Margareta wa Hungaria
Margareta wa Hungaria, O.P. (Ngome Klis, Korasya, 27 Januari 1242 - Budapest 18 Januari 1271) alikuwa binti wa mwisho wa mfalme Bela IV wa Hungaria, kaka wa Elizabeti wa Hungaria.
Kama shangazi yao huyo, yeye na dada yake Kinga pia wanaheshimiwa kama mtakatifu, mbali ya dada mwingine, Yolanda, anayeheshimiwa kama mwenye heri.
Utakatifu wake ulikubaliwa tangu zamani ukatangazwa rasmi na Papa Pius XII tarehe 19 Novemba 1943.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka katika tarehe ya kifo chake, 18 Januari[1].
Maisha
haririMargareta alizaliwa uhamishoni kwa sababu Wamongolia walikuwa wameteka Hungaria. Basi, wazazi wake walitoa nadhiri kwa Mungu kwamba hao wavamizi wakiondoka, wao watamtolea binti yao utawani.
Kweli Wamongolia walifukuzwa mwaka uleule, na baada ya miaka michache Margareta alikabidhiwa kwa masista Wadominiko kwa malezi.
Mwaka 1254, akiwa na umri wa miaka 12 tu, aliweka nadhiri za kitawa na mwaka 1261 alivaa shela akitamani kuungana na Yesu msulubiwa.
Hakupata elimu sana, lakini alipenda kusomewa Biblia akasali sana, akiheshimu hasa mateso ya Yesu na ekaristi.
Alishika sana ufukara na maisha ya malipizi akajaliwa njozi mbalimbali.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- "Bl. Margaret of Hungary". Catholic Encyclopedia. 1913. http://www.newadvent.org/cathen/09654a.htm.
- English article on the homepage of the Catholic Church in Hungary Archived 5 Machi 2008 at the Wayback Machine.
- St. Vincent Ferrer Parish Archived 12 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Catholic Exchange Archived 29 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |