Antigua na Barbuda
Antigua na Barbuda ni nchi ya visiwani ya Amerika kwenye bahari ya Karibi. Ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Each Endeavouring, All Achieving (Jaribu kila kitu, Faulu kila kitu) | |||||
Wimbo wa taifa: Fair Antigua, We Salute Thee (Antigua mzuri twakusalimu) Wimbo wa kifalme: God Save the Queen1 | |||||
Mji mkuu | Saint John's | ||||
Mji mkubwa nchini | Saint John's | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Ufalme wa Kikatiba Charles III wa Uingereza Rodney Williams Gaston Browne | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
1 Novemba 1981 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
440 km² (ya 182) -- | ||||
Idadi ya watu - 2020 kadirio - Msongamano wa watu |
100,772 (ya 182) 186/km² (57) | ||||
Fedha | East Caribbean dollar (XCD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AST (UTC-4) ADT (UTC-3) | ||||
Intaneti TLD | .ag | ||||
Kodi ya simu | +268
- | ||||
1 God Save The Queen ni kama wimbo la taifa lakini hutumiwa tu kwenye nafasi za kifalme. |
Inaundwa na visiwa viwili vya Antigua na Barbuda vinavyokaliwa na watu pamoja na visiwa vingine vidogo kama cha Redonda visivyo na wakazi.
Antigua na Barbuda ni sehemu ya funguvisiwa la Antili Ndogo pamoja na Guadeloupe, Dominica, Martinique, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadini, Barbados, Grenada, Trinidad na Tobago upande wa kusini halafu Montserrat, Saint Kitts na Nevis, Saint Barthélemy, Saint Martin na Anguilla upande wa magharibi.
Watu
haririIdadi ya wakazi ni watu 100,772 (2020). Wengi wao hukaa Antigua. Barbuda ina watu 1,638 tu.
Walio wengi sana (91 %) wametokana na watumwa kutoka Afrika waliopelekwa hapa wakati wa ukoloni, lakini kuna mchanganyiko mkubwa wa damu.
Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wengi wanazungumza Krioli na 10,000 hivi Kihispania, hasa wahamiaji.
Upande wa dini, 92.7% ni Wakristo, hasa Waanglikana (17.6%), wakifuatwa na Waadventista Wasabato, Wapentekoste, Wamoravian, Wamethodisti, Wakatoliki, Wabaptisti n.k. Wengine ni Rastafari (3.6%), Baha'i (1.1%) n.k.
Utawala
haririNchi hufuata utaratibu wa ufalme wa Kikatiba. Mkuu wa dola ni mfalme Charles III wa Uingereza anayewakilishwa na Gavana Mkuu.
Serikali imo mikononi mwa waziri mkuu anayetegemea kura za bunge.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Antigua na Barbuda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |