Ra
Nakala hii inahusu mungu Ra au Re wa Misri ya Kale . Kwa elementi ya kikemia yenye kifupi "Ra", angalia Radi.
Ra (pia: Re) alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Aliabudiwa hasa kama mungu wa Jua.
Wamisri waliona alizaliwa kila asubuhi upande wa mashariki, na kufariki kila usiku upande wa magharibi. Usiku alisafiri kupitia kuzimu. Hii ndiyo sababu upande wa magharibi wa Nile ulijulikana kama "nchi ya wafu".
Alichorwa na kichwa cha ndege wa kozi. Alitazamwa kama mkuu au mfalme wa miungu.
Jina
haririRa aliabudiwa kuwa mungu wa Jua na uumbaji. Alikuwa mungu muhimu sana katika Misri ya Kale akiwa na majina mengi, kama Amun-Ra, na Ra-Horakhti. Alifanana katika mengi na imani katika mungu Horus kwa hiyo kulikuwa na kipindi ambako miungu hiyo miwili iliabudiwa pamoja kama Ra-Horakhti ("Ra aliye Horus wa upeo mbili"). Wakati wa Ufalme Mpya, wakati mungu Amun alipendwa sana, aliunganishwa na Ra kuwa Amun-Ra.
Muonekano
haririRa alionyeshwa kwa maumbo mbalimbali wakati sanamu zake zilichongwa au picha yake zilichorwa. Umbo lililoonyeshwa mara nyingi ni lile la mtu aliye na kichwa cha kozi na jua juu yake. Aliweza kuonyeshwa pia kama mbawakawa aina ya bungo-mavi (scarab beetle). Katika umbo la Amun-Ra alionyeshwa kama mtu mwenye kichwa cha kondoo dume.
Ibada
haririIbada ya Ra ilianza kukua kutoka wakati wa nasaba ya II, ambako Ra alianza kuabudiwa kama mungu wa Jua. Kuanzia nasaba ya IV, mafarao waliitwa "Wana wa Ra". Ibada yake iliongezeka sana katika nasaba ya V, wakati alikuwa mungu wa serikali. Mafarao walijenga piramidi, nguzo na mahekalu kwa heshima yake.
Mamlaka
haririRa aliaminika kuwa mungu mkuu wa Misri aliyekuwa na mamlaka kushinda miungu mingine. Hivyo aliabudiwa kama muumbaji aliye asili ya Dunia, mbingu na watu.
Familia
haririBinti wa Ra na Nut (mjukuu wake) aliitwa Hathor, mungu wa kike wa upendo. Ra alikuwa na watoto wawili: Shu, mungu wa hewa na Tefnut, mungu wa kike wa umande wa asubuhi. Hao walikuwa na watoto wawili walioitwa Nut, mungu wa kike wa mbingu na Geb, mungu wa dunia. Tena hao walikuwa na watoto wanne walioitwa Isis, mungu wa kike wa nyumbani, Nephthys, mungu wa maombolezo, Set, mungu wa jangwa, na Osiris, mungu wa kuzimu. Wakaungana na kuwa na watoto wengine wawili, Anubis, mungu wa dawa ya kupaka dawa, na Horus, mungu wa anga.
Marejeo
hariri- Remler, Pat, Mythology ya Misri kutoka AZ 180-181
- Watterson, Barbara, Miungu ya Misri ya kale
- Wilkinson, Richard, Miungu kamili na Miungu wa kike wa Misri ya Kale
- John, Banes na Jaromir, Malek, Atlas ya Utamaduni ya Ulimwengu: Misri ya Kale 173
Tovuti za Nje
hariri- http://www.fruitofthenile.com/Ra.htm Ilihifadhiwa 6 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.
- http://www.egyptartsite.com/Ra.html
- http://ancient-egypt-online.com/egypt-god-amon-re.html Ilihifadhiwa 26 Februari 2015 kwenye Wayback Machine.
- http://www.ancient-mythology.com./egyptian/ra.php
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |