Mkataba wa Tordesillas

Mkataba wa Tordesillas wa mwaka 1494 ulikuwa mapatano kati ya Ufalme wa Kastilia (mtangulizi wa Hispania) na Ureno kuhusu ugawaji wa maeneo yaliyogunduliwa katika safari za upelelezi kwenye bahari Atlantiki. Mara nyingi mkataba huu unaitwa pia "mkataba wa ugawaji wa dunia" kati ya milki hizo mbili.

Mistari ya ugawaji ya Tordesillas na Zaragossa

Mapatano yaligawa maeneo yaliyogunduliwa nje ya Ulaya kwenye mstari wa kilomita 2,200 upande wa magharibi wa Visiwa vya Kanari. Mstari huo ulikuwa takriban katikati ya Visiwa vya Kabo Verde vilivyotawaliwa na Ureno na visiwa vipya vilivyogunduliwa na Kristoforo Kolumbus katika Karibi. Maeneo upande wa mashariki ya mstari huo yalitolewa kwa Ureno na maeneo upande wa magharibi yalitolewa kwa Hispania.

Historia ya mapatano hayo ilianza kwa teknolojia mpya ya jahazi iliyowaruhusu kwanza Wareno kusafiri kwenye Atlantiki hata mbali na pwani na kufikia Rasi ya Tumaini Jema, kusini kabisa mwa Afrika kwenye mwaka 1493. Wahispania waliwafuata katika teknolojia na hapo Kolumbus alirudi mwaka 1493 kutoka safari yake ya Amerika akiamini alifika kwenye visiwa vya Asia ya mashariki.

Nchi zote mbili zilitaka kuepukana na ugomvi kati yao na ziliwahi kumwomba Papa wa Kanisa Katoliki atoe uamuzi jinsi gani kushughulikia maeneo mapya yaliyogunduliwa na kutembelewa na meli zao.

Baada ya azimio la kwanza la Papa Alexander VI, mfalme wa Ureno hakuridhika nalo, kwa hiyo mabalozi wa pande zote mbili walikutana katika mji wa Tordesillas, Hispania, wakapatana kuhamisha mstari kwenda magharibi zaidi.

Tokeo moja la uhamisho huu lilikuwa ya kwamba Wareno walifika maeneo yaliyoitwa baadaye Brazil kama eneo lao, wakaunda huko koloni na hivyo Brazil ni nchi inayotumia lugha ya Kireno hadi leo, tofauti na sehemu kubwa ya Amerika ya Kusini ambako lugha kuu ni Kihispania.

Mkataba wa Tordesillas ulifuatwa baadaye na mkataba wa Zaragoza wa mwaka 1529. Hadi wakati ule Wahispania na Wareno walikuwa wamefika tayari katika Bahari Pasifiki; wakitaka kuepukana na ugomvi huko pia kwa kupatana tena mstari wa longitudo fulani kugawana maeneo.

Mistari hii ilikuwa muhimu kama msingi wa makoloni ya nchi zote mbili. Hata hivyo nchi nyingine za Ulaya na Asia hazikujali mapatano hayo; hasa nchi zilizoweza pia kusafiri baharini na kuwa upande wa madhehebu mapya ya Uprotestanti (Uingereza, Uholanzi) zilipuuza madai yote ya Hispania na Ureno.

Kujisomea

hariri
  • Edward G. Bourne, 'The History and Determination of the Line of Demarcation by Pope Alexander VI, between the Spanish and Portuguese Fields of Discovery and Colonization', American Historical Association, Annual Report for 1891, Washington, 1892; Senate Miscellaneous Documents, Washington, Vol.5, 1891–92, pp. 103–30.
  • James R Akerman, The Imperial Map (Chicago: University of Chicago Press, 2009) 138.
  • Leonard Y. Andaya, The world of Maluku: Eastern Indonesia in the early modern period (Honolulu: University of Hawaii Press, 1993, ISBN 0-8248-1490-8.
  • Emma Helen Blair, ed., The Philippine Islands, 1493-1803 (vol 1 of 55) (Cleveland, Ohio: 1903-1909), containing complete English translations of both treaties and related documents.
  • Stephen R. Bown, 1494: How a family feud in medieval Spain divided the world in half (New York: Thomas Dunne Books, 2012) ISBN 978-0-312-61612-0.
  • Charles Corn, The Scents of Eden, (New York: Kodansha, 1998), ISBN 1-56836-202-1.
  • Cortesao, Armando (1939). "Antonio Pereira and his map of circa 1545". Geographical Review. 29: 205–225. doi:10.2307/209943.
  • Frances Gardiner Davenport, ed., European Treaties bearing on the History of the United States and its Dependencies to 1648 (Washington, DC: Carnegie Institution of Washington, 1917/1967).
  • Henry Harrisse, The Diplomatic History of America: Its first chapter 1452—1493—1494 (London: Stevens, 1897).
  • Knowlton, Edgar C. (1963). "China and the Philippines in El Periquillo Sarniento". Hispanic Review. 31: 336–347. doi:10.2307/472212.

Viungo vya Nje

hariri
hariri
 
WikiMedia Commons