Morogoro (mji)

(Elekezwa kutoka Mji wa Morogoro)


Morogoro ni mji mkubwa mmojawapo nchini Tanzania, uliopo takriban kilomita 200 upande wa magharibi wa Dar es Salaam, ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Morogoro.

Mji wa Morogoro
Mji wa Morogoro is located in Tanzania
Mji wa Morogoro
Mji wa Morogoro

Mahali pa mji wa Morogoro katika Tanzania

Majiranukta: 6°49′12″S 37°39′36″E / 6.82000°S 37.66000°E / -6.82000; 37.66000
Nchi Tanzania
Mkoa Morogoro
Wilaya Morogoro Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 471,409
Morogoro mjini
Milima ya Uluguru nyuma ya mji wa Morogoro.
Mashamba ya mkonge karibu na mji wa Morogoro (Milima ya Uluguru inaonekana nyuma.
Kiwanja cha Jamhuri

Mji wa Morogoro una Msimbo wa Posta namba 67100.

Kulingana na sensa iliyofanyika mwaka 2012, idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 315,866. Mwaka 2022 walihesabiwa 471,409 [1].

Mji uko chini ya milima ya Uluguru, kwenye kimo cha mita 500 hivi juu ya usawa wa bahari.

Jina lake linatokana na mto Morogoro unaopitia katikati ya mji.

Morogoro ni njiapanda ya barabara muhimu za Dar es Salaam - Mbeya na Dar es Salaam - Dodoma zinazokutana hapa.

Pana pia kituo cha reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, Mwanza na Kigoma. Reli ya TAZARA hupita mbali kidogo, katika kijiji cha Kisaki, wilaya ya Morogoro vijijini.

Awamu ya kwanza ya reli ya SGR Tanzania ilipangwa kuunganisha Dar es Salaam na Morogoro kufikia mwaka 2020.

Ni kitovu cha viwanda vya mazao na mahali pa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, Chuo Kikuu Kishirikishi cha Jordan n.k.

Morogoro ni mji ujulikanao kwa muziki wa Kitanzania. Kwanza kabisa ilikuwa makao ya bendi maarufu ya Cuban marimba band chini ya mwanzilishi wake Salum Abdallah, mzaliwa wa mji huo. Makao makuu ya bendi hiyo yalikuwa Kichangani, mjini Morogoro. Nyimbo za santuri nyingi za miaka ya 1950 na 1960 zilitungwa mjini humo. Mji huo ulikuwa makao ya bendi nyingine ya Moro jazz. Mwaka 1968, Mbaraka Mwinshehe, mwanamuziki mashuhuri wa Morogoro aliiwakilisha Tanzania kwenye maonyesho ya ulimwengu ya biashara yaliyokuwa mjini Osaka, Japan, na baada ya kurudi kwake alitunga wimbo uliokuwa maarufu nchini wa maonyesho hayo. Mbaraka alifariki kwa ajali ya gari mjini Mombasa, Kenya.

Mji wa Morogoro unajulikana pia kwa klabu za mchezo wa mpira. Wapenda mchezo huo watamkubuka mchezaji wa timu ya taifa Gibson Sembuli ambaye alikuwa mchezaji maarufu wa timu ya klabu ya Yanga.

Eye Care Foundation umejenga hospitali nne za macho hapa.

Mbunge wa Morogoro Mjini ni Abdulaziz Mohamed Abood (CCM).

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Kata za Wilaya ya Morogoro Mjini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Bigwa | Boma | Chamwino | Kauzeni | Kichangani | Kihonda | Kihonda Maghorofani | Kilakala | Kingo | Kingolwira | Kiwanja cha Ndege | Luhungo | Lukobe | Mafiga | Mafisa | Magadu | Mazimbu | Mbuyuni | Mindu | Mji Mkuu | Mji Mpya | Mkundi | Mlimani | Mwembesongo | Mzinga | Sabasaba | Sultan Area | Tungi | Uwanja wa Taifa


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morogoro (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.