Tetekuwanga
Tetekuwanga, tetewanga au tetemaji (kwa Kiingereza chickenpox, kitaalamu varicella) ni ugonjwa wa kuambukiza sana unaosababishwa na maambukizo ya kimsingi ya virusi vya varisela zosta (VZV).[1] Kwa kawaida huanza kwa vipele vya lengelenge kwenye ngozi, hasa mwilini na kichwani wala si pembeni, na hugeuka kuwa makovu mabichi, yanayowasha, ambayo aghalabu hupona bila kuacha mabaka.
Tetekuwanga | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Infectious diseases, pediatrics |
ICD-10 | B01. |
ICD-9 | 052 |
DiseasesDB | 29118 |
MedlinePlus | 001592 |
eMedicine | ped/2385 derm/74, emerg/367 |
MeSH | C02.256.466.175 |
Tetekuwanga huenea kwa urahisi kwa njia ya ukohozi au kwenda chafya au kuingiliana moja kwa moja na watu wanaougua walio na vipele vinavyovuja. Baada ya maambukizi ya mwanzo, kwa kawaida, kinga ya kudumu maisha hujengeka dhidi ya matukio ya baadaye ya uambukizwaji tetekuwanga.
Tetekuwanga ni nadra kuua, ingawa kwa ujumla huwa kali zaidi kwa watu wazima wa kiume kuliko wanawake ama watoto. Wanawake wajawazito na wale wenye mfumo wa kingamaradhi uliopunguka huwa katika hatari zaidi ya kutatizika pakubwa.
Tetekuwanga kwa sasa inaaminika kuwa sababu ya theluthi moja ya matukio ya kiharusi kwa watoto.[2] Tatizo la kawaida zaidi kutokana na matukio ya tetekuwanga ya baadaye ni vipele, vinavyosababishwa na muathiriko mpya wa virusi vya varisela zosta baada ya miongo tokea matukio ya awali ya tetekuwanga.
Tetekuwanga imeonekana pia katika viumbehai wengine, wakiwa pamoja na tumbili[3] na masokwe.[4]
Dalili na ishara
haririTetekuwanga ni ugonjwa wa kuambukiza sana ambao huenea kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia maingiliano ya moja kwa moja au kwa njia ya hewa kutokana na ukohozi ama upigaji chafya wa mtu aliyeambukizwa. Kugusa majimaji ya malengelenge pia kunaweza kueneza ugonjwa. Mtu aliye na tetekuwanga anaweza kuambukiza tokea siku moja hadi tano kabla ya vipele kujionyesha.[5] Kipindi cha uambukizi huendelea hadi malengelenge yote kugeuka vigaga, ambavyo vinaweza kuchukua siku 5-6 kabla ya kutoweza tena kuambukiza.[6]
Inachukua siku 10-21 kwa mtu kupata tetekuwanga baada ya maingiliano na mtu aliyeambukizwa. Tetekuwanga mara nyingi hudhihirika kama prodromu ya anoreksia, mialgia, kichefuchefu, homa, kuumwa kwa kichwa, maumivu ya koo, masikioni, malalamiko ya shinikizo kichwani au kuvimba uso, na unyonge kwa vijana waliobalehe na watu wazima, ilhali katika watoto, dalili za mwanzo kwa kawaida huwa kutokea kwa vipele vibivu, vikifuatiwa na kuanza kwa unyonge, homa (joto la mwili la °C 38 (°F 100), ingawa zinaweza kufikia kiwango cha juu °C 42 (°F 108) kwa nyakati adimu), anoreksia. Ni kwa nadra, ambapo kikohozi, rhiniti, maumivu ya tumbo, na dhiki za utumbo zimeripotiwa katika wagonjwa wa varisela. Kwa kawaida, ugonjwa huu ni sugu zaidi kwa watu wazima.[7]
Utambuzi
haririUtambuzi wa varisela kimsingi ni wa kimatibabu, ambazo kikawaida huanza kwa "dalili" za mapema za prodroma, na kisha vipele vya kawaida. Thibitisho la utambuzi linaweza kupatikana ama kwa njia ya uchunguzi wa majimaji ya ndani mwa vilengelenge vya upele, au na upimaji damu kwa ushahidi wa hali sugu ya ukingaji wa kujibia.
Maji ya malengelenge yanaweza kuchunguzwa kwa Tsanck smear, au hata kwa uchunguzi wa moja kwa moja wa vikinga-mwili vinavyojichochea. Maji hayo yanaweza pia "kuchachwa", ambapo majaribio hufanywa kukuza na virusi kutokana na sampuli ya maji. Vipimo vya damu vinaweza kutumika kubainisha upokevu na makabiliano ya mwili na maambukizi sugu (IgM) au maambukizi ya awali na kinga ya baadaye (IgG).[8]
Utambuzi wa maambukizi ya varisela katika mimba kabla ya kuzaliwa unaweza kufanywa kwa upimaji wa sauti zisizosikika, ingawa uchelewaji wa wiki 5 tokea aambukizwapo mwanzoni mama mjamzito hakupendekezwi. Majaribio ya PCR (DNA) maji ya kifuko cha mimba pia yanaweza kufanywa, ingawa hatari ya mimba kutoka yenyewe kutokana na utaratibu wa amniosentesi huwa kubwa zaidi kuliko hatari ya mtoto kupata dalili za varisela ya kijusi.[9]
Uenezi
haririVarisela ya mwanzo ni ugonjwa unaoenea sana. Matukio ya varisela hutokea wakati wowote katika mwaka, lakini hasa katika majira ya baridi na ya kuchipua. Varisela ni moja ya magonjwa ya kawaida ya utotoni, huku kiwango cha juu cha maambukizi kikiwa katika kundi la umri wa miaka 4-10. Kama Rubela, si kawaida miongoni mwa watoto ambao hawajaanza shule. Varisela kuambukiza sana, kwa kiwango cha 90% katika maingiliano ya karibu. Watu wengi huambukizwa kabla ya utu uzima lakini 10% ya vijana hubakia katika hatari ya kuambukizwa.
Kihistoria, varisela imekuwa ugonjwa unaoathiri zaidi watoto wenye umri wa kabla ya shule na wa umri wa kwenda shule. Kwa watu wazima mabaka huwa meusi na makovu huonekana zaidi kuliko kwa watoto.[10]
Pathofisiolojia
haririMkumbano wa mtoto aliye na afya bora na VZV husababisha kingaglobulini G (IgG), kingaglobulini M (IgM), na A kingaglobulin A (IgA) kingamwili; kingamwili IgG hudumu kwa maisha na hujenga kinga. Majibu ya kinga yanayozalika kwa seli pia ni muhimu katika kukwaza ueneaji na muda wa maambukizi ya varisela ya mwanzoni. Baada ya maambukizi ya mwanzo, VZV huaminika kuenea kutoka mukosa na vidonda vya ngozi hadi kwa neva za hisia. VZV basi hubakia katika hali fiche kwenye seli za kifundo cha neva mgongoni kwenye neva za hisia. Kuibuka upya VZV husababisha katika dalili za malengelenge zosta (yaani, vipele), na wakati mwingine Ramsay Hunt aina ya II.
Maambukizi katika ujauzito na utotoni
haririKwa wanawake wajawazito, kingamwili zinazozalika kutokana na chanjo au maambukizi ya awali na kuhamishwa kupitia kwa plasenta na kijusi.[11] Wanawake ambao wana kinga ya tetekuwanga hawawezi kuambukizwa na hawatakiwi kuwa na wasiwasi kuhusu hilo kwao wenyewe au kwa watoto wao wakati wa ujauzito.[12]
Varisela kwa wanawake wajawazito inaweza kusababisha maambukizi ya virusi kupitia plasenta na maambukizi ya kijusi. Maambukizi yakitokea katika wiki 28 za kwanza za ujauzito, yanaweza kusababisha dalili za varisela ya kijusi (pia hujulikana kama dalili za varisela ya kuzaliwa). [13] Athari kwa kijusi zinaweza kuwa mbalimbali, kuanzia usugu wa kutokua kikamilifu kwa vidole miguuni na mikononi hadi kwa uumbikaji mbaya wa tupu ya nyuma na kibofu cha mkojo. Matatizo yanayowezekana ni pamoja na:
- Uharibifu wa ubongo: ensefaliti,[14] mikrosefali, haidrosefali, aplasia ya ubongo
- Uharibifu wa macho: shina la jicho, kifuniko cha jicho, na kilengelenge cha lenzi, mikrophthalmia, ugonjwa wa jicho, korioretiniti, optic kudhoufika kwa jicho
- Madhara mengine ya neva: uharibifu wa mlango wa kizazi, uti wa ukanda wa kiuno , upungufu wa hisi,ukosefu wa hisia za misuli ya ndani, anisokoria dalili za Horner /
- Uharibifu wa mwili: haipoplasia ya peo za juu/chini, mvurugo wa misuli ya mkundu na kibofu
- Ugonjwa wa ngozi (sikatrishia), vidonda vya ngozi, hipopigmenti
Maambukizi ya baadaye katika kipindi cha ujajauzito au mara tu baada ya kuzaliwa hujulikana kama varisela ya utotoni ".[15] Maambukizi ya wajawazito huhusishwa na utoaji mimba kabla kukomaa. Hatari ya mtoto kukumbwa na ugonjwa kutokana na maambukizi uko juu zaidi katika kipindi cha siku 7 kabla ya kuzaliwa hadi siku 7 baada ya kuzaliwa. Mtoto huweza pia kukumbwa na hatari ya virusi vinavyoambukiza kupitia maingiliano na nduguze ama watu wengine walioambukizwa, lakini hilo halitakiwi kuzua shaka, hasa iwapo mama ana kinga. Watoto wanaozaliwa ambao huonyesha dalili wako katika hatari kubwa ya homa ya mapafu na matatizo mengine changamano ya ugonjwa huo.[9]
Vipele
haririBaada ya maambukizi ya tetekuwanga, virusi hubakia katika hali ya ubwete kwenye tishu za neva mwilini. Mfumo wa kingamaradhi hudumisha virusi katika hali ya kudhibitiwa, lakini baadaye maishani, hasa wakati wa utu uzima, vinaweza kuibushwa upya na kusababisha aina tofauti za virusi viitwavyo vipele.[16]
Kuzuia
haririHatua za usafi
haririUenezi wa tetekuwanga unaweza kuzuiwa kwa kuwatenga watu walioathirika. Uambukizaji ni kutokana na mkumbano na majimaji ya mpumuo, au mkumbano wa moja kwa moja na vidonda vya vipele, katika kipindi cha siku tatu kabla ya kuanza kwa vipele, hadi siku nne baada ya kuanza kwa vipele.[17] Kwa hivyo, kujiepusha na ukaribu au maingiliano ya kimwili na watu walioathirika katika kipindi hicho kutazuia maambukizi. Virusi vya tetekuwanga (VZV) vinaweza kukabiliwa na kemikali za kuuwa viini, hasa klorini ya kusafisha (yaani, sodiamu hipokloriti). Pia, kama virusi vyote vilivyogubikwa, VZV huathirika na ukaushaji, joto na sabuni. Kwa hivyo virusi hivi ni rahisi kuua kwa kiasi.
Chanjo
haririChanjo ya varisela ilizotengenezwa kwa mara ya kwanza na Michiaki Takahashi mwaka wa 1974 kutoka kwa uzao wa Oka. Imekuwa ikipatikana Marekani tangu 1995 kama kinga dhidi ya ugonjwa huo. Baadhi ya nchi huhitaji au kutohitaji chanjo ya varisela kabla ya kujiunga na shule ya msingi. Kinga si ya maisha na chanjo zaidi huhitajika miaka mitano baada ya chanjo ya awali.[18] Chanjo ya tetekuwanga si mojawapo katika orodha ya chanjo za kawaida utotoni nchini Uingereza: huko chanjo hii hutolewa tu kwa watu ambao wako katika hatari kubwa ya kupata tetekuwanga.[19]
Tiba
haririIngawa hakujakuwa na tafiti rasmi za kimatibu za kutathmini ufanisi wa kutumia losheni ya kisasa ya kalamini, ambacho ni kizuizi cha kisasa kinachoandaliwa kwa zinki oksidi kama mojawapo ya njia za kawaida zaidi za uzuiaji, ina historia bora ya usalama.[20] Ni muhimu kudumisha usafi bora na kusafisha ngozi kila siku kwa maji moto ili kuzuia maambukizi ya bakteria kwa mara nyingine.[21] Kujikuna pia kunawezakuongeza hatari ya maambukizi ya baadaye.[22] Kuongeza kiasi kidogo cha siki kwenye maji hupendekezwa wakati mwingine. Dawa za kuzuia maumivu zinaweza kumezwa ili kuzuia kuhisi mwasho [23]
Ili kukabiliana na dalili za tetekuwanga, watu kwa kawaida hutumia krimu na loshen kuzuia mwasho. Losheni hizi hazifai kutumika usoni au karibu na macho. Kujipaka kiowevu cha uji wa shayiri pia kunaweza kusaidia kupunguza usumbufu.[24]
Matibabu ya varisela hasa hujumuisha kupunguza dalili, kwa vile hakuna tiba halisi ya hali hii. Hata hivyo, baadhi ya tiba hupatikana kwa minajili ya kupunguza dalili wakati ambapo mfumo wa kingamaradhi husafisha virusi toka mwilini. Kama hatua ya kinga, wagonjwa kwa kawaida hutakiwa kukaa nyumbani wakiwa katika hali ya kuweza kuambukiza ili kuepuka kueneza ugonjwa kwa wengine. Pia, mara kwa mara walioambukizwa hutakiwa kukata kucha zao au kuvaa glovu ili kuzuia kujikuna na kupunguza hatari ya maambukizi kwa mara nyingine.
Hali hii humalizika yenyewe kwa kipindi cha wiki chache lakini wakati huohuo ni lazima wagonjwa wazingatie kwa makini usafi wa binafsi.[25] Upele unaosababishwa na virusi vya varisela zosta huweza hata hivyo kudumu hadi mwezi mmoja, ingawa hatua ya kuambukiza haichukui zaidi ya wiki moja au mbili.[26] Pia, kukaa katika mazingira baridi kunaweza kusaidia kupunguza mwasho kwani joto na jasho huuzidisha. Losheni ya kalamini inaweza kujaribiwa kwa kuwa inaweza kupunguza dalili kutokana na uwezo wake wa kutuliza na kupoza ngozi.
Utatuzi wa kiasili wa tetekuwanga ni pamoja na maji ya pea, magadi ya kuoka, mafuta ya vitamini E, asali, chai mitishamba au karoti na korianda. Inaaminika kwamba mwasho wa ngozi unaweza kupunguzwa kwa kiwango fulani kwa maji ambayo yametumika kupikia mbaazi mbichi.[27] Losheni inayotengenezwa kwa magadi ya kuoka na maji yanaweza kuwekwa kwenye ngozi za wagonjwa kwa sponji ili kupunguza mwasho. Pia, kupaka mafuta ya vitamini E au asali kwa ngozi hudhaniwa kuwa na athari ya uponyaji kwa alama ambazo zinaweza kubakia baada ya maambukizi kutibiwa. Baadhi ya watu wanadai kuwa athari za kutuliza kwa kadri za chai ya kijani zina ufanisi wa kupunguza dalili. Hata hivyo, haijulikani ni kwa kiasi gani tiba hizi za nyumbani zinaweza kwa hakika kusaidia wagonjwa kukabiliana vizuri na maambukizi.
Chanjo ya varisela inapatikana kwa watu ambao wamekumbwa na virusi, lakini bado hawajahisi dalili. Chanjo hii ina ufanisi zaidi ikitolewa kwa muda wa siku tatu hadi siku tano baada ya kuambukizwa. Imeonekana kuwa chanjo ya tetekuwanga inaweza kuzuia au kupunguza dalili katika 90% ya matukio ya kuambukizwa, kama ikitolewa kwa muda wa siku tatu baada ya kukumbana na virusi. Kwa watu ambao wamekumbana na virusi lakini huathirika watumiapo chanjo hii, kuna dawa inapatikana, aitwayo varisela kingaglobulin zosta au VZIG ambayo inaweza kuzuia au kupunguza dalili za baada ya maambukizi. VZIG kimsingi hutolewa kwa watu walio katika hatari ya kupatwa na matatizo kutokana na gharama yake ya juu na kinga ya muda mfupi. Aina hii ya tiba hupendekezwa tu kwa watoto wachanga ambao mama zao wamekumbwa na tetekuwanga siku chache kabla au baada ya kujifungua, watoto walio na lukemia au limfoma, watu wenye mfumo hafifu wa kingamaradhi au wanawake wajawazito. VZIG inapendekezwa kwa muda usiozidi saa 96 baada ya kukumbana na virusi.
Watoto
haririIkiwa asikloviri itaanzishwa kwa saa 24 ya mwanzo wa vipele itapunguza dalili lakini haina athari kwa kiwango cha kutatiza. Kwa sasa basi, matumizi ya asikloviri haipendekezwi kwa watu wenye kinga imara (yaani, watu wenye siha bora, wasio na upungufu wa kinga kwa sasa au wanaotumia tiba za udhibitikinga).[28]
Matibabu ya tetekuwanga kwa watoto hulenga dalili wakati, ambapo mfumo wa kingamaradhi hukabiliana na virusi.[29] Huku watoto wadogo zaidi ya miaka 12 wakikata kucha na kuziweka safi ni sehemu muhimu ya matibabu kwa vile wao huwa hatarini zaidi mwa kukuna malengelenge yao. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 12 lakini kuzidi mwezi mmoja hawafai kupata dawa za kuzuia virusi iwapo hawaugui ugonjwa wowote mwingine ambao unaweza kuwaweka katika hatari ya kupatwa na matatizo.
Ili kuepuka kuishiwa na maji mwilini, unywaji wa kiasi kikubwa cha maji unashauriwa hasa iwapo mtoto atapatwa na homa. Homa au maumivu ya kichwa yanaweza kupunguzwa kwa dawa za kupunguza maumivu kama vile parasetamoli au ibuprofeni. Watoto ambao ni wakubwa kuzidi mwaka mmoja wanaweza kupewa vidonge vya antihistamini au dawa za maji ambazo husaidia wakati ambapo mtoto hawezi kupata usingizi kwa sababu ya kuwashwa.
Asikloviri au kingaglobulini kwa jumla huagizwa kwa watoto walio katika hatari ya kukumbwa na matatizo yatokanayo na tetekuwanga. Wao hupokea matibabu sawa na iliyotajwa hapo juu kuongezea na dawa dhidi ya virusi. Kategoria za watoto wanaoonekana kuwa katika hatari ya kupatwa na matatizo ni pamoja na watoto wachanga wa chini ya umri wa mwezi mmoja, walio na mfumo wa kinga hafifu, wale ambao hutumia steroidi au dawa za kudhibiti kinga au watoto walio na magonjwa sugu ya moyo, mapafu na ngozi. Aidha, watu wazima na vijana huchukuliwa kuwa katika hatari ya kupata matatizo na kwa kawaida hupewa dawa ya kuzuia virusi.
Aspirini haikubaliki sana kwa watoto wadogo wa chini ya miaka 16 kwa vile imekuwa ikihusiana na uwezekano wa hali mbaya na hatari ijulikanayo kama dalili za Reye.
Watu wazima
haririMaambukizi kwa watu wazima ambao kwa kawaida huwa na siha bora huelekea kuwa kali na kuathiri zaidi; matibabu kwa dawa za kuzuia virusi (k.v. asikloviri) hupendekezwa kwa jumla, mradi ianzishwe kwa muda wa saa 24-48 tokea kuanza kwa vipele.[30]
Tiba za kupunguza dalili za tetekuwanga kwa watu wazima kimsingi ni sawa na zinazotumiwa kutibia watoto. Aidha, watu wazima mara nyingi huagiziwa dawa za kuzuia virusi kama kwa vile zina ufanisi katika kupunguza ukali wa hali na uwezekano wa kupatwa na matatizo zaidi. Dawa za kuzuia virusi, hata hivyo, halengwi kuua virusi, bali kukomesha kuongezeka kwa dalili.
Watu wazima pia hushauriwa kuongeza unywaji wa maji ili wasiishiwe na maji mwilini na wapunguze maumivu ya kichwa. Dawa za kuzuia maumivu kama vile parasetamoli na ibuprofeni pia hupendekezwa kwa kuwa zina ufanisi wa kupunguza mwasho na dalili nyingine kama vile homa au maumivu. Dawa za mzio zinaweza kutumika katika hali ambapo dalili husababisha ukosefu wa usingizi, kwa vile zina ufanisi katika kupunguza mwasho na pia kutumika kama kitulizi.
Kama vile katika watoto, dawa za kuzuia virusi huonekana kuwa na umuhimu zaidi kwa watu wazima walio katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo zaidi. Hawa ni pamoja na wanawake wajawazito au watu walio na mfumo hafifu wa kinga.[31]
Sorivudini, ambavyo ni viini vinavyoshabihiana vimeonekana kutoka katika ripoti za matukio machache kuwa na mafanikio katika kutibu matukio ya varisela kwa watu wazima walio na siha bora. Majaribio makubwa ya kimatibabu yanahitajika ili kuonyesha ufanifu wa dawa hii.[32]
Prognosi
haririMuda wa kujitokeza kwa vilengelenge vinavyosababishwa na virusi vya varisela zosta hutofautiana miongoni mwa watoto aghalabu kutoka siku 4 hadi 7, kisha kujitokeza kwa dalili ya malengelenge mapya huanza kupunguka baada ya siku 5. Maambukizi ya tetekuwanga ina hatari ya kadri kwa watoto wadogo, na ya matibabu ya dalili, kwa kujipaka sodiumu bikaboneti au dawa za uzio /1} ili kupunguza mwasho.[33] Parasetamoli (asetaminopheni) hutumika sana kupunguza homa. Aspirini au bidhaa zilizo na aspirini, hazipaswi kutolewa kwa watoto walio na tetekuwanga kwa vile inaweza kusababisha dalili za Reye.[34]
Kwa watu wazima, ugonjwa huo ni kali zaidi,[35], ingawa matukio yake ni machache sana. Maambukizi kwa watu wazima huhusishwa zaidi na vifo kutokana na homa ya mapafu,[36] hepatiti, na ensefaliti.[onesha uthibitisho] kwa hakika, hadi 10% ya wanawake wajawazito walio na tetekuwanga hupata homa ya mapafu, na ukali wake huongezeka baadaye katika kipindi cha ujauzito. Nchini Uingereza na Welsi, 75% ya vifo kutokana na tetekuwanga ni vya watu wazima.[9] Uvimbe wa ubongo, au ensefaliti, unaweza kutokea kwa watu ambao kinga yao imeathiriwa, ingawa kiwango cha hatari huzidishwa na malengelenge ya zosta[37] Fasiiti nekrotizi pia ni tatizo nadra.[38]
Maambukizi ya bakteria kwa vidonda vya ngozi kwa mara nyingine, yanayodhihirika kama impetigo, seluliti, na erisipela, ni matatizo ya kawaida zaidi kwa watoto wenye siha njema. Maambukizi ya varisela ya kimsingi yaliyosambaa ambayo kwa kawaida huonekana kwa watu wenye kinga iliyoathirika yanaweza kuzua kiwango cha juu cha kuugua. Asilimia tisini ya matukio ya nimonia ya varisela hutokea miongoni mwa watu wazima. Matatizo yasiyo ya kawaida ya tetekuwanga iliyosambazwa pia hujumuisha miokaditi, hepatiti, na glomerulonefriti.[39]
Matatizo ya kufuja damu hutokea zaidi kwa watu wenye kinga zilizoathirika au kinga zilizopunguka, ingawa watoto wenye afya bora na watu wazima pia huathirika. Dalili kuu tano za kimatibabu zimeelezwa: purpura febrili, tetekuwanga yenye kudhuru na purpura, purpura baada ya maambukizi, fulminans purpura, na purpura anafilaktoidi. Dalili hizi zina mikondo inayobadilikabadilika, huku purpura febrile ikiwa ndiyo tulivu zaidi kati ya dalili zote ikiwa na matokeo yasiyotatiza. Kinyume na hayo, tetekuwanga tulivu na purpura ni hali hatari za kimatibabu ambayo ina kiwango cha vifo cha zaidi ya 70%. Etiolojia ya dalili hizi za tetekuwanga inayovuja haijulikani.[39]
Historia
haririTetekuwanga ilitambuliwa kwa mara ya kwanza na mwanasayansi Mwislamu wa Kiajemi Muhammad ibn Zakariya ar-Razi (865-925), anayejulikana katika nchi za magharibi kama "Rhazes", ambaye aliitofautisha bayana na ndui na surua.[40]Baadaye Giovanni Filippo (1510-1580) wa Palermo alitoa maelezo ya kina zaidi.
Marejeo
hariri- ↑ Wood MJ (2000). "History of Varicella Zoster Virus". Herpes. 7 (3): 60–65. PMID 11867004.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ http://stroke.ahajournals.org/cgi/content/abstract/32/6/1257
- ↑ Cohen JI, Moskal T, Shapiro M, Purcell RH (1996). "Varicella in Chimpanzees". Journal of Medical Virology. 50 (4): 289–92. doi:10.1002/(SICI)1096-9071(199612)50:4<289::AID-JMV2>3.0.CO;2-4. PMID 8950684.
{{cite journal}}
:|access-date=
requires|url=
(help); Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Myers MG, Kramer LW, Stanberry LR (1987). "Varicella in a gorilla". Journal of Medical Virology. 23 (4): 317–22. doi:10.1002/jmv.1890230403. PMID 2826674.
{{cite journal}}
:|access-date=
requires|url=
(help); Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ "Onset of rashes in infectious disease". lifehugger. 2009-10-14. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-26. Iliwekwa mnamo 2009-10-14.
- ↑ New Zealand Dermatological Society (2006-01-14). "Chickenpox (varicella)". Iliwekwa mnamo 2006-08-18.
- ↑ "General questions about the disease". Varicella Disease (Chickenpox). CDCP. 2001-12-02. Iliwekwa mnamo 2006-08-18.
- ↑ [20] ^ McPherson & Pincus: Utambuzi wa kimatibabu wa Henry na usimizi kwa Njia za Maabara, 21 ed. 2007, Sura ya 54.
- ↑ 9.0 9.1 9.2 Royal College of Obstetricians and Gynaecologists (2007). "Chickenpox in Pregnancy" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2009-07-05. Iliwekwa mnamo 2009-07-22.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ "Epidemiology of Varicella Zoster Virus Infection, Epidemiology of VZV Infection, Epidemiology of Chicken Pox, Epidemiology of Shingles". Iliwekwa mnamo 2008-04-22.
- ↑ Brannon, Heather (2007-07-22). "Chicken Pox in Pregnancy". Dermatology. About.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-27. Iliwekwa mnamo 2009-06-20.
- ↑ "Chickenpox in Pregnancy". March of Dimes. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-19. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
{{cite web}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ Boussault P, Boralevi F, Labbe L, Sarlangue J, Taïeb A, Leaute-Labreze C (2007). "Chronic varicella-zoster skin infection complicating the congenital varicella syndrome". Pediatr Dermatol. 24 (4): 429–32. doi:10.1111/j.1525-1470.2007.00471.x. PMID 17845179. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-05. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help); Unknown parameter|https://archive.today/20130105080133/http://www3.interscience.wiley.com/resolve/openurl?genre=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Matsuo T, Koyama M, Matsuo N (1990). "Acute retinal necrosis as a novel complication of chickenpox in adults". Br J Ophthalmol. 74 (7): 443–4. doi:10.1136/bjo.74.7.443. PMC 1042160. PMID 2378860.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Sauerbrei, Andreas, Wutzler, Peter (Desemba 2001). " Varisela ya utotoni ". Jarida la Perinatolojia (Perinatology). 21 (8): 545-549.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-24. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ [38] ^ Patrick R. Murray et al., Mikrobiolojia ya Utabibu, toleo la 5 (Elsevier), p.551.
- ↑ Chaves SS, Gargiullo P, Zhang JX; na wenz. (2007). "Loss of vaccine-induced immunity to varicella over time". N Engl J Med. 356 (11): 1121–9. doi:10.1056/NEJMoa064040. PMID 17360990.
{{cite journal}}
: Explicit use of et al. in:|author=
(help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ http://www.nhs.uk/conditions/varicella-vaccine/pages/introduction.aspx Ilihifadhiwa 13 Julai 2010 kwenye Wayback Machine. </>
- ↑ Tebruegge M, Kuruvilla M, Margarson I (2006). "Does the use of calamine or antihistamine provide symptomatic relief from pruritus in children with varicella zoster infection?" (Abstract). Arch. Dis. Child. 91 (12): 1035–6. doi:10.1136/adc.2006.105114. PMC 2082986. PMID 17119083.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Domino, Frank J. (2007). The 5-Minute Clinical Consult, 2007. Lippincott Williams & Wilkins. p. 248. ISBN 978-0-7817-6334-9.
- ↑ Brannon, Heather (21 Mei 2008). Matibabu ya Tetekuwanga Ilihifadhiwa 26 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine. . About.com.
- ↑ Gleeson, Rachael. "Chicken Pox - A Guide To Management - From Incubation To Recuperation". NaturalParenting. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-07. Iliwekwa mnamo 2009-06-20.
- ↑ Parmet, Sharon, Lynm, Cassio (18 Februari 2004). Tetekuwanga . Jarida la Shirika la Matabibu la Marekani. 291 (7): 906.
- ↑ "Chickenpox (varicella)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-05. Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Varicella Zoster Virus". Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
- ↑ "Home Remedies for Chicken Pox". Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
- ↑ "BestBets: Should acyclovir be prescribed for immunocompetent children presenting with chickenpox?".
- ↑ "Chickenpox in Children Under 12". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-07-15. Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-07-26. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ "What is chickenpox?". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-07-26. Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
- ↑ "Chickenpox: Treatment & Medication". Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
- ↑ Somekh E, Dalal I, Shohat T, Ginsberg GM, Romano O (2002). "The burden of uncomplicated cases of chickenpox in Israel". J. Infect. 45 (1): 54–7. doi:10.1053/jinf.2002.0977. PMID 12217733.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ US Centers for Disease Control and Prevention. "Varicella Treatment Questions & Answers". CDC Guidelines. CDC. Iliwekwa mnamo 2007-08-23.
- ↑ Jill M Baren MD, Philip L Henneman MD, Roger J Lewis MD, PhD (1996). "Primary Varicella in Adults: Pneumonia, Pregnancy, and Hospital Admissions". Annals of Emergency Medicine. 28 (2): 165–169. doi:10.1016/S0196-0644(96)70057-4. PMID 8759580. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-02-01. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help); Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ http://www.erj.ersjournals.com/cgi/content/abstract/21/5/886
- ↑ "Definition of Chickenpox". MedicineNet.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-07-28. Iliwekwa mnamo 2006-08-18.
- ↑ "Is Necrotizing Fasciitis a complication of Chickenpox of Cutaneous Vasculitis?". atmedstu.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-15. Iliwekwa mnamo 2008-01-18.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help) - ↑ 39.0 39.1 [79] ^ Matatizo ya Tetekuwanga Ilihifadhiwa 28 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Otri AM, Singh AD, Dua HS (2008). "Abu Bakr Razi". The British Journal of Ophthalmology. 92 (10): 1324. PMID 18815419. Iliwekwa mnamo 2009-06-20.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
Viungo vya nje
hariri- Tetekuwanga katika Open Directory Project