Katarina wa Uswidi

Katarina wa Uswidi (kwa Kiswidi: Katarina Ulfsdotter au Katarina av Vadstena) (1332 hivi - 24 Machi 1381) alikuwa mwanamke wa ukoo bora wa Uswidi ambaye anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sanamu ya Mt. Katarina, Trönö Old Church.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Machi[1].

Maisha hariri

Katarina alikuwa binti Ulf Gudmarsson, Mtawala wa Ulvåsa, na mama yake alikuwa mtakatifu Birgita wa Sweden.[2]

Akiwa na umri wa miaka 12/13, aliolewa na Eggert van Kyren, lakini alimfanya akubali waishi kama kaka na dada.[2] Mwaka 1349 aliongozana na mama yake kuhiji Roma, na huko aliarifiwa kifo cha mume wake.

Alibaki na mama na kuongozana naye katika safari zake hadi Nchi Takatifu. Birgita alipofariki, Katarina alirudi Uswidi na maiti akimzika katima monasteri kubwa ya Vadstena[3] iliyoanzishwa na marehemu, akawa abesi[2] akijitahidi kulea jumuia kufuatana na kanuni ya mama yake. Ndiyo sababu huo "Utawa wa Mwokozi Mtakatifu" ukajulikana kama Wabirgita.

Miaka kadhaa baadaye alirudi Roma ili kushughulikia suala la mama yake kutangazwa mtakatifu. Akiishi huko miaka 5 alifunga urafiki mkubwa na Katerina wa Siena.[3]

Mwaka 1484, Papa Inosenti VIII aliruhusu Katarina pia aheshimiwe kama mtakatifu na sikukuu yake ilipangwa tarehe 22 Machi. Mwaka 1488, Papa huyohuyo aliruhusu masalia yake yahamishiwe Vadstena.

Kutokana na Matengenezo ya Kiprotestanti, kesi ya kawaida ya kumtangaza mwenye heri, halafu mtakatifu haijakamilishwa.[4][5]

Maandishi hariri

Aliandika kitabu Faraja ya Roho (kwa Kiswidi cha wakati ule Siælinna tröst), ambacho nakala moja ya mwaka 1407 ipo hadi leo.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum
  2. 2.0 2.1 2.2 Kirsch, Johann P. (1908). "St. Catherine of Sweden". In The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. Retrieved 21 February 2014.
  3. 3.0 3.1 Stevens, Clifford. Nakala iliyohifadhiwa. The One Year Book of Saints. Our Sunday Visitor Publishing. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-12-02. Iliwekwa mnamo 21 February 2014. Hosted at EWTN.com.
  4. http://findarticles.com/p/articles/mi_m2386/is_1999_Annual/ai_55983644/?tag=content;col1
  5. "Katarina Ulfsdotter". Nordisk Familjebok (1910). pp. 1281–1283. Retrieved on 21 February 2014. (in Swedish)

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.