Kalenda ya Kiyahudi
Kalenda ya Kiyahudi (pia: Kalenda ya Kiebrania) ni kalenda inayotumiwa katika dini ya Uyahudi na pia nchini Israel. Inatumiwa kupanga tarehe za sikukuu za Kiyahudi na utaratibu wa kusoma Torati kwa kila wiki.
Mwaka
haririKalenda hiyo inajua miaka tofauti ndani ya kipindi kilekile.
Kanuni za msingi
haririKalenda ya Kiebrania ni kalenda jua-mwezi.
- Miezi ya kalenda hiyo hufuata mwonekano halisi wa Mwezi angani, sawa na kalenda ya Kiislamu. Mwezi mpya unaanza wakati wa kuonekana kwa hilali.
- Wakati huo huo, Pasaka ya Kiyahudi inapaswa kutokea kwenye majira ya machipuo, wakati wa mwezi Aprili au mwisho wa Machi. Ilhali majira ya machipuo hufuata mwendo wa Jua, kanuni hii inafunga makadirio ya mwaka na mwendo wa Jua.
- Hii inasababisha ulazima wa kupatanisha tofauti kati ya muda wa mwaka wa Jua (siku 365) na muda wa mwaka wa Mwezi (takriban siku 354).
- Hapo kalenda ya Kiebrania inaongeza mwezi wa nyongeza mara saba katika kila kipindi cha miaka 19. Kwa hiyo kuna miaka ya kawaida yenye siku 354 na miezi 12. Lakini kila mwaka wa pili au wa tatu ni mwaka mrefu wenye miezi 13 na siku 384.
Juma
haririNje ya kalenda hiyo kuna utaratibu wa wiki ya siku saba zinazoendelea mfululizo, sawa na kalenda ya kimataifa. Hutumiwa kubaini siku ya Shabbat, ambayo ni siku ya kupumzika. Wiki haitegemei mwaka wa jua wala wa mwezi. Badala yake, inategemea hesabu ya siku saba ambazo zinaaminika kurudi nyakati za zamani za Babeli na kutajwa katika masimulizi ya kuumbwa kwa Dunia katika Biblia.
Siku za juma la Kiyahudi
haririSiku ya juma (Kiebrania) |
Tafsiri | Siku inaanza kutoka kuzama kwa Jua | Siku inaendelea mpaka kuzama kwa jua |
---|---|---|---|
יום ראשון yom rishon |
siku ya kwanza | Jumamosi | Jumapili |
יום שני yom sheni |
siku ya pili | Jumapili | Jumatatu |
יום שלישי yom shelishi |
siku ya tatu | Jumatatu | Jumanne |
יום רביעי yom revi'i |
siku ya nne | Jumanne | Jumatano |
יום חמישי yom hamishi |
siku ya tano | Jumatano | Alhamisi |
יום ששי yom shishi |
siku ya sita | Alhamisi | Ijumaa |
שבת shabbat |
Shabbat (Sabato) |
Ijumaa | Jumamosi |
Miezi
haririMwezi namba katika Biblia |
Jina la mwezi | Jina la mwezi kwa Kiebrania |
Idadi ya siku |
Wakati wa mwaka | Maelezo |
---|---|---|---|---|---|
1 | Nisan | נִיסָן | 30 | Machi - Aprili | Mwezi wa Pasaka |
2 | Iyar | אִייָר | 29 | Aprili- Mei | |
3 | Sivan | סִיוָן | 30 | Mei- Juni | Mwezi wa Shavuot |
4 | Tammuz | תַּמּוּז | 29 | Juni- Julai | |
5 | Av | אָב | 30 | Julai- Agosti | Mwezi wa Tisha B'Av |
6 | Elul | אֱלוּל | 29 | Agosti- Septemba | |
7 | Tishri | תִּשְׁרֵי | 30 | Septemba- Oktoba | Mwezi wa Rosh Hashanah, Yom Kippur na Sukkot |
8 | Heshvan (au Marheshvan) |
(מַרְ)חֶשְׁוָן | 29 au 30 [1] | Oktoba - Novemba | |
9 | Kislev | כִּסְלֵו | 30 au 29 | Novemba - Desemba | Mwezi wa Hanukka |
10 | Tevet | כִּסְלֵו | 29 | Desemba- Januari | |
11 | Shevat | שְׁבָט | 30 | Januari- Februari | |
12 | Adar | אֲדָר | 29 | Februari-Machi | Katika mwaka mrefu, mwezi wa 13 unaongezwa unaoitwa pia Adar, lakini inapewa namba; kwa hiyo katika mwaka mrefu kuna Adar I na Adar II |
Siku na wiki
haririKatika kalenda ya Kiyahudi, siku inafafanuliwa kufuatana na Biblia ya Kiebrania: [2] "Na ilikuwa jioni, na ilikuwa asubuhi, siku moja". Kwa sababu "jioni" inakuja kabla ya "asubuhi", siku katika kalenda ya Kiyahudi huanza jioni baada ya machweo . Ni muhimu kuhakikisha kuwa siku iliyopita imekwisha kabisa, hivyo siku mpya huanza wakati wa usiku umeanza. [3]
Katika kalenda zinazochapishwa, tofauti hii haionekani maana hapa tarehe za kalenda ya Kiyahudi na tarehe za Kalenda ya Gregori zinazoanza usiku wa manane huonyeshwa kandokando. Ineleweka kuwa watu wanaotumia kalenda hizi wanajua utaratibu wa kuanza siku baada ya machweo. Wakati wowote sikukuu, siku ya kuzaliwa au ya kumbukumbu ikionekana kwenye kalenda iliyochapishwa, kwa kweli huanza jioni iliyotangulia, baada ya machweo.
Molad
haririHesabu ya kalenda ya Kiebrania mwaka na mwezi huanza na molad inayomaanisha hilali. Molad ni neno la Kiebrania linalomaanisha "kuzaliwa". Neno hilo linamaanisha "kuzaliwa" kwa mwezi mpya kila mwezi. Kalenda ya kisasa ya Kiebrania hutumia molad iliyohesabiwa: urefu wa wastani wa muda kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya. Urefu wa Molad ni siku 29, masaa 12, dakika 44, sekunde 3 na nusu. [4]
Tanbihi
hariri- ↑ Idadi inaweza kubadilika katika miaka kadhaa
- ↑ Genesis 1:5
- ↑ "The Jewish Day". Chabad.org. Iliwekwa mnamo 11 Mei 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bromberg, Dr. Irving. "Moon and the Molad of the Hebrew Calendar". Iliwekwa mnamo 19 Mei 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
hariri- Msimbo wa Maimonides (Mishneh Torah), Kitabu cha Tatu, Tolea Nane: Utakaso wa Mwezi Mpya . Ilitafsiriwa na Solomon Gandz. Yale Judaica Series Vol XI, Press University University of Yale, New Haven, Conn., 1956.
- Bonnie Blackburn na Leofranc Holford-Strevens. Mpenzi wa Oxford kwa Mwaka: Uchunguzi wa Forodha ya Kalenda na Uhesabuji wa wakati . Vyombo vya Habari vya Chuo Kikuu cha Oxford; USA, 2000. pp 723-730.
Tovuti nyingine
hariri- Kalenda ya Kiyahudi inaelezea maoni mbali mbali ya Kiyahudi kuhusu historia ya kalenda ya Kiyahudi / kalenda ya Kiebrania. Ni pamoja na chati kadhaa.
- Kalenda ya Kiyahudi na Zmanim - nyakati za Halachic na kibadilishaji cha tarehe chabad.org
- Historia ya Wayahudi: Kalenda
- Kalenda ya Kiyahudi Maelezo ya Archived 18 Juni 2020 at the Wayback Machine. kina zaidi, ya kisayansi katika wavuti ya NASA
- Kalenda ya Kiebrania kwa tovuti ya Wakristo