Methodio
Methodio wa Thesalonike (kwa Kigiriki: Μεθόδιος - Methodios; kwa Kislavoni: Мефодии; Thesalonike, Ugiriki, mnamo 826 - Velehrad, Moravia, leo nchini Ucheki, 6 Aprili 885) alikuwa mmisionari wa Waslavoni wa Ulaya ya kusini-mashariki katika karne ya 9 BK akishirikiana na kaka yake Sirili.
Methodio | |
---|---|
Ndugu Sirili na Methodi mitume wa Waslavoni. | |
Amezaliwa | 826 |
Feast |
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na kaka yake.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifo cha kaka yake, 14 Februari[1].
Maisha
haririAlizaliwa kwa jina la "Mikaeli" mjini Thesalonike au Saloniki katika Ugiriki ya kaskazini wakati wa enzi za Dola la Bizanti kama mtoto wa Leontios askari wa Kibizanti na Maria mke wake Mslavoni.
Methodio alijiunga na wamonaki akawa msimamizi wa monasteri.
Mnamo mwaka 861 Rastislav mtawala wa Moravia alitafuta njia ya kuimarisha utawala wake kwa kupunguza athira ya majirani wake Wafrankoni wa Mashariki (au Wajerumani jinsi walivyoitwa baadaye). Wajerumani waliwahi kuleta imani ya Kikristo Moravia. Ratislav alitaka kuwa na maaskofu na mapadri wasio Wajerumani. Hivyo alimwomba Kaisari wa Bizanti kutuma wamisionari kwake kutoka huko.
Kaisari Michael III Konstantino wa Konstantinopoli alituma ndugu Kyrilo na Methodio kwa sababu wote wawili walikuwa watu wa Kanisa wenye elimu nzuri wakijua lugha ya Kislavoni tangu utoto wao.
Baadaya ya kifo cha Kyrilo, Methodio aliendelea akiwa amefanywa na Papa Adriani II kuwa askofu wa Srijem (leo nchini Kroatia) na mwalimu wa Kikristo mwenye athira kubwa kati ya Waslavoni. Tangu mwaka 883 alitafsiri Biblia katika lugha ya Kisalvoni na kuweka misingi ya liturgia ya Kislavoni.
Anasifiwa kama mmisionari aliyefaulu kuunganisha ujumbe wa Ukristo na utamaduni wa Waslavoni, akifanya kazi bila kujibakiza na kwa kuvumilia vipingamizi vingi, akitegemezwa daima na Mapapa wa Roma.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- The Life and Miracles of Saints Cyril and Methodius, Bishops and Apostles of the Christian Church Archived 3 Septemba 2014 at the Wayback Machine.
- Slavorum Apostoli by Pope John Paul II
- Waraka wa Papa Yohane Paulo II
- Cyril and Methodius – Encyclical letter (Epistola Enciclica), 31 December 1980 Waraka wa Papa Yohane Paulo II]
- "Cyril and Methodius, Saints" article in Encyclopædia Britannica.
- "Sts. Cyril and Methodius". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- "Equal to Apostles SS. Cyril and Methodius Teachers of Slavs", by Prof. Nicolai D. Talberg
- Catholic Culture
- Cyril and Methodius at orthodoxwiki
- Bulgarian Official Holidays, National Assembly of the Republic of Bulgaria: in English Archived 9 Juni 2008 at the Wayback Machine., in Bulgarian Archived 28 Novemba 2010 at the Wayback Machine.
- Bank holidays in the Czech Republic, Czech National Bank: in English Archived 31 Oktoba 2007 at the Wayback Machine., in Czech Archived 3 Novemba 2010 at the Wayback Machine.
- 24 May – The Day Of Slavonic Alphabet, Bulgarian Enlightenment and Culture
- Cyril Archived 2 Februari 2011 at the Wayback Machine. at Patron Saints Index Archived 25 Juni 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |