Richard wa Chichester

Richard wa Chichester (1197 - Dover, 3 Aprili 1253) alikuwa askofu wa Uingereza ambaye alipigania adhimisho la ekaristi lifanyike kwa heshima, sakramenti zitolewe bure kwa waamini na makasisi washike vema useja kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.

Sanamu ya Mt. Richard mbele ya kanisa kuu la Chicester.
Kanisa kuu la Chicester (la Mt. Richard wa Chichester).

Papa Urban IV alimtangaza kuwa mtakatifu tarehe 22 Januari 1262.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha hariri

Kijana hariri

Ujanani alitakiwa kufanya kazi nzito ili kutegemeza familia yake. Baadaye aliweza kwenda masomoni kwenye chuo kikuu cha Oxford, chini ya Edmund Rich na Grosseteste, halafu Paris (Ufaransa) na Bologna (Italia).

Katibu mkuu wa jimbo hariri

Akiwa na umri wa miaka 38 akarudi Oxford, alipochaguliwa mara awe gombera wa chuo kikuu, lakini mwaka 1237 mwalimu wake wa zamani Rich, kisha kuchaguliwa Askofu mkuu wa Canterbury, alimtaka awe katibu mkuu wa jimbo lake; katika kazi hiyo alijitokeza katika jitihada za kurekebisha mwenendo wa mapadri na kupinga uvamizi wa serikali katika mamlaka ya Kanisa.

Padri hariri

Aliposhuhudia kifo cha askofu wake huko Soissy, Ufaransa, mwaka 1240, na kuachiwa kikombe cha Misa kama urithi, aliamua kuingia upadri akaenda kusomea teolojia miaka miwili kwa Wadominiko wa Orléans.

Baada ya kupadirishwa mwaka 1242 akiwa na miaka 45, akarudi Uingereza na kufanya kazi ya paroko Charing na Deal (mkoa wa Kent), lakini akarejeshwa mapema katika ukatibu mkuu.

Askofu hariri

Mwaka 1244 alichaguliwa na maaskofu kuongoza jimbo la Chichester, lakini mfalme Henry II alimtaka Richard Passelewe, hivyo akazuia mali na mapato ya jimbo.

Papa Inosenti IV alipoombwa usuluhisho alimtibithisha na kumweka wakfu mwaka 1245 huko Lyons.

Askofu mpya aliporudi Chichester, alilazimika kuishi kifukara katika nyumba ya paroko wa Tarring (Sussex), akifanya kazi za mikono na kutembelea jimbo lote kwa miguu. Miaka miwili baadaye mfalme Henry III alilazimishwa na Papa kulirudishia jimbo mali zote.

Matendo ya upendo hariri

Richard alikuwa mkarimu sana kwa fukara na mpole kwa wakosefu. Alitunga sheria za jimbo, ambazo zinadumu hadi leo, kuhusu masuala mbalimbali.

Kifo hariri

Akiwa Dover ili kumjengea kanisa hayati mwalimu wake Edmund Rich, aliugua sana akafa tarehe 3 Aprili 1253.

Sala yake hariri

Asante kwako, Bwana wangu Yesu Kristo, kwa fadhili zote ulizonistahilia.

Kwa mateso na matusi yote uliyoyavumilia kwa ajili yangu.

Mkombozi, rafiki na kaka mwenye huruma nyingi, naomba niweze kukufahamu wazi zaidi, kukupenda kwa hisani zaidi, kukufuata kwa karibu zaidi, siku kwa siku.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. Martyrologium Romanum