Mkoa wa Langenburg (DOA)

(Elekezwa kutoka Mkoa wa Langenburg)

Mkoa wa Langenburg ulikuwa mkoa mmojawapo kati ya mikoa 21 ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (DOA, Deutsch Ostafrika) lililokuwa mtangulizi wa nchi za Tanzania bara, Rwanda na Burundi za leo.

Ramani ya Mkoa wa Langenburg (XI) katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani; namba za Kirumi hudokeza mikoa jirani: X Ssongea (Songea), XX Iringa, XII Bismarckburg (Kasanga (Ufipa))

Mkoa huo ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 28,900. Eneo lake lililingana na sehemu za kusini za Mikoa ya Mbeya na Songwe, takriban na wilaya za leo za Rungwe, Kyela, Ileje, Makete, Mbozi, Songwe na Mbeya Mjini na Vijijini.

Makao makuu (jer. Bezirksamt) yalikuwepo kiasili pale Alt-Langenburg (leo Lumbila) kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa. Kutokana na mabadiliko kwenye uwiano wa maji ya ziwa na mafuriko kituo kipya kilianzishwa kilomita yalikuwepo mjini Neu-Langenburg (leo: Tukuyu). Ofisi ndogo za mkoa (jer. Bezirksnebenstelle) zilikuwepo Makete na hadi mwaka 1910 pia Wiedhafen (Manda (Ludewa). Baadaye eneo la Wiedhafen yaani ufuko wa mashariki wa Ziwa Nyasa hadi mpaka wa Afrika ya Mashariki ya Kireno (Msumbiji) lilihamishwa kwenda Mkoa wa Ssongea (Songea).

Mkoa huu (XI kwenye ramani) ulipakana na

Mwaka 1913 kulikuwa na wakazi Waafrika 195,800 pamoja na Wazungu 137 na Wahindi au Waarabu 32.

Takwimu ya Wajerumani ilihesabu walowezi Wazungu 9 waliolima pamba, miti ya mpira na kahawa au kufuga kwenye km2 29 jumla ya ng'ombe 2892, kondoo au mbuzi 412, nguruwe 279 na punda 287. Kwa jumla km² 34.2 zilitawaliwa na Wazungu.

Wenyeji Waafrika walikuwa na ng'ombe 102,880, kondoo 21,400 na mbuzi 29,800.

Kabla ya mwaka 1914 zilikuwepo kampuni za biashara ya Kizungu 2.

Marejeo

hariri