Orodha ya vitabu vya Biblia


Vitabu vya Biblia ya Kikristo vilivyoorodheshwa hapa chini ni vile 66 tu vinavyotambuliwa na Wakristo wote. Zingatia lakini kwamba walio wengi, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki, katika Biblia wanavyoitumia wana vitabu vingine 7 vinavyoitwa Deuterokanoni, navyo vyote vimo katika Agano la Kale: Yoshua Bin Sira, Kitabu cha Hekima, Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo, Kitabu cha pili cha Wamakabayo, Tobiti, Yudithi, Baruku.

Biblia ikiwa imefunguliwa.

Majina ya vitabu yameandikwa hapa kufuatana na tafsiri ya Kiswahili cha kisasa maarufu kama Habari Njema. Kama kuna jina lingine limeongezeka katika mabano.


Agano la KaleEdit

Vitabu vya kihistoriaEdit

Mwanzo (Kitabu cha Kwanza cha Musa)
Kutoka (Kitabu cha Pili cha Musa)
Walawi (Kitabu cha Tatu cha Musa)
Hesabu (Kitabu cha Nne cha Musa)
Kumbukumbu la Sheria (Kumbukumbu la Torati; Kitabu cha Tano cha Musa)
Yoshua
Waamuzi
Ruthu (Kitabu cha Ruthi)
Samueli I
Samueli II
Wafalme I
Wafalme II
Mambo ya Nyakati I
Mambo ya Nyakati II
Ezra
Nehemia (Kitabu cha Pili cha Ezra)
Esta

Vitabu vya hekimaEdit

Yobu (Kitabu cha Ayubu)
Zaburi
Methali
Mhubiri
Wimbo Ulio Bora
Maombolezo (Maombolezo ya Yeremia)

Vitabu vya kinabiiEdit

Isaya
Yeremia
Ezekieli
Danieli
Hosea
Yoeli
Amosi
Obadia
Yona
Mika
Nahumu
Habakuki
Sefania
Hagai
Zekaria
Malaki


Agano JipyaEdit

Vitabu vya kihistoriaEdit

Injili ya Mathayo
Injili ya Marko
Injili ya Luka
Injili ya Yohane (Injili ya Yohana)
Matendo ya Mitume

Barua za PauloEdit

Barua kwa Waroma (Waraka kwa Warumi)
Barua ya Kwanza kwa Wakorintho
Barua ya Pili kwa Wakorintho
Barua kwa Wagalatia
Barua kwa Waefeso
Barua kwa Wafilipi
Barua kwa Wakolosai
Barua ya Kwanza kwa Wathesalonike
Barua ya Pili kwa Wathesalonike
Barua ya Kwanza kwa Timotheo
Barua ya Pili kwa Timotheo
Barua kwa Tito
Barua kwa Filemoni

Barua nyingineEdit

Barua kwa Waebrania
Barua ya Yakobo
Barua ya Kwanza ya Petro
Barua ya Pili ya Petro
Barua ya Kwanza ya Yohane
Barua ya Pili ya Yohane
Barua ya Tatu ya Yohane
Barua ya Yuda

Kitabu cha kinabiiEdit

Ufunuo (Ufunuo wa Yohane)

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Orodha ya vitabu vya Biblia kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.