Wakristadelfiani
Wakristadelfiani (kutoka jina la Kiingereza "Christadelphians") ni dhehebu dogo la Ukristo lililoanzishwa katika Uingereza na Marekani katika karne ya 19. Jina lilibuniwa na mwanzilishi wake John Thomas aliyeunganisha maneno ya Kigiriki "khristos" (Kristo) na "adelfoi" ("ndugu") kwa maana ya " ndugu wa Kikristo".
Kwa hiyo maana ya jina Kristadelfiani ni 'Ndugu katika Kristo'.
Duniani kote wapo wanachama 55~65,000 hivi.[1]
Imani
haririWakristadelfiani wanadai ya kwamba wanaamini mafundisho yote ya Biblia ambayo ni pamoja na:[2]
- 1. Biblia ndio ujumbepekee na wa kweli kutoka kwa Mungu.
- 2. Kuna Mungu mmoja tu, Baba, aliyeumba dunia na ana kusudi kubwa nayo.
- 3. Roho Mtakatifu ni uwezo (nguvu) wa Mungu mwenyewe, ambao huitumia kufanya mapenzi yake matakatifu.
- 4. Yesu ni mwana wa Mungu. Yeye pia ni mwana wa Adamu kupitia kuzaliwa kwake na Bikira Mariamu.
- 5. Yesu alishinda majaribu yote akafa awaokoe wafuasi wake kutoka kwa dhambi na mauti.
- 6. Yesu alifufuliwa na Mungu kutoka kwa wafu akapaa mbinguni lakini atarudi.
- 7. Wakati atakaporudi atawafufua na kuwahukumu waumini waliokufa na kuwapa kutokufa (uzima wa milele) wale waaminiifu.
- 8. Atakuwa mfalme juu ya ufalme wa Mungu utakaorudishwa Israeli, na juu ya dunia nzima.
- 9. Wafuasi wake ambao watakuwa na miili isiyoweza kufa watamsaidia kuleta haki ya milele na amani duniani kote.
- 10. Ibilisi si kiumbe kisicho cha ulimwengu huu, yaani si malaika lakini ni jina lingine la dhambi iharibiwayo tu katika Kristo.[3]
- 11. Wokovu unahusiana na kufunikwa kwa dhambi kupitia kwa Yesu na uhuru kutoka kwa dhambi na mauti wakati atakaporudi.
- 12. Wakati mtu anapokufa hukoma kuishi. Tumaini pekee ya uhai ni ufufuo wakati Yesu atakaporudi.
- 13. Kuamini katika ahadi za Mungu juu ya ufalme wake na kazi za Yesu Kristo ni muhimu.
- 14. Toba na ubatizo katika Kristo kwa kuzikwa ndani ya maji na ufuasi wa kila siku wa Kristo ni muhimu kwa wokovu hatimaye.
Jamii
haririWatumishi wa Iklezia, yaani (1) Mwenyekiti, (2) Katibu, (3) Mtunza Hazina na (4) Mkaguzi wa Hesabu. Iklezia mpya watahitaji ndugu wanne ili kutenda kazi wakiwa ni watumishi wa Iklezia na kushika kazi mahususi. Watumishi wa Iklezia hawatakiwi kutawala iklezia, bali watende kazi kama watumishi wa Bwana na wa ndugu zao na dada. Hawatakiwi wawe madikteta katika mambo ya Iklezia bali kama watumishi wa Bwana na wa Iklezia. Hawatakiwi kuishi kwa pesa za Iklezia au kujiona wenyewe ni wachungaji au watu wa kuheshimiwa sana kama padri n.k.
Tanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Maswali Yako Yajibiwa Kuhusu Kanisa La Kikristadelfiano (2004) Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Imani yangu (My faith, 1979) Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Mambo yanayohusu imani, ambayo ni msingi wa ushirika wetu (BASF 1898) Archived 19 Juni 2010 at the Wayback Machine.
- Misingi ya Biblia.doc (1993)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wakristadelfiani kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |