Petro Regalado (kwa Kihispania San Pedro Regalado) (Valladolid, Hispania, 1390La Aguilera, 30 Machi 1456) alikuwa mtawa na padri aliyechangia urekebisho wa shirika lake la Kifransisko.

Sanamu yake huko Valladolid, alipozaliwa.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Inosenti XI tarehe 11 Machi 1684, halafu mtakatifu na Papa Benedikto XIV tarehe 29 Juni 1746.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifo chake[1] au 13 Mei, ambapo maiti yake ilifukuliwa miaka 36 baada ya kifo chake ikaonekana haijaoza, ikazikwa mahali pa heshima zaidi.

Maisha hariri

Familia yake ilikuwa tajiri na adilifu. Kisha kufiwa baba, alilelewa na mama tu.

Alipofikia umri wa miaka 10 aliomba kujiunga na Ndugu Wadogo Wakonventuali, akakubaliwa miaka 3 baadaye.

Mwaka 1404 akawa mmojawapo kati ya wafuasi wa kwanza wa Pedro de Villacreces, aliyeanzisha urekebisho wa Observansya nchini Hispania mwaka 1397.

Katika konventi mpya ya La Aguilera, Petro alikuta maisha ya upweke, sala na ufukara mkuu aliyoyatamani, akayaeneza kwa nguvu zote.

Mtu mnyenyekevu sana na mwenye nidhamu kamili ya toba, mwaka 1415 akawa mhudumu wa konventi hiyo.

Mwaka 1422, kutokana na kifo cha Villacreces, Petro akawa kiongozi wa urekebisho hadi kifo chake.

Alijenga vyumba viwili ambamo waishi wakaapweke wasiozidi kumi na wawili.

Sifa zake za utakatifu zikazidi kuvuma, pia kutokana na miujiza mingi iliyosemekana kutokea.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  • Marcelo González, San Pedro Regalado, en Año Cristiano, Tomo I, Madrid, Ed. Católica (BAC 182), 1959, pp. 710-716.
  • Luis Carrión González, Historia documentada de convento DOMUS DEI de La Aguilera. Madrid 1930.
  • Daniel Elcid, El Santo Regalado. La Aguilera 1997.
  • José Miguel López Cuétara, San Pedro Regalado, fraile franciscano, el Santo de La Aguilera. Diario de Burgos, 1991 - San Pedro Regalado, un vallisoletano desconocido. El Norte de Castilla, 1994 - Seiscientos años de la fundación del Convento Domus Dei de La Aguilera. Diario de Burgos, 2004.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. Martyrologium Romanum