Methodio

(Elekezwa kutoka Mt. Methodio)

Methodio wa Thesalonike (kwa Kigiriki: Μεθόδιος - Methodios; kwa Kislavoni: Мефодии; Thesalonike, Ugiriki, mnamo 826 - Velehrad, Moravia, leo nchini Ucheki, 6 Aprili 885) alikuwa mmisionari wa Waslavoni wa Ulaya ya kusini-mashariki katika karne ya 9 BK akishirikiana na kaka yake Sirili.

Methodio

Ndugu Sirili na Methodi mitume wa Waslavoni.
Amezaliwa 826
Feast

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na kaka yake.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifo cha kaka yake, 14 Februari[1].

Maisha

hariri

Alizaliwa kwa jina la "Mikaeli" mjini Thesalonike au Saloniki katika Ugiriki ya kaskazini wakati wa enzi za Dola la Bizanti kama mtoto wa Leontios askari wa Kibizanti na Maria mke wake Mslavoni.

Methodio alijiunga na wamonaki akawa msimamizi wa monasteri.

Mnamo mwaka 861 Rastislav mtawala wa Moravia alitafuta njia ya kuimarisha utawala wake kwa kupunguza athira ya majirani wake Wafrankoni wa Mashariki (au Wajerumani jinsi walivyoitwa baadaye). Wajerumani waliwahi kuleta imani ya Kikristo Moravia. Ratislav alitaka kuwa na maaskofu na mapadri wasio Wajerumani. Hivyo alimwomba Kaisari wa Bizanti kutuma wamisionari kwake kutoka huko.

Kaisari Michael III Konstantino wa Konstantinopoli alituma ndugu Sirili na Methodio kwa sababu wote wawili walikuwa watu wa Kanisa wenye elimu nzuri wakijua lugha ya Kislavoni tangu utoto wao.

Baadaya ya kifo cha Sirili, Methodio aliendelea akiwa amefanywa na Papa Adriani II kuwa askofu wa Srijem (leo nchini Kroatia) na mwalimu wa Kikristo mwenye athira kubwa kati ya Waslavoni. Tangu mwaka 883 alitafsiri Biblia katika lugha ya Kisalvoni na kuweka misingi ya liturgia ya Kislavoni.

Anasifiwa kama mmisionari aliyefaulu kuunganisha ujumbe wa Ukristo na utamaduni wa Waslavoni, akifanya kazi bila kujibakiza na kwa kuvumilia vipingamizi vingi, akitegemezwa daima na Mapapa wa Roma.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.