Yohane Leonardi ((kwa Kiitalia: Giovanni Leonardi; Diecimo, 1541Roma, 9 Oktoba 1609) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki mjini Lucca (Toscana, Italia).

Mt. Yohane Leonardi.
Mt. Yohane Leonardi.

Huko alianzisha shirika la Wakleri wa Kanuni wa Mama wa Mungu ili kufundisha katekesi kwa watoto, kuleta upyaisho katika utume wa wakleri na kueneza imani ya Kikristo duniani kote. Kwa ajili hiyo alipaswa kukabili tabu nyingi.

Alipolazimika kuhamia Roma, aliweka msingi wa Chuo cha Propaganda Fide akafa kwa amani kwa kuishiwa nguvu na wingi wa kazi zake[1].

Alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri tarehe 10 Novemba 1861, halafu na Papa Pius XI kuwa mtakatifu tarehe 17 Aprili 1938.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Maisha

hariri

Kwanza alifanya kazi kama mfamasia.

Kisha kupewa upadrisho mwaka 1572, alijitosa katika malezi ya vijana parokiani mwake akijiita "Yohane wa Mama wa Mungu".

Mwaka 1574 kama sehemu ya Urekebisho wa Kikatoliki alianzisha kundi lenye juhudi za kiroho la kufundisha imani. Leonardi alitumia kundi hilo kueneza heshima kwa Bikira Maria na desturi ya kuabudu Ekaristi saa arubaini mfululizo.

Baadaye Leonardi alifukuzwa Lucca akahamia Roma akawa rafiki wa Filipo Neri ambaye alimshauri asiende Amerika.

Mwaka 1586 Papa Klementi VIII alimpa kazi ya kurekebisha monasteri za Wabenedikto wa jamii za Monte Vergine, Vallombrosa na Monte Senario.

Baadaye alianzisha na J. Vivès tapo la kimisionari lililozaa seminari ya Uenezaji wa Imani (kwa Kilatini "Propaganda Fide") ambayo baadaye tena ikawa idara ya Papa kwa umisionari.

Alifariki akihudumia wenzake waliougua influenza iliyoenea Roma.

Urithi

hariri

Kundi lake lilikuja kukubaliwa na Papa Paulo V mwaka 1614. Kanuni ya kudumu ilitolewa mwaka 1851.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • "Encyclopédie des Saints et de la Sainteté," Hachette (Kifaransa)

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.