Mbwa-kaya

Mnyama anayeishi na watu; kazi yake hasa ni kulinda nyumbani
(Elekezwa kutoka Canis lupus familiaris)
Mbwa

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Jenasi: Canis (Mbwa)
Linnaeus, 1758
Spishi: C. lupus
Linnaeus, 1758
Nususpishi: C. l. familiaris
(Linnaeus]], 1758)

Mbwa (Canis lupus familiaris) ni mnyama anayefugwa na binadamu tangu muda mrefu. Kibiolojia anahesabiwa kati ya mamalia wala nyama.

Utangulizi hariri

Mbwa-kaya ni jamii ya mbwa mwitu wanaohusishwa na binadamu. Mbwa wamekuwa pamoja na binadamu kwa muda mrefu, wakisaidia kazi mbalimbali na kuwa kampani ya binadamu.

Mbwa wamekuwa na thamani kubwa sana kwa binadamu wa kale walisaidia ulinzi, uwindaji, kuchunga mifugo, kusaidia polisi na wanajeshi, mpaka kuwasaidia watu wenye ulemavu. Tabia hizi zinawafanya kuonekana ndio wanyama rafiki wa binadamu kuliko wengine wote. Mpaka sasa inakadiriwa kuna mbwa milioni 400 duniani kote.

Watu na mbwa hariri

Watu wametumia mbwa kulingana na utamaduni wao kwa njia mbalimbali kama mnyama wa kazi akilinda nyumba na mifugo au kubeba mzigo.

  • Waeskimo wa Aktiki wanatumia mbwa kwa usafiri wakivuta sleji yaani vitoroli vinavyoteleza juu ya barafu.
  • Watu wa China Kusini, Korea na Vietnam wanakula nyama ya mbwa. Inakadiriwa kuwa mbwa kati ya milioni 13-16 huliwa kila mwaka katika bara la Asia.
  • Mara nyingi mbwa wanafugwa nyumbani kama wanyama wa kusindikiza watu tu wakitazamiwa kama marafiki.
  • Kinyume chake katika utamaduni mwingine mbwa anaangaliwa kama najisi.

Mbwa wametumiwa kwa kazi nyingi:

  • Wanalinda nyumba za watu.
  • Wanaangalia na kulinda mifugo kwa mfano kondoo
  • Wanaongoza watu vipofu,
  • wanasaidi polisi,
  • wanatafuta madawa ya kulevya au mabomu yaliyofichwa.
  • Kiumbe cha kwanza kilichotoka duniani alikuwa mbwa jike Laika aliyerushwa angani tar. 3 Novemba 1957 kwa chombo cha angani cha kirusi Sputnik 2 akafa huko siku ileile.

Tabia hariri

Kutokana na historia ndefu ya kufugwa na uteuzi wa kibinadamu kuna aina nyingi za mbwa wanaoonyesha miili tofautitofauti, hata hivyo mbwa wote ni spishi moja tu na wote wanaweza kuzaliana.

Mbwa huwa na uwezo mzuri wa kusikia na kunusa lakini hawaoni vizuri sana hasa rangi. Wanaweza kusikia sauti kwa umbali wa kilomita kadhaa.

Mbwa wengi hufikia umri wa kati ya miaka 10 na 13.[1]

Kiasili mbwa waliishi katika makundi yenye ufuatano wa vyeo. Mbwa mkuu huitwa "dume alfa". Mbwa wakiishi pamoja na binadamu wanawakubali kama mbwa wenye cheo cha juu.

Utafiti unaonyesha kuwa, kutokana na kuishi na binadamu wa muda mrefu, mbwa wana uelewa wa pekee wa tabia za binadamu.[2] Mbwa-kaya wanaweza kuishi kwa kula chakula cha wanga tu, wakati aina nyingine za mbwa haziwezi.

Mwili hariri

Mbwa wamekuwa wakikuzwa kwa makusudi mbalimbali duniani, kutokana na uwezo wao wa hisia na kutumia maungo yao. Mbwa hutofautiana sana kwa vizazi vyao, hasa katika muonekano, ukubwa, uzito na tabia kuliko wanyama wengine wowote. Hata hivyo maungo yao yanasimama kwa ajili yao, mbwa mwitu wa kafiawia. Mbwa hula nyama kwa kuwinda, na mabaki, na kama ilivyo kwa wanyama wengi wala nyama (wawindaji), mbwa wana misuli yenye nguvu, mifupa inayomruhusu kuruka na uvumilivu pamoja na meno kwa ajili ya kukamata na kurarua.

Kuona hariri

Kama ilivyo kwa wanyama wengi, mbwa huwa hawaoni rangi zote kama binadamu, na badala yake kwa buluu na nyekundu tu. Uoni wa mbwa umeimarika kutokana na shughuli zake za uwindaji. Hata hivyo mbwa wameonekana mahiri zaidi katika utambuzi wa vitu vilivyo katika mwendo, hasa pale wanapowatambua wamiliki wao, hata wakiwa kilometa moja kutoka kwa mbwa.

Kusikia hariri

Uwezo wa kusikia wa mbwa ni zaidi ya ule wa binadamu, hivyo mbwa huweza kusikia hata sauti ndogo kabisa ambazo binadamu hawezi kuzisikia. Wana uwezo mkubwa sana wa kujua hata sehemu ilipotokea sauti Wana misuli kumi na nane inayoweza kugeuza, kuinua, kushusha na kuzungusha masikio.

Chakula hariri

Pamoja na kuwa na asili ya mbwa mwitu ambao ni wala nyama, chakula cha mbwa ni cha aina mbalimbali na sio nyama pekee. Licha ya nyama mbwa hula mboga na nafaka. Kiafya haishauriwi kuwapa mbwa chakula cha nyama peke yake kutokana na ukosefu wa madini ya chuma na kalsiamu. Ukilinganisha na mbwa mwitu, mbwa-kaya wana uwezo mkubwa wa kula vyakula vya wanga.

Dini na tamaduni hariri

Kwenye dini na utamaduni wa Kiyahudi mbwa hutunzwa kama wanyama wengine wanaoishi na binadamu. Sheria ya Kiyahudi inahitaji Wayahudi kulisha mbwa (na wanyama wengine) kabla yao wenyewe, na kupanga jinsi ya kuwalisha kabla ya kuanza kuishi nao.

Katika Ukristo, mbwa huonekana kama alama ya uaminifu.

Katika dini ya Uislamu, mbwa huonekana kama najisi.

Huko Uchina, Korea na Japani, mbwa huchukuliwa kuwa walinzi.

Filamu hariri

Filamu mbalimbali zimetolewa kuhusu mbwa. Mojawapo ni The Fox and the Hound (kwa KiswahiliMbweha na Mbwa), filamu ya katuni iliyotolewa mwaka wa 1981.

Picha hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbwa-kaya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.