Effat Nagy

Msanii kutoka Misri


Effat Nagy (Nagi, Effat Naghi, au Effat Nagui; 5 Aprili 1905 - 4 Oktoba 1994) alikuwa msanii wa Misri ambaye ana jumba la makumbushohuko Cairo aliyejitolea yeye na kazi za mumewe. Jumba hilo linaitwa jumba la kumbukumbu la Saad El-Khadem na Effat Nagy.

Effat nagy
Amezaliwa 5 appril 1905
Bandari
Amekufa 1994
Nchi Misiri
Majina mengine Effat Nagui
Kazi yake Msanii

Maisha

hariri

Effat Mousa Nagy alizaliwa katika bandari ya Mediteranea ya Alexandria mnamo mwaka 1905. Alivutiwa na utamaduni na alifundishwa muziki na hisabati.[1] Alifundishwa sanaa na mkufunzi wa kibinafsi na kaka yake Mohamed Nagy. Mafunzo yake rasmi yalikuwa katika chuo cha sanaa huko Roma mnamo mwaka 1947.[2] Alifanya kazi huko Misri chini ya André Lhote na walitumia akiolojia ya Misri kama mada.[3]

Aliolewa na Saad Al-Khadem mnamo 1945.[4]Alikuwa msanii lakini pia mtafiti. Utafiti wa mumewe uliongoza sanaa yake.

Mnamo 1956 alipokea pongezi kutoka kwa kaka yake. Alisema kuwa kazi yake ilizidi yake kwani alihisi kuwa kazi yake ilizuiliwa sana na mafunzo yake ya masomo.[3]

Mnamo 1964 alionyesha kazi yake katika maonyesho ya High Dam (kama-Sad al-'Aali).[1]Hii ilikuwa matokeo ya kazi ambayo alikuwa ameagizwa kufanya mwaka uliopita. Aliombwa kurekodi akiolojia ambayo ingeweza kupotea kwani ilikuwa imezamishwa chini ya maji ya bwawa la Aswan ilipojengwa. Alikuwa mmoja wa wasanii 64 waliochaguliwa kufanya kazi hii.[2]

Mnamo 1968 jumba la kumbukumbu la Mohamed Nagy lilianzishwa na Nagy alitoa mchango wa picha arobaini za kaka yake kusaidia kuunda mkusanyiko wa kazi za kaka yake.

Nagy alifariki mnamo mwaka 1994[1] ingawa chanzo kingine kinasema 1997.

Maonyesho ya solo yaliyochaguliwa

hariri

Urithi

hariri

Nagy na mumewe wana jumba la makumbusho huko Cairo ambalo lina picha zao 200 na ufinyanzi.[4]Jumba la kumbukumbu la Saad El-Khadem na Effat Nagy lina picha 24 za Nagy na 34 na mumewe pamoja na picha ya uchi kubwa ambapo Nagy ndiye mfano.[3]Jengo hilo pia lina maktaba yao ya zamani[2] ambayo ina vitabu vingi muhimu juu ya ngano na unajimu. Nagy aliiachia serikali ya Misri nyumba yake, lakini ni serikali ya Ufaransa iliyolipa wasifu wake uchapishwe.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Effat Mousa Nagy Ilihifadhiwa 7 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine., CV, FineArt.gov.uk, Retrieved 16 September 2015
  2. 2.0 2.1 2.2 Pioneers: Saad El-Khadem and Effat Nagy Museum: Recharge your inspiration, 2011, Daily News Egypt, Retrieved 16 September 2015
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Pioneers: Saad El-Khadem and Effat Nagy Museum, Youmna Salah, 1 January 2011, Masress.com, Retrieved 17 September 2015
  4. 4.0 4.1 Effat Nagy and Saad al-Khadem Museum Archived 2016-03-04 at the Wayback Machine, Cairo.gov.eg, Retrieved 16 September 2015
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Effat Nagy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.