Yosefu wa Leonesa, O.F.M. Cap., (jina la kitawa kwa Kiitalia Giuseppe da Leonessa, jina la awali Eufranio Desiderio) aliishi zaidi nchini Italia (8 Januari 15564 Februari 1612) na anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Mt. Fidelis wa Sigmaringen na Mt. Yosefu wa Leonesa walivyochorwa na Tiepolo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha

hariri

Alizaliwa Leonessa, mji mdogo wa Italia ya Kati, na alionyesha mapema mwelekeo mkubwa kwa mambo ya dini, hata kujipiga mijeledi siku ya Ijumaa ili kushiriki mateso ya Yesu.

Kinyume cha matarajio ya mlezi wake aliyetaka aoe, alipofikia umri wa miaka 16 alijiunga na urekebisho wa Ndugu Wadogo ulioitwa wa Wakapuchini akawa mnovisi huko Carcerelle karibu na Assisi.

Kama mtawa alishika sana matendo ya toba na kujinyima.

Alipata upadrisho tarehe 24 Septemba 1580.

Mwaka 1587 Mtumishi mkuu wa shirika lake alimtuma Konstantinopoli ili kuhudumia Wakristo waliotekwa na Waislamu akatumikishwa huko. Ufukara wake na wa wenzake ulivuta Waturuki wengi waende kuwaona, naye alikuwa akihubiri mjini kila siku hadi alipokamatwa na kufungwa mpaka alipoachiliwa kwa juhudi za watu wa Venezia.

Alifikia hatua ya kujaribu kuhubiri Injili katika ikulu la sultani Murad III, lakini alikamatwa tena na kuhukumiwa adhabu ya kifo. Kwa siku tatu aling'ing'inia msalabani hadi (inavyosemekana) alipofunguliwa na malaika na kurudishwa Italia.

Hapo akaanza kazi ya kuhubiri katika kanda yake hadi mara 6 au 7 kwa siku, pamoja na kuanzisha huduma mbalimbali za kijamii, hasa kwa maskini, hadi alipofariki huko Amatrice mwaka 1612.

Alitangazwa na Papa Klementi XII kuwa mwenye heri tarehe 22 Juni 1737, halafu Papa Benedikto XIV alimtangaza mtakatifu tarehe 29 Juni 1746.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Giuseppe Maria Guglielmi, S. Giuseppe da Leonessa predicatore cappuccino in Otricoli. Appunti e memorie, Roma, Tipografia arte e lavoro, 1919.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.