia kutokana na miujiza iliyofanyika kwa njia yake,[1] Galvão alitangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 11 Mei 2007, akiwa wa kwanza kati ya wazawa wa Brazil.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake kila mwaka[3].

Maisha

hariri

Asili na utoto

hariri

Galvão alizaliwa Santo Antonio of Guaratinguetá, katika jimbo la São Paulo, akiwa wa nne kati ya watoto kumi wa familia yenye hadhi kubwa kijamii na pia kiimani.[1][4][5] Baba yake, Antônio Galvão de França, pamoja na kuwa kiongozi wa kijiji, alikuwa mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko na kujulikana kwa ukarimu wake.[4] Mama yake, Isabel Leite de Barros, alitokea kwa wakulima, lakini wajukuu wa mvumbuzi Fernão Dias Pais[4]

Alipofikia umri wa miaka 13, Galvão alitumwa kwenye seminari ya Wajesuiti Colégio de Belém[4][5] huko Cachoeira, Bahia akimfuata kaka yake, José.

Akiwa huko tangu mwaka 1752 hadi 1756, Galvão alipiga hatua kubwa katika masomo na katika maadili ya Ukristo. Alitamani kuwa padri Mjesuiti, lakini dhuluma dhidi ya shirika hilo iliyongozwa na Sebastião José de Carvalho e Melo, ilimfanya ajiunge na Wafransisko.[5] huko Taubaté, alivyomshauri baba yake.[1][4]

 
Sanamu ya Frei Galvão katika mji wa Guaratinguetá alipozaliwa.

Mfransisko

hariri

Akiwa na miaka 16, Galvão alijinyima maendeleo makubwa yaliyokuwa mbele yake, akawa mnovisi kwenye konventi ya Mt. Bonaventura huko Vila de Macacu, Rio de Janeiro.[4][5][6] akitwaa jina la kitawa Antoni wa Mt. Ana.[4]

Galvão aliweka nadhiri kuu tarehe 16 Aprili 1761, akijiongezea ile ya kutetea sifa ya Bikira Maria ya kuwa "Mkingiwa Dhambi ya Asili", ambayo ilikuwa bado ikijadiliwa wakati huo katika Kanisa Katoliki.[4]

Tarehe 11 Julai 1762, Galvão alipewa upadirisho na kuhamishiwa mjini São Paulo, alipoendelea kusoma teolojia na falsafa.[4]

Mwanzoni mwa mwaka 1766, Antoni alijitoa kuwa "mtumishi na mtumwa" wa Bikira Maria, akisaini hati hiyo kwa damu yake tarehe 9 Machi.[7]

Mwaka 1768 alifanywa mhubiri, muungamishi na bawabu wa konventi.[4][5]

Mwanzilishi

hariri

Tangu 1769 hadi 1770 Galvão akiwa muungamishi wa monasteri ya Mt. Teresa [4][5] alitambua wito wa Helena Maria wa Roho Mtakatifu wa kuanzisha monasteri mpya,[4][5][4] akamsaidia kuianzisha tarehe 2 Februari 1774 mjini huko[4][5] kwa kufuata kielelezo cha Wakonsesyoni,[4] ila nadhiri.[1][5] Helena alipofariki ghafla tarehe 23 Februari 1775, Galvão akawa mkubwa wa jumuia hiyo.[4] [5]

 
Frei Galvão katika kanisa kuu la Mt. Anthony huko Guaratinguetá.

Wakati huo mkuu mpya wa jimbo la São Paulo's aliagiza monasteri hiyo ifungwe.[4] Galvão alikubali, lakini masista walikataa kuhama. Hatimaye shinikizo la umati na juhudi za askofu wa São Paulo, monasteri ilifunguliwa tena[4] na kuendelea kupanuliwa ili kupokea miito mingi.[4][5] Galvão alitumia miaka 28 kujenga nyumba na kanisa lake, ambalo lilizinduliwa tarehe 15 Agosti 1802.[4] Katika juhudi zake za malezi kwa masista, aliwatungia pia Katiba maalumu.[4]

Mambo yalipoonekana kuwa yametulia, ilitokea shida nyingine kutoka kwa serikali[4] kwa sababu Antoni alifukuzwa kwa kupinga adhabu ya kifo iliyotolewa na mtawala kwa mtu aliyemtukana mwanae[4] Kwa mara nyingine, jamii ilidai uamuzi ufutwe.[4]

Mwaka 1781, Galvão alichaguliwa mlezi wa wanovisi huko Cachoeiras de Macacu,[4][5] lakini masista wake pamoja na askofu walifaulu kumrudisha kwa hoja ya kwamba "hakuna mkazi wa mji huu ambaye angeweza kuvumilia mtawa huyo asiwepo hata sekunde moja".[4]

Baadaye aliteuliwa mhudumu wa konventi mwaka 1798, tena mwaka 1801.[4][5]

Mwaka 1811 Galvão alianzisha konventi ya Mt. Klara huko Sorocaba.[4][5] Miezi 11 baadaye akarudi São Paulo.[4]

Uzeeni aliruhusiwa kuishi katika monasteri ya masista wake,[4] ambapo alifariki tarehe 23 Desemba 1822.[1][4] Galvão alizikwa katika kanisa lao, akiendelea kufikiwa na waamini wanaoomba sala zake.[4]

Maendeleo ya kazi yake

hariri

Mwaka 1929, monasteri hiyo iliungana na shirika la Wakonsesyoni.[4]

Jengo, ambalo sasa linaitwa "Monasteri ya Mwanga", limetangazwa na UNESCO kuwa urithi wa dunia[8] na kutumika kama Makumbusho ya Sanaa Takatifu ya São Paulo.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Profile: Saint Antonio Galvao". BBC News. May 11, 2007.
  2. "Pope names Brazil's first saint". BBC News. May 11, 2007.
  3. Martyrologium Romanum
  4. 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 4.12 4.13 4.14 4.15 4.16 4.17 4.18 4.19 4.20 4.21 4.22 4.23 4.24 4.25 4.26 4.27 4.28 4.29 4.30 4.31 4.32 "Fr. Anthony of Saint Anne Galvão (1739 - 1822) - Biography". Vatican.va.
  5. 5.00 5.01 5.02 5.03 5.04 5.05 5.06 5.07 5.08 5.09 5.10 5.11 5.12 5.13 Frei Galvão Archived 10 Aprili 2010 at the Wayback Machine. at Patron Saints Index.
  6. This is the age given by the website maintained by his descendents, which would be in keeping with the standard practice of the Order [1]
  7. Official website
  8. Pomi, Ana Maria (Deutsche Presse-Agentur). "Profile: Brazil's soon-to-be saint performed paper-pill miracles" Archived 2013-01-29 at Archive.today. Monstersandcritics.com. May 9, 2007.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.